Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 65

Mat 12:1 Wakati huo katika siku ya Sabato Yesu alipitia mashamba ya nafaka; na wanafunzi wake walihisi njaa, nao wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.

Mat 12:6-8 Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.

Hebu kwanza tuangalie dondoo hii: “Wakati huo katika siku ya Sabato Yesu alipitia mashamba ya nafaka; na wanafunzi wake walihisi njaa, nao wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.”

Kwa nini tumeichagua dondoo hii? Dondoo hii ina uhusiano upi na tabia ya Mungu? Katika maandiko haya kitu cha kwanza tunachojua ni kwamba ilikuwa ni siku ya Sabato, lakini Bwana Yesu alipita kule nje na kuwaongoza wanafunzi Wake katika mashamba ya nafaka. Lakini zaidi “cha kufedhehesha” ni kwamba waliweza hata “wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.” Katika Enzi ya Sheria, sheria za Yehova Mungu zilikuwa kwamba watu wasingeweza kuenda vivi hivi tu au kushiriki katika shughuli katika siku ya Sabato—kulikuwa na mambo mengi ambayo hayangefanywa siku ya Sabato. Hatua hii ya Bwana Yesu ilikuwa ya kuchanganya hasa kwa wale waliokuwa wameishi chini ya sheria kwa muda mrefu, na iliweza hata kuchochea upinzani mkubwa. Kuhusiana na mchanganyiko wao na namna walivyouzungumzia kile ambacho Bwana Yesu alifanya, tutaweka hilo pembeni kwa sasa na kuzungumzia kwanza kwa nini Bwana Yesu alichagua kufanya hivi katika siku ya Sabato, kwa siku zote, na kile Alichotaka kuwasilisha kwa watu waliokuwa wakiishi katika enzi ya kale kupitia katika hatua hii. Huu ndio uhusiano kati ya dondoo hii na tabia ya Mungu ambayo Ningependa kuzungumzia.

Bwana Yesu alipokuja, Alitumia vitendo Vyake utendanji kuweza kuwasiliana na watu: Mungu alikuwa ameiondoa Enzi ya Sheria na alikuwa ameanza kazi mpya, na kazi hii mpya haikuhitaji uadhimisho wa Sabato; wakati Mungu alipotoka katika mipaka ya siku ya Sabato, hicho kilikuwa tu kionjo cha mapema cha kazi Yake mpya, na kwa kweli kazi Yake kubwa ilikuwa ikiendelea kujitokeza. Bwana Yesu aliopanza kazi Yake, tayari Alikuwa ameacha nyuma zile pingu za Enzi ya Sheria, na alikuwa ametupilia mbali zile taratibu na kanuni zilizokuwa za enzi hiyo. Ndani yake hakuwa na dalili za chochote kuhusiana na sheria; Alikuwa ameitupa nje mzima mzima na hakuifuata tena, na Hakuhitaji tena mwanadamu kuifuata. Kwa hivyo hapa unaona kwamba Bwana Yesu alipita katika mashamba siku ya Sabato; Bwana hakupumzika lakini, alikuwa akipita kule nje akifanya kazi. Hatua hii Yake ilikuwa ya kushtua kwa dhana za watu na iliweza kuwawasilishia ujumbe kwamba Hakuishi tena chini ya sheria na kwamba Alikuwa ameacha ile mipaka ya Sabato na kujitokeza mbele ya mwanadamu na katikati yao katika taswira mpya, huku akiwa na njia mpya ya kufanya kazi. Hatua hii Yake iliwaambia watu kwamba Alikuwa ameleta pamoja naye kazi mpya iliyoanza kwa kwenda nje ya sheria na kwenda nje ya Sabato. Wakati Mungu alitekeleza kazi Yake mpya, Hakushikilia tena ya kale, na Hakujali tena kuhusu taratibu za Enzi ya Sheria. Wala Hakuathirika na kazi Yake mwenyewe katika enzi ya awali, lakini Alifanya kazi kwa kawaida katika siku ya Sabato na wakati wanafunzi Wake waliona njaa, waliweza kuvunja masuke na wakala. Haya yote yalikuwa kawaida sana machoni mwa Mungu. Mungu angeweza kuwa na mwanzo mpya kwa nyingi za kazi Anazotaka kufanya na mambo Anayotaka kusema. Punde Anapokuwa na mwanzo mpya, Hataji kazi Yake ya awali tena wala kuiendeleza. Kwani Mungu anazo kanuni Zake katika kazi Yake. Anapotaka kuanzisha kazi mpya, ndipo Anapotaka kumleta mwanadamu katika awamu mpya ya kazi Yake, na wakati kazi Yake imeingia katika awamu ya juu zaidi. Kama watu wanaendelea kutenda kulingana na misemo au taratibu za kale au kuendelea kushikilia kabisa kwazo, Hatakumbuka au kulisifu jambo hili. Hii ni kwa sababu tayari Ameileta kazi mpya, na ameingia katika awamu mpya ya kazi Yake. Anapoanzisha kazi mpya, Anaonekana kwa mwanadamu akiwa na taswira mpya kabisa, kutoka katika mtazamo mpya kabisa, na kwa njia mpya kabisa ili watu waweze kuona dhana zile tofauti za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hii ni mojawapo ya malengo Yake katika kazi Yake mpya. Mungu hashikilii ya kale au kutumia njia isiyotumika na wengi; Anapofanya kazi na kuongea sio njia ya kutilia mipaka kama vile watu wanavyofikiria. Ndani ya Mungu, vyote ni huru na vimekombolewa, na hakuna hali ya kukinga, hakuna vizuizi—kile Anachomletea mwanadamu vyote ni uhuru na ukombozi. Yeye ni Mungu aliye hai, Mungu ambaye kwa kweli, na kwa hakika yupo. Yeye si kikaragosi au sanamu ya udongo, na Yeye ni tofauti kabisa na sanamu ambazo watu huhifadhi na kuabudu. Yeye yuko hai na mwenye nguvu na kile ambacho maneno Yake na kazi Yake humletea binadamu vyote ni uzima na nuru, uhuru na ukombozi wote, kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi yoyote Yake. Bila kujali watu wanavyosema na namna wanavyoona au kukadiria kazi Yake mpya, Ataitekeleza kazi Yake bila kusita. Hatakuwa na wasiwasi kuhusu dhana zozote za yeyote au kazi na maneno Yake kuelekezewa vidole, au hata upinzani wao mkubwa katika kazi Yake mpya. Hakuna yeyote miongoni mwa viumbe vyote anayeweza kutumia akili ya binadamu, au kufikiria kwa binadamu, maarifa au maadili ya binadamu kupima au kufasili kile ambacho Mungu anafanya, kutia fedheha, au kutatiza au kukwamiza kazi Yake. Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya, na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, kitu chochote, au kifaa chochote, na haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili. Katika kazi Yake mpya, Yeye ni Mfalme anayeshinda daima, na nguvu zozote za kikatili na uvumi wote na hoja za uwongo zote kutoka kwa mwanadamu zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu. Haijalishi ni hatua gani mpya ya kazi Yake ambayo Anatekeleza, lazima iendelezwe na ipanuliwe katika mwanadamu, na lazima itekelezwe bila kuzuiliwa kote ulimwenguni mpaka pale ambapo kazi Yake kubwa imekamilika. Huu ndio uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu Zake. Hivyo basi, Bwana Yesu angeweza kwenda kule nje waziwazi na kufanya kazi katika siku ya Sabato kwa sababu ndani ya moyo Wake hakukuwa na sheria zozote, na hakukuwa na maarifa au kanuni zozote zilizotokana na binadamu. Kile Alichokuwa nacho kilikuwa ni kazi mpya ya Mungu na njia Yake, na kazi Yake ndio iliyokuwa njia ya kumweka huru mwanadamu, kumwachilia, kumruhusu kuwepo katika nuru na kumruhusu kuishi. Na wale wanaoabudu sanamu au miungu ya uwongo wanaishi kila siku wakiwa wamefungwa na Shetani, wakiwa wamezuiliwa na aina zote za sheria na mila—leo kitu kimoja hakiruhusiwi, kesho kingine—hakuna uhuru katika maisha yao. Wao ni sawa na wafungwa katika pingu wasio na shangwe ya kuzungumzia. “Kuzuiliwa” linawakilisha nini? Linawakilisha shurutisho, utumwa na uovu. Punde tu mtu anapoabudu sanamu, anaabudu mungu wa uwongo, akimwabudu roho wa uovu. Kuzuiliwa kunaenda sambamba na hilo. Huwezi kula hiki au kile, leo huwezi kwenda nje, kesho huwezi kuwasha jiko lako, siku inayofuata huwezi kuhamia katika nyumba mpya, siku fulani lazima zichaguliwe kwa minajili ya harusi na mazishi, na hata za wakati wa kujifungua mtoto. Haya yote yanaitwa nini? Haya yanaitwa kuzuiliwa; ni utumwa wa mwanadamu, na ndizo pingu za maisha za Shetani na roho wa maovu wanaowadhibiti, na wanaozuilia mioyo yao na mili yao. Je, kuzuiliwa huku kunapatikana kwa Mungu? Tunapozungumzia utakatifu wa Mungu, unafaa kwanza kufikira haya: Kwa Mungu hakuna vizuizi. Mungu anazo kanuni katika maneno na kazi Yake, lakini hakuna kuzuiliwa, kwa sababu Mungu Mwenyewe ndiye ukweli, njia na uzima.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp