Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 582

10/09/2020

Kwa kuwa maneno Yangu yametimilika, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu. Naenda Nikipitia dunia nzima, Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida. Leo hii, nyote mko hai mbele Yangu: kesho nyote mtakua hai ndani ya ufalme Wangu. Je, si hii ndiyo baraka kubwa zaidi ambayo Nimempa mwanadamu? Kwa sababu ya gharama ambayo mnalipa leo, mtarithi baraka za wakati ujao na mtaishi ndani ya utukufu Wangu. Je, si bado mnataka kujihusisha na kiini cha Roho Wangu? Je, bado mnataka kujiua wenyewe? Watu wako tayari kufuata ahadi ambazo wanaweza kuziona, hata kama ni za muda mfupi, lakini hakuna aliye tayari kukubali ahadi za kesho, hata kama ni za milele. Vitu vinavyoonekana kwa mwanadamu ni vitu ambavyo Nitaangamiza, na vitu visivyoweza kushikika na mwanadamu ndivyo Nitakavyotimiza. Hii ndiyo tofauti ya Mungu na mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp