Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kazi na Kuonekana kwa Mungu | Dondoo 63

Katika ufalme, vitu vingi visivyohesabika vya uumbaji vinaanza kufufuka na kupata nguvu ya maisha yao. Kwa sababu ya mabadiliko katika hali ya dunia, mipaka kati ya nchi moja na nyingine pia inaanza kusonga. Hapo awali, Nimetabiri: Wakati ardhi itagawanywa kutoka kwa ardhi, na ardhi kujiunga na ardhi, huu ndio utakuwa wakati ambao Nitayapasua mataifa kuwa vipande vidogo. Katika wakati huu, Nitafanya upya uumbaji wote na kuugawa tena ulimwengu mzima, hivyo kuweka ulimwengu katika mpangilio, Nikibadilisha hali yake ya awali kuwa mpya. Huu ndio mpango Wangu. Hizi ni kazi Zangu. Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikipitisha wazi amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayeyakiuka:

Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa viwango tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.

Sauti Yangu inapoimarika kwa uzito, pia Ninaichunguza hali ya ulimwengu. Kupitia kwa maneno Yangu, vitu visivyohesabika vya uumbaji vyote vinafanywa upya. Mbingu inabadilika, na dunia pia inabadilika. Wanadamu wanafichuliwa katika hali yao halisi na, polepole, kila mmoja kulingana na aina yake, wanadamu bila kujua wanajipata wakirejea katika ngome za familia zao. Kwa sababu ya hili, Nitafurahishwa sana. Niko huru kutokana na vurugu, na kazi Yangu kuu inakamilika, bila kujua, vitu visivyohesabika vya uumbaji vinabadilishwa, bila kujua. Nilipoumba ulimwengu, Niliunda kila kitu kulingana na aina yake, Nikifanya kila kitu kilicho na umbo la kuonekana vikusanyike pamoja na aina zao. Wakati mpango wa usimamizi Wangu unapokaribia tamati, Nitarejesha hali ya awali ya uumbaji, Nitarejesha kila kitu kiwe katika hali ya awali, Nikibadilisha kila kitu kwa namna kubwa, ili kila kitu kirudi ndani ya mpango Wangu. Muda umewadia! Hatua ya mwisho katika mpango Wangu iko karibu kutimika. Ah, dunia ya kitambo yenye uchafu! Kwa hakika mtaanguka chini kwa maneno Yangu! Kwa hakika mtafanywa kuwa bure kwa mujibu wa mpango Wangu! Ah, vitu visivyo hesabika vya uumbaji! Wote mtapata maisha mapya katika maneno Yangu, sasa mko na Bwana Mkuu! Ah, dunia mpya, safi isiyo na uchafu! Kwa kweli mtafufuka katika utukufu Wangu! Ah Mlima Zayuni! Usiwe kimya tena. Nimerudi kwa ushindi! Kutoka miongoni mwa uumbaji, Ninaichunguza dunia nzima. Duniani, wanadamu wameanza maisha mapya, wameshinda tumaini mpya. Ah, watu Wangu! Mtakosaje kurudi kwa maisha ndani ya mwanga Wangu? Mtakosaje kuruka kwa furaha chini ya uongozi Wangu? Ardhi zinapiga kelele kwa furaha, maji yanapiga kelele na vicheko vya furaha! Ah, Israeli iliyofufuka! Mtakosaje kuhisi fahari kwa mujibu wa maajaliwa Yangu? Ni nani amelia? Ni nani ameomboleza? Israeli ya kitambo haiko tena, na Israeli ya leo imeamka, imara na kama mnara, katika dunia, imesimama katika mioyo ya binadamu wote. Israeli ya leo kwa hakika itapata chanzo cha uwepo kupitia kwa watu Wangu! Ah, Misri yenye chuki! Hakika, bado hamsimama dhidi Yangu? Mnawezaje kuichukulia huruma Yangu kimzaha na kujaribu kuepuka kuadibu Kwangu? Mtakosaje kuwa katika kuadibu Kwangu? Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp