Nimeunganishwa Tena na Bwana

02/12/2019

Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. … Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima(Neno Laonekana katika Mwili). Kifungu hiki cha maneno ya Mwenyezi Mungu kilinifanya nikumbuke imani yangu ya hapo awali. Kwa kuwa nilishikilia mawazo ya kidini na maneno ya Biblia, nilikuwa karibu kuufungia mlango wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Mungu alitumia njia za kushangaza ili niwe na bahati nzuri ya kusikia sauti Yake na kukaribisha kurudi kwa Bwana.

Asubuhi moja miaka michache iliyopita, niliamka mapema sana na nikafungua Biblia iliyokuwa kando ya mto wangu. Nilisoma kuhusu Bwana Yesu kuwakemea Mafarisayo: “Na Yesu akaingia katika hekalu la Mungu, naye akawaondoa wote waliokuwa wakiuza na kununua katika hekalu, naye akaziangusha meza za wabadilishaji wa fedha, na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, na akawaambia, Imeandikwa, nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi; lakini mmeifanya pango la wezi(Mathayo 21:12-13). Nilikuwa na huzuni kidogo wakati huo. Nilihisi kama kwamba hali ya wakati huo ya kanisa haikuwa tofauti na ile ya hekalu mwishoni mwa Enzi ya Sheria. Wachungaji na wazee katika kanisa walikuwa wakisema kila mara kwamba waumini wanapaswa kupendana, lakini wao wenyewe walikuwa kila mara wakiingia katika mabishano ya wivu, na kugombania sadaka. Hata walikubali rushwa kutoka kwa waumini ili wawaombee, na wakati mwingine waliamua wangeomba kwa muda gani kulingana na kiwango cha rushwa walichopata. Washirika wengi wa kanisa walikuwa hasi na dhaifu, na watu wachache walihudhuria mikutano kila siku. Wachungaji na wazee hawakutoa mahubiri yao kwa dhati na hawakutafuta jinsi ya kuchunga kondoo wa Bwana vyema, lakini hawakuchoshwa kamwe na kuongoza harusi za waumini. Mchungaji katika kanisa langu la zamani alikuwa vivyo hivyo pia. Kanisa linapaswa kuwa mahali pa ibada, lakini ilianza kuwa mahali pa kufanyia harusi. Sikuweza kujizuia kuwaza, “Wachungaji na wazee wamepotoka kutoka kwenye njia ya Bwana. Kanisa lilionekana kama la kidunia kabisa. Ni kama tu mwishoni mwa Enzi ya Sheria, wakati ambapo hekalu lilikuwa na ukiwa na likaanza kuwa pango la wezi. Je, Bwana ataonekana katika kanisa la aina hii Atakaporudi?”

King’ora cha simu yangu kililia ghafla nilipokuwa tu nikifikiria hayo, na nilipokizima, niliona pendekezo la video ya YouTube kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilishangazwa sana. Sikuwa nimewahi kujisajili kwenye kituo cha kanisa hilo, kwa hivyo kwa nini nilipata taarifa hiyo? Kisha nikakumbuka kuwa mwezi mmoja uliopita, rafiki yangu alikuwa amenipeleka huko ili niyasikie mahubiri, na yale niliyoyasikia yalikuwa mapya na ya kutia nuru kwa kweli. Kwa kweli nilipata kitu kutoka katika mahubiri hayo. Nilitaka kuendelea kuyachunguza, lakini walishuhudia kwamba Bwana Yesu tayari alikuwa Amerudi, kwamba Alikuwa akifanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho na kuonyesha ukweli mwingi, na kwamba kitabu, Neno Laonekana katika Mwili, kilijaa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu. Walisema kwamba katika mikutano, wote walisoma na kufanya ushirika juu ya maneno ya Mwenyezi Mungu. Sikuweza kuelewa hilo. Wachungaji na wazee walituambia kila mara kwamba maneno na kazi yote ya Mungu yako katika Biblia, na kwamba maneno na kazi Yake hayako nje ya Biblia. Wanawezaje kushuhudia kwamba Bwana alikuwa Amenena maneno mapya? Kwa vyovyote vile, vizazi vya waumini vilikuwa vimetegemeza imani yao kwenye Biblia, kwa hivyo kumwamini Bwana kulikuwa kuiamini Biblia. Je, kitu kingine kinawezaje kuwa kumwamini Bwana? Kila wakati rafiki yangu aliponiomba niende kuyasikia mahubiri mengine zaidi katika kanisa hilo, nilikataa. Kwa hivyo, nilipoona kiunga hicho kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwenye simu yangu, sikukibofya.

Lakini ajabu ni kwamba, kwa siku kadhaa baadaye niliendelea kupata mapendekezo ya YouTube ya filamu na nyimbo za kidini kwenye kituo cha kanisa hilo. Niliwaza, “Sijasajili kwenye kituo chao, lakini naendelea kupata taarifa hizi. Je, Bwana ananielekeza? Je, ni mapenzi ya Bwana kwamba nichunguze kituo cha Kanisa la Njia ya Mwenyezi Mungu?” Nilipofikiria hilo nilimwomba Bwana: “Ee Bwana! Kwa nini video hizi zinaendelea kujitokeza kwenye simu yangu? Zinashuhudia kuwa tayari Umerudi. Je, hiyo ni kweli? Napaswa kutazama video hizi? Bwana, tafadhali niongoze.” Baada ya sala yangu, nilikumbuka maneno haya kutoka kwa Bwana Yesu: “Wamebarikiwa wao walio maskini kiroho: kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao(Mathayo 5:3). Kweli. Kuja kwa Bwana ni jambo muhimu, kwa hivyo niliwaza, ninaposikia kulihusu, napaswa kutafuta kwa unyenyekevu, kulichunguza, na kulifikiria kwa makini ili nione kama kweli Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Nisipotafuta au kulichunguza, na iwe Bwana kwa kweli amerudi, je, sitakosa nafasi yangu ya kukaribisha kuja Kwake? Baada ya kufikiria hayo, niliamua kutazama baadhi ya video za kanisa. Nilipoangalia tovuti ya kanisa hilo, niliona kwamba kulikuwa na maudhui mengi mbalimbali, yakiwa ni pamoja na filamu, video za wimbo, kwaya maalum, na makala yanayohusu matukio na ushuhuda. Video moja ya wimbo, “Mpenzi Wangu, Tafadhali Nisubiri,” Wimbo huo ulinivutia sana. ulikuwa na maneno ambayo yalinigusa sana. Yalinifanya nifikirie wakati wote ambapo nilikuwa katika kanisa lenye ukiwa, nikitafuta kila mahali kanisa ambalo lilikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kadiri nilivyozidi kudurusu wavuti, ndivyo nilivyozidi kupata riziki zaidi kutoka kwayo. Nilitaka kuelewa na kulichunguza kanisa hilo, kwa hivyo nilitafuta filamu nyingine zaidi za kutazama kwenye wavuti yao.

Siku moja nilitazama filamu ya injili ambayo hasa ilihusu uhusiano kati ya Mungu na Biblia. Kulikuwa na kifungu cha maneno ya Mungu ndani ya filamu ile ambayo sitasahau kamwe: “Kuanzia kipindi ambapo kulikuwa na Biblia, imani ya watu kwa Bwana imekuwa imani katika Biblia. Badala ya kusema watu wanamwamini Bwana, ni bora kusema kwamba wanaamini Biblia; badala ya kusema wameanza kusoma Biblia, ni bora kusema wameanza kuamini Biblia; na badala ya kusema wamerudi mbele ya Bwana, ingekuwa vyema kusema wamerudi mbele ya Biblia. Kwa njia hii, watu wanaiabudu Biblia kana kwamba ni Mungu, kana kwamba ni damu yao ya uzima na kuipoteza itakuwa ni sawa na kupoteza maisha yao. Watu wanaitazama Biblia kuwa ni kuu kama Mungu, na hata kuna wale wanaoiona kuwa ni kuu kuliko Mungu. Kama watu hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ikiwa hawawezi kuhisi Mungu, wanaweza kuendelea kuishi—lakini punde tu watakapoipoteza Biblia, au kupoteza sura na maneno maarufu sana kutoka katika Biblia, basi inakuwa ni kana kwamba wamepoteza maisha yao. … Watu wengi hawaelewi kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu, wala jinsi ya kumwamini Mungu, na hawafanyi chochote zaidi ya kutafuta kiupofu dondoo ili kufasiri sura za Biblia. Watu hawajawahi kufuata mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu; muda wote huo, hawajafanya chochote, bali kujifunza na kuchunguza Biblia kwa papara, na hakuna hata mmoja ambaye amepata kazi mpya ya Roho Mtakatifu nje ya Biblia, hakuna ambaye amewahi kujitenga na Biblia, wala kuthubutu kujitenga na Biblia(Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kutazama sehemu hii, niliwaza, “Huo hasa ndio mtazamo wangu kwa Biblia. Nahisi kama kwamba inamwakilisha Bwana, kwamba kumwamini Yeye ni kuiamini Biblia, na mawili hayo hayawezi kutenganishwa. Lakini kile ambacho sielewi ni hiki: Biblia ni ushuhuda wa Bwana na msingi wa imani yetu. Kama Wakristo, tumetegemeza imani yetu kwenye Biblia kwa miaka elfu mbili, kwa hivyo inaweza kweli ikawa kwamba hii haikubaliani na mapenzi ya Bwana? Nini kinaendelea hapa kwa kweli?”

Niliendelea kutazama filamu ile, nikitamani maswali haya yajibiwe. Mhusika aliyeshiriki injili alisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia(Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma maneno haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu, waliendelea na ushirika. Walisema kwamba watu wote wa imani hufikiri kwamba kumwamini Bwana ni kuiamini Biblia, vinginevyo, si kumwamini Bwana, lakini maoni haya si sahihi. Walisema pia, “Bwana Yesu alipokuwa akihubiri na kufanya kazi, wafuasi Wake waliondoka kwenye Maandiko ili kukubali kazi na maneno Yake, kwa hivyo tunaweza basi kusema kwamba kweli hawakuwa waumini wa Bwana? Mafarisayo wote wa Uyahudi walishikilia Maandiko, lakini walimsulibisha Bwana Yesu, ambaye alionyesha ukweli na kufanya kazi ya ukombozi. Tatizo lilikuwa gani hapo? Je, kushikilia Maandiko kunamaanisha kwamba mtu anamjua Bwana? Je, kunamaanisha kuwa yeye hufuata njia ya Bwana, na kwamba anamcha na kumtii? Mungu ndiye Bwana wa uumbaji, chanzo cha uzima wa vitu vyote, wakati Biblia ni rekodi tu ya kazi na maneno ya zamani ya Mungu. Inawezaje kusawazishwa na Mungu? Waumini wa Bwana huiamini na kuiabudu Biblia kwa upofu na kuichukulia kuwa sawa na Mungu, na hata wanabadilisha nafasi ya Bwana na kazi Yake na Biblia. Je, huko si kumshushia Bwana thamani na kumkufuru? Je, mtu anayeishikilia Biblia bila kutafuta kuonekana kwa Bwana na kazi Yake kweli ni muumini au mfuasi wa Bwana? Hivi ndivyo Bwana Yesu alivyowaambia Mafarisayo: ‘Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai(Yohana 5:39-40). Alisema pia: ‘Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu(Yohana 14:6). Bwana Yesu alieleza waziwazi kuhusu uhusiano kati ya Mungu na Maandiko. Maandiko yanamshuhudia tu Mungu—hayamwakilishi Bwana, wala hayawezi kuchukua nafasi ya kazi Yake ya wokovu. Kuishikilia Biblia pekee hakuwezi kutuletea uzima wa milele. Kristo pekee ndiye njia, ukweli na uzima. Ili kupata uzima, lazima tumtafute Bwana!”

Niliguswa sana baada ya kumaliza kutazama filamu hiyo. Nilihisi kwamba yote yaliyosemwa yalikuwa sahihi na yalilingana na maneno ya Bwana Yesu. Nilitambua kuwa Biblia kwa kweli haimwakilishi Bwana. Yeye ndiye Anayetupa uzima, si Biblia. Kuiamini si sawa na kumwamini na kumfuata Bwana! Lakini nilifikiri siku zote kuwa Biblia ilimwakilisha Yeye. Je, sikuwa nimeichukulia Biblia kuwa ya juu kuliko Bwana? Kadiri nilivyozidi kufikiria hilo, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba kulikuwa na ukweli katika maneno ya Mwenyezi Mungu, kwamba yanaweza kutatua mkanganyiko wangu. Nilijua kwamba nilihitaji kutafuta kwa makini na kuchunguza ili nisikose fursa yangu ya kumkaribisha Bwana. Kisha niliamua kurudi katika Kanisani la Mwenyezi Mungu pamoja na rafiki yangu. Ndugu wote walitupokea kwa ukunjufu tulipofika kanisani na wakashiriki nasi kwa uvumilivu sana. Niliwaeleza mkanganyiko wangu, nikisema, “Wachungaji na wazee hutuambia kila wakati katika mikutano kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yako katika Biblia, na kwa hivyo kitu chochote ambacho kiko nje ya Biblia hakiwezi kuwa na kazi au maneno Yake. Lakini mnashuhudia ya kuwa Bwana Yesu amerudi kama Mwenyezi Mungu na kwamba Anafanya kazi mpya katika siku za mwisho, na kuonyesha maneno mapya. Je, nini kinaendelea kwa kweli?”

Dada Zhou alisoma vifungu vichache vya maneno ya Mwenyezi Mungu ili kujibu. “Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria?” “Yote yaliyoandikwa katika Biblia ni machache na hayawezi kuwakilisha kazi yote ya Mungu. Injili Nne zina chini ya sura mia moja zote pamoja ambamo mliandikwa mambo yale yaliotendeka yanayohesabika, kwa mfano Yesu Akilaani mti wa mkuyu, Petro akimkana Bwana mara tatu, Yesu Akiwaonekania wanafunzi Wake baada ya kusulubiwa na ufufuo Wake, Akifunza kuhusu kufunga, kufunza kuhusu maombi, kufunza kuhusu talaka, kuzaliwa na kizazi cha Yesu, uteuzi wa Yesu wa wanafunzi, na mengine mengi. Hata hivyo, mwanadamu anayathamini kama hazina, hata kuthibitisha kazi ya leo kulingana nayo. Hata wanaamini kuwa Yesu Alitenda kiasi tu katika muda baada ya kuzaliwa Kwake. Ni kana kwamba wanaamini kuwa Mungu anaweza kufanya hayo tu, kwamba hakuna kazi nyingine. Je huu si upumbavu?” “Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri katika Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. … Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu. Hasa, haingekuwa tendo la imani ya uwongo kutafuta ndani ya Biblia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Nini unaweza kupambanua tu kwa kushika Biblia kwa mikono yako? Uwe mkalimani wa Biblia ama mhubiri, nani anaweza kujua mbeleni kazi ya leo?” “Ikiwa unatamani kuiona kazi ya Enzi ya Sheria, na kuona jinsi gani Waisraeli waliifuata njia ya Yehova, basi ni lazima usome Agano la Kale; ikiwa unatamani kuelewa kazi ya Enzi ya Neema, basi ni lazima usome Agano Jipya. Lakini unawezaje kuona kazi ya siku za mwisho? Ni lazima ukubali uongozi wa Mungu wa leo, na kuingia katika kazi ya leo, maana hii ni kazi mpya na hakuna ambaye ameirekodi katika Biblia hapo nyuma. … Kazi ya leo ni njia ambayo mwanadamu hajawahi kuiendea, na njia ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kuiona. Ni kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla—ni kazi ya Mungu ya hivi karibuni kabisa duniani. … Ni nani ambaye angeweza kurekodi kila hatua ya kazi ya leo, bila kuondoa kitu? Ni nani angeweza kurekodi kazi hii kubwa na yenye hekima ambayo inakataa maagano ya kitabu cha kale? Kazi ya leo sio historia, na kama vile, ikiwa unatamani kutembea katika njia ya leo, basi mnapaswa kutengana na Biblia, unapaswa kwenda mbele zaidi ya vitabu vya unabii au historia ya Biblia. Baada ya hapo tu ndipo utaweza kutembea njia mpya vizuri, na baada ya hapo ndipo utaweza kuingia katika ufalme mpya na kazi mpya(Neno Laonekana katika Mwili).

Baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, Dada Zhou aliendeleza ushirika wake. Alisema, “Kila mtu anayeijua Biblia anajua kwamba Agano la Kale na Jipya ni rekodi tu ya hatua mbili za kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Ni ushuhuda wa kazi ya Mungu. Kila wakati Mungu alipomaliza hatua ya kazi, watu walioipitia waliandika kazi na maneno Yake, na kisha rekodi hizi baadaye zilijumuishwa na kuwa Biblia. Lakini kazi na maneno ya Mungu katika enzi hizo mbili havikuandikwa kikamilifu katika Biblia. Maneno ya Bwana Yesu yaliyomo katika Biblia ni machache tu. Kama Injili ya Yohana inavyosema: ‘Na pia kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya, ambayo, yote yakiandikwa, ninafikiri kwamba hata dunia yenyewe haingetosha vitabu hivyo ambavyo vitaandikwa’ (Yohana 21:25). Kulikuwa na unabii fulani wa manabii katika Enzi ya Sheria ambao haukuandikwa kikamilifu katika Maandiko. Hii inajulikana na wote. Kwa hivyo wachungaji na wazee wanaposema kwamba maneno yote ya Mungu yamo katika Biblia, na hakuna kazi au maneno Yake ambayo yamo nje ya Biblia, je, hawakanushi ukweli? Je, hawasemi uwongo na kudanganya? Mm. Mungu ndiye Bwana wa uumbaji. Yeye ni mkuu sana na mwenye mengi, kitabu kimoja, Biblia, kinawezaje kujumuisha kikamilifu kazi na maneno Yake?” Kisha akasoma kutoka katika Kitabu cha Ufunuo: “Na nikaona katika mkono wa kulia wa yeye ambaye anaketi kwa kiti cha enzi kitabu ambacho kiliandikwa ndani na nyuma, kilichofungwa kwa muhuri saba(Ufunuo 5:1). “Na mmoja wa wazee hao aliniambia, Usitoe machozi: tazama, Simba wa kabila ya Yuda, Shina lake Daudi, ameweza kukifungua hicho kitabu, na kuzitoa muhiri saba zilizoko(Ufunuo 5:5). Alishiriki, “Inasemekana hapa kwamba kuna maandishi ndani na nje ya kitabu hiki, ni kwamba tu kimetiwa mihuri saba, na Bwana wa siku za mwisho pekee ndiye Anayeweza kufungua kitabu hicho na kufungua mihuri saba. Ni kwa njia hiyo pekee ndiyo tunaweza kuona kile kilichoandikwa ndani ya kitabu hiki. Pia imetabiriwa mara nyingi katika Ufunuo: ‘Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho(Ufunuo 2-3). Utabiri huu wa Biblia unathibitisha kuwa Bwana atanena maneno mengine zaidi atakaporudi. Kwa hivyo kazi na maneno ya Bwana aliyerudi kweli yangeweza kuandikwa katika Biblia mapema? Je, maneno ya Mungu katika Biblia yanaweza kuchukua nafasi ya yale ambayo Roho Mtakatifu anayaambia makanisa katika siku za mwisho? Je, yanaweza kuchukua nafasi ya kitabu kilichofunguliwa na Mwanakondoo? Je, yanaweza kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho?” Niliposikia hayo, niliwaza, “Nimesoma mistari hii kidogo. Kwa nini maswali haya hayajawahi kunijia akilini?” Dada yule kisha aliendelea na ushirika: “Biblia ni kumbukumbu ya kazi ya Mungu ya zamani. Miaka mingi baada ya Agano la Kale kubuniwa, Bwana Yesu alikuja na kufanya kazi ya ukombozi kwa ajili ya Enzi ya Neema. Kwa hivyo je, kazi Yake na maneno Yake yalijiingiza yenyewe katika Maandiko? Kazi ya Mungu na maneno Yake yalihitaji kukusanywa na kufanywa kuwa Biblia. Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho na Ameonyesha ukweli wote ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu. Je, ukweli huu ungeweza kujiingiza wenyewe katika Biblia? Kwa hivyo kudai kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yameandikwa katika Biblia, na kwamba hakuwezi kuwa na mengine nje ya Biblia, ni maoni yasiyo sahihi na ya upuuzi, na ni matokeo tu ya fikira na mawazo ya watu.”

Kusikia ushirika wa Dada Zhou kulinipa nuru sana. Nilihisi kwamba kila kitu alichoshiriki kilikubaliana na ukweli. Biblia ni rekodi tu ya hatua mbili za kazi ya Mungu: Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Ni ushuhuda wa kazi Yake, lakini haiwezi kumwakilisha Bwana au kazi na maneno Yake katika siku za mwisho. Kazi na maneno ya Bwana Yesu hata hayakuandikwa katika Biblia kwa ukamilifu, kwa hivyo kazi na maneno ya Mungu katika siku za mwisho yangewezaje kuandikwa katika Biblia kabla ya wakati? Nilifuata maneno ya wachungaji na wazee, na hivyo kuwekea mipaka kazi na maneno ya Mungu kuwa yale yaliyomo katika Biblia, na kuamini kuwa hakuna chochote nje ya hayo kilichotoka kwa Mungu. Je, sikuwa nikiongea tu upuuzi waziwazi? Je, sikuwa nikimwekea Bwana mipaka na kumkufuru? Nilijawa na majuto nilipofikiria hayo. Kwa nini sikuwa nimesoma maneno ya Mwenyezi Mungu mapema? Kwa kweli sikupaswa kuwafuata wachungaji na wazee kwa upofu, na kuiwekea kazi ya Mungu mipaka kulingana na fikira na mawazo. Maoni haya yanadhuru sana!

Dada Zhou kisha akaibua hoja nyingine ya kujadili: Ni kwa nini kushikilia Biblia tu bila kukubali kazi na maneno ya Mungu ya siku za mwisho kunamaanisha watu hawawezi kuingia katika ufalme wa Mungu na kupata uzima wa milele? Alisema, “Biblia ni rekodi tu ya hatua mbili za kazi ya Mungu. Haiwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu ya kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu katika siku za mwisho. Katika Enzi ya Sheria, kazi kuu ya Mungu ilikuwa kutangaza sheria na amri ili kuongoza maisha ya watu hapa duniani. Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi pekee. Alisulubiwa ili kuwakomboa wanadamu kutoka katika miliki ya Shetani, kutukomboa kutoka katika dhambi zetu, na kutufanya tustahiki kumwomba Mungu ili tuweze kufurahia neema zote za Mungu. Lakini asili yetu ya dhambi na chanzo cha dhambi yetu havikutatuliwa. Hii ndiyo maana bado tunasema uwongo, tunatenda dhambi, tunamwasi na kumpinga Mungu kila mara, na hatustahili kuingia katika ufalme wa Mungu. Hii ndiyo maana Bwana Yesu alitabiri kwamba Atarudi na kuonyesha ukweli katika siku za mwisho ili kuhukumu na kumwokoa mwanadamu kikamilifu. Injili ya Yohana inasema, ‘Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). Pia inasema, ‘Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48). Mwenyezi Mungu kuja katika siku za mwisho kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu kunatimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu. Mwenyezi Mungu ameonyesha mamilioni ya maneno na maneno haya yanajumlisha kila kitu. Siri za Biblia zimefunuliwa, kuna unabii wa siku zijazo za ufalme, mengine yanajadili hatima ya wanadamu, na mengine yanachambua chanzo cha upinzani wa wanadamu kwa Mungu. Mungu pia anafunua waziwazi ukweli ambao watu wanahitaji ili kupata wokovu kamili. Hiyo ni pamoja na ukweli wa ndani wa hatua tatu za kazi za Mungu za kuwaokoa mwanadamu, siri za kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, na siri za miili ya Mungu. Mungu anafichua jinsi Shetani anavyowapotosha wanadamu, jinsi Mungu anavyofanya kazi ili kuwaokoa mwanadamu, kiini na ukweli wa wanadamu kuptoshwa na Shetani, imani, utiifu, na kumpenda Mungu kwa kweli ni nini, jinsi ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na kadhalika. Ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni njia ya uzima wa milele ambayo Tukishikilia tu Biblia bila kukubali hukumu na utakaso wa Mungu katika siku za mwisho, hatutawahi kupata ukweli, kuacha dhambi, kuokolewa kabisa, na kuingia katika ufalme wa mbinguni.”

Ushirika huo kutoka kwa kina ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu ulinisaidia nione kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inatimiza kikamilifu unabii wa Biblia. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, ni sauti ya Mungu, na ni njia ya uzima wa milele ambayo Mungu hutupa katika siku za mwisho! Nilikuwa nimedhani kwamba kazi na maneno ya Mungu yalikuwa tu yale yaliyomo katika Biblia kwa sababu nilikuwa nimewasikiliza wachungaji na wazee, na nikashikilia mawazo ya kidini. Nilikataa kukubali au kutafuta kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Sikuweza kupata riziki ya maneno ya sasa ya Mungu na nikaingia gizani. Bila huruma ya Mungu na wokovu wa kupata mapendekezo ya video za YouTube za Kanisa la Mwenyezi Mungu, zilizonipa bahati nzuri ya kuisikia sauti ya Mungu, bado ningekuwa nikiwafuata wachungaji na wazee, na singetafuta au kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Iwapo hali ingekuwa hivyo, ningesoma Biblia kwa miaka mia moja lakini singekaribisha kamwe kurudi kwa Bwana hata kidogo. Naona kuwa uwezo wangu wa kupata wokovu wa Mungu katika siku za mwisho ni kwa sababu tu ya mwongozo Wake. Huu ni wokovu wa Mungu wa ajabu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuja Nyumbani

Na Muyi, Korea ya Kusini“Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia,...

Nimekaribisha Kurudi Kwa Bwana

Na Chuanyang, Vereinigte StaatenMajira ya baridi kali ya mwaka wa 2010 huko Amerika yaliniacha nikihisi baridi sana. Kando na baridi kali...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp