Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 213

03/08/2020

Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kuwatakasa binadamu ili binadamu aweze kuwa na ukweli, kwa sababu binadamu kwa sasa anao ukweli mdogo sana! Kufanya kazi ya kushinda kwa watu hawa ni jambo la umuhimu mkubwa mno. Nyote mmeanguka katika ushawishi wa giza na mmeumizwa mno. Shabaha ya kazi hii, basi, ni kuwawezesha kujua maumbile ya binadamu na hivyo basi kuishi kwa ukweli. Kufanywa kuwa mtimilifu ni kitu ambacho viumbe vyote vinafaa kukubali. Kama kazi ya awamu hii inahusu tu kufanya watu kuwa watimilifu, basi inaweza kufanywa Uingereza, au Amerika, au Israeli; inaweza kufanywa kwa watu wa taifa lolote. Lakini kazi ya kushinda ni yaupambanuzi. Hatua ya kwanza ya kazi ya kushinda ni ya mudamfupi; aidha, itatumika kudhalilisha Shetani na kuushinda ulimwengu mzima. Hii ndiyo kazi ya mwanzo ya kushinda. Mtu anaweza kusema kwamba kiumbe chochote kinachomwamini Mungu kinaweza kufanywa kuwa kiimilifu kwa sababu kufanywa kuwa mtimilifu ni kitu ambacho mtu anaweza kufikia tu baada ya mabadiliko ya muda mrefu. Lakini kushindwa ni tofauti. Mfano wa kushinda ndio ambao lazima ni yule anayebaki nyuma kabisa, akiishi kwenye giza lile totoro kabisa, na vilevile ndiye aliyedhalilishwa, na asiyekuwa radhi kumkubali Mungu, na asiyetii Mungu kabisa. Huyu ndiye aina ya mtu anayeweza kutoa ushuhuda wa kushindwa. Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kumshinda Shetani. Shabaha kuu ya kufanya watu kuwa watimilifu, kwa upande mwingine, ni kuwapata watu wale. Ni kuwawezesha watu kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa kwamba kazi ya kushinda imefanywa hapa, kwa watu kama ninyi. Lengo ni kuwafanya watu kutoa ushuhuda baada ya kushindwa. Watu hawa walioshindwa watatumika kufikia shabaha ya kudhalilisha Shetani. Kwa hivyo, mbinu kuu ya ushindi ni gani? Kuadibu, hukumu, kutupilia mbali laana, na kufichua—kwa kutumia tabia ya wenye haki katika kuwashinda watu ili waweze kushawishika kabisa, kujawa na imanikatika mioyo yao na vinywa vyao kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu. Ili kutumia uhalisi wa neno na kutumia mamlaka ya neno ili kuwashinda watu na kuwashawishi kabisa—hivi ndivyo ilivyo kushindwa. Wale waliofanywa kuwa watimilifu hawawezi tu kuwa watiifu baada ya kushindwa, lakini wanaweza pia kuwa na maarifa na kubadilisha tabia yao. Wanamjua Mungu, wamepitia njia ya Mungu mwenye upendo, na wamejazwa na ukweli. Wanajua namna ya kupitia kazi ya Mungu, wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na wanayo mapenzi yao wenyewe. Wale waliofanywa kuwa watimilifu ni wale walio na uelewa halisi wa ukweli kutokana na kuwa na ukweli ulio na uzoefu. Wale walioshindwa ni wale walio na ukweli lakini hawajakubali maana halisi ya ukweli. Baada ya kushindwa, wanatii, lakini utiifu wao unatokana na hukumu waliopokea. Hawana uelewa kabisa wa hali halisi ya ukweli mwingi. Wanautambua ukweli kwa matamshi, lakini bado hawajaanza kuonyesha ukweli; wanauelewa ukweli, lakini hawajapitia ule ukweli. Kazi inayofanywa kwa wale wanaofanywa kuwa watimilifu inajumuisha kuadibiwa na kuhukumiwa, pamoja na toleo la maisha. Mtu anayethamini kuonyesha ukweli ni mtu wa kufanywa kuwa mtimilifu. Tofauti kati ya wale watakaofanywa kuwa watimilifu na wale walioshindwa inapatikana katika hoja kama wataendeleza ukweli huu. Wale wanaouelewa ukweli, wameanza kuonyesha ukweli, na wanauishi ukweli huo ndio wale waliofanywa kuwa watimilifu; wale wasioelewa ukweli, hawauingii ukweli, yani, wale wasioishi ukweli, ni watu wasioweza kufanywa watimilifu. Watu kama hao wanaweza sasa kutii kabisa, basi wameshindwa. Kama wale walioshindwa hawatatafuta ukweli—kama watafuata tu lakini wasiishi kwa ukweli, kama wataushuhudia na kuusikia ukweli lakini wakakosa kuthamini kuishi kwa ukweli—hawawezi kufanywa kuwa watimilifu. Wale wa kufanywa kuwa watimilifu wanaendeleza ukweli kulingana na njia ya kuwa watimilifu, yani wanaendeleza ukweli kutokana na njia ya kuwa watimilifu. Kupitia haya, wanatimiza mapenzi ya Mungu, na wanapata kufanywa kuwa watimilifu. Yeyote anayefuata hadi mwisho kabla ya kazi hiyo ya ushindi kuhitimishwa ni mshinde, lakini hawezi kusemekana kuwa ndiye aliyefanywa kuwa mtimilifu. Kufanywa kuwa watimilifu kunarejelea wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanaweza kufuatilia ukweli na kufaidika kutoka kwa Mungu. Kunaashiria wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanasimama imara katika majaribio na wanaishi kwa kudhihirisha ukweli. Kile kinachotofautisha kushindwa na kufanywa kuwa mtimilifu ni zile tofauti kwenye hatua za kufanya kazi na tofauti katika kiwango ambacho ukweli unashikiliwa. Wale wote ambao hawajaanza kushughulikia njia ya kuwa watimilifu, kumaanisha wale wasio na ukweli, kwa hakika wataishia kuondolewa kabisa. Ni wale tu walio na ukweli na wanaoishi ukweli wanaoweza kumilikiwa kabisa na Mungu. Yani, wale wanaoishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro ndio wanaofanywa kuwa watimilifu, huku wengine wote ndio wameshindwa. Kazi inayofanywa kwa wale wote wanaoshindwa inajumuisha tu uwekwaji laana, adibu, na kuonyesha hasira, na kile kinachowapata vyote vinahusu tu uadilifu na laana. Kushughulikia mtu kama huyo ni kufichua waziwazi—kufichua tabia potoshi iliyo ndani yake ili aweze kujitambua na kushawishika kabisa. Punde binadamu anapokuwa mtiifu kabisa, kazi ya ushindi inakamilika. Hata kama wingi wa watu wangali wanatafuta ukweli, kazi ya ushindi itakuwa imekamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp