Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 3

Watu wengi huyashika maneno ya Mungu kuyasoma siku baada ya siku, kiasi kwamba wanaviweka akilini vifungu vyote maarufu humo kama vitu vyao vyenye thamani zaidi, na zaidi kuyahubiri maneno ya Mungu kila mahali, wakiwatolea na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno Yake. Wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, kuwa na ushuhuda kwa maneno Yake, kwamba kufanya hivi ni kufuata njia ya Mungu; wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kwamba kufanya hivi ni kuleta maneno Yake katika maisha yao halisi, kuwa kufanya hivi kutawawezesha kupokea pongezi ya Mungu, na kuokolewa na kukamilika. Lakini, hata wanapohubiri maneno ya Mungu, hawazingatii maneno ya Mungu katika matendo, ama kujaribu kujileta sambamba na yale yanayofichuliwa katika maneno ya Mungu. Badala yake, wanayatumia maneno ya Mungu kupata upendo na imani ya wengine kwa hila, kuingia katika usimamizi wao wenyewe, na kubadhiri na kuiba sifa za Mungu. Wanatarajia, kwa ubatili, kutumia nafasi waliyopata kwa kueneza maneno ya Mungu ili kupewa kazi ya Mungu na pongezi Yake. Miaka mingapi imepita, lakini hao watu hawajaweza tu kupata pongezi ya Mungu katika hatua ya kuyahubiri maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kugundua njia ambayo wanafaa kufuata katika hatua ya kushuhudia maneno ya Mungu, na hawajajisaidia tu ama kujipatia wenyewe katika hatua ya kuwapa na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kumjua Mungu, ama kuamsha ndani yao uchaji wa kweli wa Mungu, katika hatua ya kufanya haya yote; kwa upande mwingine, kutoelewa kwao kuhusu Mungu kunakuwa hata wenye kina zaidi, kutokuwa na imani kwao kwa Mungu kunazidi kuwa na mashaka, na mawazo yao kumhusu yanatiwa chumvi zaidi. Wakijazwa na kuongozwa na mawazo yao kuhusu maneno ya Mungu, wanaonekana kuwa katika haki yao kamili, kana kwamba wanapitia ujuzi wao bila juhudi, kana kwamba wamepata kusudi lao katika maisha, wito wao, na kana kwamba wameshinda maisha mapya na kuokolewa, kana kwamba, maneno ya Mungu yakibiringika kutoka kwenye ulimi kwa kukariri, wameupata ukweli, kushika nia za Mungu, na kugundua njia ya kumjua Mungu, kana kwamba, katika wakati wa kuhubiri maneno ya Mungu, wanakuja kila wakati uso kwa uso na Mungu, pia, wana “sukumwa” kila wakati mpaka kiwango cha kilio, na kila wakati kuongozwa na “Mungu” katika maneno ya Mungu, wanaonekana kushika bila kukoma wasiwasi Wake wenye ari na nia njema, na wakati uo huo kushika wokovu wa Mungu kwa mwanadamu na usimamizi Wake, kuja kujua kiini Chake, na kuelewa tabia Yake ya haki. Msingi huu ukizingatiwa, wanaoneka kuamini hata zaidi katika uwepo wa Mungu, kujua zaidi hali ya utukufu Wake, na kuhisi hata kwa kina zaidi ukuu Wake na kuvuka mipaka Kwake. Wakiwa wameinuka katika ufahamu wao wa kijuujuu wa maneno ya Mungu, itaonekana kuwa imani yao imekua, kuamua kwao kupitia mateso kumetiwa nguvu, na maarifa yao kwa Mungu yamekuwa na kina. Ila hawajui kwamba, hadi watakapopitia maneno ya Mungu kwa kweli, maarifa yao yote kuhusu Mungu na mawazo yao kumhusu Yeye yanatoka kwa mawazo yao wenyewe ya kufikiri kwa ubunifu na kukisia. Imani yao haiwezi kusimama jaribio lolote kutoka kwa Mungu, wanachoita kiroho na kimo haviwezi kusimama chini ya majaribu ya Mungu na ukaguzi, uamuzi wao ni ngome tu iliyojengwa juu ya changarawe, na wanachoita maarifa juu ya Mungu pia sio zaidi ya ubunifu wa mawazo yao. Kwa hakika, watu hawa, ambao, ilivyokuwa, wameweka juhudi kubwa katika maneno ya Mungu, hawajawahi kutambua imani ya kweli ni nini, kujiwasilisha kwa kweli ni nini, kujali kwa kweli ni nini, ama maarifa ya kweli ya Mungu ni nini. Wanachukua nadharia, mawazo, maarifa, zawadi, utamaduni, ushirikina na hata tabia nzuri za binadamu, na kuyafanya kuwa “uwekezaji wa msingi” na “zana za kijeshi” za kumwamini Mungu na kumfuata, hata kuyafanya kuwa misingi ya imani yao kwa Mungu na katika kumfuata Yeye. Wakati uo huo, pia wanachukua uwekezaji msingi huu na silaha na kuyafanya kuwa hirizi ya uchawi kwa kumjua Mungu, ya kukutana na kubishana na ukaguzi wa Mungu, majaribu, kuadibu, na hukumu. Mwishowe, wanachopata bado hakijumlishi chochote zaidi ya hitimisho kumhusu Mungu zinazoegemea hisia za kidini, katika kabaila za ushirikina, na kwa yote yaliyo ya kimapenzi, ya kustaajabisha, na yenye ugumu kuelewa, na njia yao ya kujua na kumweleza Mungu imepigwa muhuri katika muundo sawa na wa wale watu wanaomini katika Mbingu iliyo Juu pekee, ama Mtu Mzee aliye Mawinguni, wakati ukweli wa Mungu, kiini Chake, tabia Zake, miliki Zake na asili, na kadhalika, yote yanayomhusu Mungu wa kweli Mwenyewe, ni vitu ambavyo kuvijua kumekosa mshiko, havina uhusiano kabisa na viko mbali kabis. Katika njia hii, ingawa wanaishi chini ya upaji na ustawishaji wa maneno ya Mungu, hawawezi hata hivyo kutembea kwa kweli katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Sababu ya hakika ya hii ni kwamba hawajawahi kupata kujuana na Mungu, wala hawajawahi kuwa na mawasiliano ya kweli ama ushirika Naye, kwa hivyo haiwezekani kufikia maelewano ya pamoja na Mungu, ama kuamsha ndani mwao imani halisi katika, kufuata, ama ibada ya Mungu. Kwamba wanafaa kuyahusisha maneno ya Mungu, kwamba wanafaa kumhusisha Mungu—mwelekeo huu na tabia imewahukumu kurudi mkono mtupu kutoka kwa jitihada zao, imewahukumu katika maisha yote wasiweze kutembea katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Lengo wanalolengea, na mwelekeo wanaoelekea, inamaanisha kuwa ni maadui wa Mungu milele, na kwamba hata milele hawatawahi kuweza kupokea wokovu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp