Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 424

07/10/2020

Katika hatua ya sasa, ni muhimu sana kujua ukweli kwanza, na kisha kuuweka katika vitendo na kujitayarisha zaidi na maana ya kweli ya ukweli. Mnapaswa kutafuta kupata hili. Badala ya kutafuta tu kuwafanya wengine wafuate maneno yako, unapaswa kuwasababisha wafuate vitendo vyako. Ni kwa njia hii pekee ndiyo unaweza kupata kitu cha maana. Bila kujali kitakachokukumba, bila kujali utakutana na nani, alimradi una ukweli, utaweza kusimama imara. Neno la Mungu ndicho kitu kimleteacho mwanadamu uzima, si kifo. Ikiwa baada ya kusoma neno la Mungu huchangamki, bali bado wewe ni mfu, basi una kasoro. Ikiwa baada ya muda fulani umesoma maneno mengi ya Mungu, na umesikiza mahubiri mengi ya vitendo, lakini bado uko katika hali ya kifo, basi hili ni thibitisho kwamba wewe si mtu anayethamini ukweli, wala wewe si mtu anayefuatilia ukweli. Ikiwa kweli mngetafuta kumpata Mungu, hamngelenga kujitayarisha na mafundisho na kutumia mafundisho ya juu sana kuwafunza wengine, lakini badala yake mngelenga kupitia neno la Mungu na kuweka ukweli katika vitendo. Je, hampaswi kutafuta kuingia katika hili sasa?

Mungu ana muda mdogo wa kufanya kazi Yake ndani ya mwanadamu, kwa hivyo kunaweza kuwa na matokeo yapi ikiwa hushirikiani na Yeye? Mbona Mungu daima anawataka mtende neno Lake punde mnapolielewa? Ni kwa sababu Mungu amewafichulia maneno Yake, na hatua yenu ifuatayo ni kuyatenda kwa kweli. Mnapotenda maneno haya, Mungu atatekeleza kazi ya nuru na mwongozo. Hivi ndivyo inavyopaswa kufanywa. Neno la Mungu linamwezesha mwanadamu asitawi maishani na asiwe na dalili zozote zinazoweza kumsababisha mwanadamu apotoke ama asionyeshe hisia. Unasema umesoma neno la Mungu na umelitenda, lakini bado hujapokea kazi yoyote kutoka kwa Roho Mtakatifu. Maneno yako yanaweza tu kumpumbaza mtoto. Huenda watu wengine wasijue ikiwa dhamira zako ni njema, lakini, je, unafikiri kwamba inawezekana Mungu asijue? Ni kwa nini wengine wanatenda neno la Mungu na kupokea nuru ya Roho Mtakatifu, lakini unatenda neno Lake na hupokei nuru ya Roho Mtakatifu? Je, Mungu ana mhemuko? Ikiwa dhamira zako kweli ni njema na wewe ni wa kushirikiana, basi Roho wa Mungu atakuwa nawe. Watu wengine daima hutaka kuonyesha utawala wao wenyewe, lakini kwa nini Mungu hawaruhusu wainuke na kuliongoza kanisa? Watu wengine wanatimiza kazi zao na kutenda wajibu wao tu, lakini kufumba na kufumbua, wamepata idhini ya Mungu. Hilo linawezekanaje? Mungu huchunguza moyo wa ndani sana wa mwanadamu, na watu wanaofuatilia ukweli lazima wafanye hivyo kwa dhamira njema. Watu wasio na dhamira njema hawawezi kusimama imara. Kimsingi kabisa, lengo lenu ni kuacha neno la Mungu lifanye kazi ndani yenu. Yaani, ni kuwa na ufahamu wa kweli wa neno la Mungu mnapolitenda. Pengine uwezo wenu wa kufahamu neno la Mungu ni duni, lakini unapotenda neno la Mungu, Anaweza kurekebisha dosari hii, kwa hivyo hampaswi tu kujua ukweli mwingi, lakini pia lazima muutende. Hili ni lengo kubwa zaidi ambalo haliwezi kupuuzwa. Yesu alivumilia fedheha nyingi na mateso mengi katika maisha Yake ya miaka thelathini na tatu na nusu. Aliteseka sana kwa sababu tu Alitenda ukweli, alifanya mapenzi ya Mungu katika vitu vyote, na alijali tu mapenzi ya Mungu. Haya yalikuwa mateso ambayo Hangepitia iwapo Angejua ukweli bila kuutenda. Ikiwa Yesu angefuata mafundisho ya Wayahudi na awafuate Mafarisayo, basi Hangeteseka. Unaweza kujifunza kutoka kwa matendo ya Yesu kwamba ufanisi wa kazi ya Mungu kwa mwanadamu hutokana na ushirikiano wa mwanadamu, na hili ni jambo ambalo lazima mtambue. Je, Yesu angeteseka jinsi Alivyoteseka msalabani ikiwa Hangetenda ukweli? Je, Angesali sala ya huzuni sana kama Hangetenda kulingana na mapenzi ya Mungu? Kwa hiyo, mnapaswa kuteseka kwa ajili ya kutenda ukweli; mtu anapaswa kupitia mateso ya aina hii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp