Kuna tofauti ipi kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya neema na maisha ya kanisa katika Enzi ya Ufalme?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na wakati walipokuwa wakila, Yesu alichukua mkate, na akaubariki, na kuumega, na akawapa wanafunzi wake, na kusema, Chukueni, kuleni; huu ni mwili wangu. Naye akakichukua kikombe, na kushukuru, na kuwapa akisema, Ninyi nyote kunyweni kutoka katika kikombe hiki; Kwa kuwa hii ni damu yangu ya agano jipya, ambayo inamwagwa kwa ajiki ya msamaha wa dhambi” (Mathayo 26:26-28).
“Nami nikaenda kwa yule malaika, na kumwambia, Nipe kile kitabu kidogo. Naye akaniambia, Kichukue, na ukile; na kitafanya tumbo lako kuwa chungu, lakini kitakuwa kitamu mithili ya asali ndani ya kinywa chako” (Ufunuo 10:9).
Maneno Husika ya Mungu:
Wakati ambapo, katika Enzi ya Neema, Mungu alirudi kwa mbingu ya tatu, kazi ya Mungu ya kuwakomboa wanadamu wote ilikuwa kwa kweli tayari imeendelea katika tendo lake la kumaliza. Vyote vilivyobaki duniani vilikuwa msalaba ambao Yesu aliubeba, sanda ya kitani ambayo Yesu alifungiwa ndani, na taji ya miiba na joho la rangi nyekundu ambavyo Yesu alivaa (hivi vilikuwa vitu ambavyo Wayahudi walitumia kumdhihaki Yeye). Yaani, kazi ya kusulubiwa kwa Yesu ilikuwa imesababisha ghasia kwa muda na kisha ikatulia. Tangu wakati huo na kuendelea, wanafunzi wa Yesu wakaanza kuendeleza kazi Yake, wakiyachunga na kunyunyizia katika makanisa kila mahali. Maudhui ya kazi yao yalikuwa haya: kuwafanya watu wote watubu, waungame dhambi zao, na wabatizwe; mitume wote wakieneza hadithi ya ndani ya kusulubiwa kwa Yesu na kile kilifanyika kwa kweli, kila mtu asiweze kujizuia kuanguka chini mbele za Yesu kuungama dhambi zake, na zaidi ya hayo mitume wakieneza kila mahali maneno yaliyonenwa na Yesu na sheria na amri Alizozianzisha. Kuanzia wakati huo ujenzi wa makanisa ulianza katika Enzi ya Neema.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika mikutano maalum ya zamani au mikutano mikuu iliyokuwa katika sehemu mbalimbali, ni kipengele kimoja tu cha vitendo kilichozungumziwa. Vitendo kama hivyo ni vile vilivyotiwa katika vitendo katika Enzi ya Neema na hapakuwa na mfanano wowote na ufahamu wa Mungu kwani maono ya Enzi ya Neema yalikuwa tu maono ya kusulubiwa kwa Yesu, na hapakuwa na maono ya juu zaidi. Mwanadamu hakuhitajika kujua zaidi ya kazi Yake ya ukombozi wa mwanadamu kupitia kusulubiwa, na kwa hivyo katika Enzi ya Neema hapakuwa na maono mengine ya kufahamiwa na mwanadamu. Kwa njia hii, mwanadamu alikuwa na ufahamu mdogo sana wa Mungu na mbali na upendo na huruma za Yesu, kulikuwa na vitu vichache tu vya mwanadamu kuweka katika vitendo, vitu ambavyo vilikuwa tofauti na hali ya leo. Zamani, haikujalisha ni aina gani ya mkutano, mwanadamu hakuwa na uwezo wa kuzungumzia ufahamu wa vitendo wa kazi ya Mungu, aidha hapakuwa na yeyote aliyeweza kusema kwa dhahiri njia iliyokuwa sawa ya utendaji kwa mwanadamu kuiingilia. Aliongeza tu mambo kidogo katika msingi wa stahamala na uvumilivu; hapakuwa na mabadiliko yoyote katika kiini cha vitendo vyake kwani katika enzi hiyo Mungu hakufanya kazi yoyote mpya na matakwa ya pekee Aliyomwekea mwanadamu yalikuwa stahamala na uvumilivu, au kuubeba msalaba. Mbali na vitendo kama hivyo, hapakuwa na maono ya juu zaidi kuliko yale ya kusulubishwa kwa Yesu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu
Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanauliza, “Dada, umeshinda vipi siku hizi?” Anajibu, “Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kuridhisha matakwa ya moyo Wake.” Mwingine anasema, “Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kumkidhi.” Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha mambo maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inampinga Mungu. Wale ambao huzingatia uhalisi huwasilisha vyovyote vilivyomo katika nyoyo zao na kufungua mioyo yao katika mawasiliano. Hakuna shughuli hata moja ya uongo, hakuna heshima ama salamu na mazungumzo matupu. Wao daima huwa na uwazi na hawafuati sheria za duniani. Kuna wale ambao wako na upendeleo wa kujionyesha kwa nje, hata bila maana yoyote. Wakati mwingine anaimba, yeye anaanza kukatika, bila hata kugundua kuwa wali katika sufuria yake umeshaungua. Watu wa aina hii si wacha Mungu au waheshimiwa, bali ni watu wa kijinga kupindukia. Hizi zote ni maonyesho ya ukosefu wa ukweli! Wakati watu wengine wanawasiliana kuhusu masuala ya maisha katika roho, ingawa hawasemi kuhusu kuwa wadeni wa Mungu, wao hubaki na upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Kuwa kwako mdeni kwa Mungu hakuhusiani na watu wengine; wewe ni mdeni kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Kwa hiyo ina maana gani wewe daima kuzungumzia haya kwa watu wengine? Lazima uweke umuhimu kwa kuingia katika uhalisi, si kwa bidii au maonyesho ya nje.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani, Mtu Lazima Alenge Ukweli—Kujihusisha na Kaida za Dini Sio Imani
“Kushiriki na kuwasiliana kuhusu uzoefu” kunamaanisha kuzungumza kuhusu kila wazo katika moyo wako, hali yako, uzoefu wako na maarifa ya maneno ya Mungu, na pia tabia potovu ndani yako. Na baada ya hayo, wengine wanatambua mambo haya, na kukubali mazuri na kutambua kile kilicho hasi. Huku tu ndiko kushiriki, na huku tu ndiko kuwasiliana kwa kweli. Hakumaanishi tu kuwa na umaizi katika maneno ya Mungu ama sehemu ya wimbo wa kidini, na kuwasiliana upendavyo na kisha kutofanya mengine zaidi, na kutosema chochote kuhusu maisha yako halisi. Kila mtu huongea kuhusu maarifa ya mafundisho na ya nadharia, na hawasemi chochote kuhusu maarifa yaliyotoka kwa uzoefu halisi. Nyote mnaepuka kuzungumza kuhusu vitu kama hivyo, kuhusu maisha yenu binafsi, kuhusu maisha yenu katika kanisa pamoja na ndugu zenu, na kuhusu dunia yenu ya ndani. Kwa kufanya hili, kunawezaje kuwa na kuwasiliana kwa kweli kati ya watu? Kunawezaje kuwa na imani ya kweli? Hakuwezi kuwa hata kidogo! Iwapo mke hazungumzi kamwe kuhusu maneno ndani ya moyo wake kwa mume wake, wao ni wasiri? Je, wanaambiana siri? Tuseme kwamba siku nzima, “Nakupenda!” Wanasema tu haya, lakini hajawahi kuweka wazi wanayoyafikiri katika mioyo yao, kile wanachotaka kutoka kwa kila mmoja, ama ni shida zipi walizo nazo. Hawajawahi kuzungumza wao kwa wao kuhusu mambo kama hayo, wala hajawahi kuambiana siri—na iwapo hao wawili hawajawahi kuambiana siri, basi, je, wao ni wachumba wanaopendana? Iwapo hawana lolote isipokuwa maneno yenye kuvutia kwa mwingine wakiwa pamoja, kweli wao ni mke na mume? Bila shaka sio! Ikiwa ndugu wanaweza kuambiana siri, kusaidiana, na kuruzukiana wakiwa pamoja, basi kila mtu lazima azungumze kuhusu uzoefu wake binafsi wa kweli. Usipozungumza kuhusu uzoefu wako binafsi wa ukweli, na unazungumza tu maneno yenye kuvutia, na maneno ambayo ni ya mafundisho na ya juu juu, basi wewe si mtu mwaminifu, na huna uwezo wa kuwa mwaminifu.
Umetoholewa kutoka katika “Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mnapokuwa na ushuhuda wa, mnapaswa kuzungumza hasa kuhusu jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwaadibu watu, ni majaribio yapi anayoyatumia kuwasafisha wanadamu na kubadilisha tabia zao. Mnapaswa pia kuzungumza kuhusu kiwango cha upotovu ambacho kimefichuliwa katika uzoefu wenu,, kiasi ambacho mmestahimili na jinsi ambavyo hatimaye mlishindwa na Mungu; kiasi cha maarifa ya kweli ya kazi ya Mungu mlicho nacho, na jinsi mnavyopaswa kumshuhudia Mungu na kumlipiza kwa ajili ya upendo Wake. Mnapaswa kuweka umuhimu kwa aina hii ya lugha, huku mkiisema kwa njia rahisi. Msijihami kwa nadharia zinazoonekana kuu, zilizo tupu katika juhudi za kujigamba; kufanya hivyo huwafanya muonekane wenye majivuno sana na msio na maana. Zungumzeni zaidi kuhusu mambo ya kweli kutoka kwa uzoefu wa vitendo na mzungumze kutoka moyoni mwenu; hili ndilo lenye manufaa zaidi kwa wengine, na la kufaa zaidi kwa wao kuona. Mlikuwa watu waliompinga Mungu zaidi na wale ambao waliegemea kumtii Mungu kwa kiasi kidogo zaidi, lakini sasa mmeshindwa na maneno Yake—msisahau hilo kamwe. Mnapaswa kutenga tafakari na fikira nyingi kwa masuala haya kwa bidii. Baada ya kugundua hili, mtajua jinsi ya kushuhudia; vinginevyo mnaweza kufanya vitendo vya aibu na vya kipumbavu.
Umetoholewa kutoka katika “Akili ya Msingi Ambayo Mwanadamu Anapaswa Kumiliki” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?