Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 108

Ingawa Kristo duniani Anaweza kufanya kazi kwa niaba ya Mungu Mwenyewe, hajakuja na nia ya kuonyesha watu wote mfano Wake katika mwili. Yeye hajakuja kwa watu wote kumwona; Anakuja kwa ajili ya kuwaruhusu binadamu kuongozwa na mkono Wake, na hivyo kuingia katika enzi mpya. Kazi ya mwili wa Kristo ni kwa ajili ya kazi ya Mungu Mwenyewe, yaani, kwa ajili ya kazi ya Mungu katika mwili, na si ili kuwawezesha binadamu kuelewa kikamilifu kiini cha mwili Wake. Haijalishi jinsi Anaovyofanya kazi, haiwezi kuzidi yanayoweza kupatwa na mwili. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, anafanya hivyo katika mwili na ubinadamu wa kawaida, na wala hafichui kwa kikamilifu kwa mwanadamu uso wa kweli wa Mungu. Zaidi ya hayo, kazi Yake katika mwili kamwe sio isiyo ya kawaida au isiyokadirika kama mwanadamu anavyodhani. Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo. Mungu hupata mwili tu kukamilisha kazi ya mwili, na sio tu kuwaruhusu watu wote kumwona. Badala yake, Yeye huacha kazi Yake ithibitishe utambulisho Wake, na kuruhusu Anachofichua kushuhudia dutu Yake. Dutu Yake haikosi msingi; utambulisho Wake haukukamatwa na mkono Wake; huamuliwa kwa kazi Yake na dutu Yake. Ingawa Anacho kiini cha Mungu Mwenyewe na uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, Yeye bado, hata hivyo, mwili ambao sio kama Roho. Yeye si Mungu na sifa za Roho; Yeye ni Mungu na ganda la mwili. Kwa hivyo, haijalishi jinsi ya ukawaida Wake na Alivyo mdhaifu, na vyovyote vile Anavyotafuta mapenzi ya Mungu Baba, uungu Wake ni usioweza kupingwa. Katika mwili wa Mungu haupo tu ubinadamu wa kawaida na udhaifu Wake; kunao hata zaidi uzuri na mambo yasiyoeleweka ya uungu Wake, na vile vile matendo Yake yote katika mwili. Kwa hiyo, ubinadamu na uungu kwa kweli vipo kwa matendo ndani ya Kristo. Hili sio jambo tupu au lisilo la kawaida kwa vyovyote vile. Yeye huja duniani na lengo kuu la kufanya kazi; ni muhimu kumiliki ubinadamu wa kawaida kutekeleza kazi duniani; la sivyo, haijalishi ukubwa wa nguvu ya uungu Wake, kazi Yake ya awali haiwezi kutiwa katika utumizi mzuri. Ingawa ubinadamu Wake ni wa umuhimu mkubwa, sio dutu Yake. Dutu Yake ni uungu; Kwa hiyo, wakati Anapoanza kufanya huduma Yake hapa duniani ndio wakati Yeye huanza kuonyesha nafsi ya uungu Wake. Ubinadamu Wake uko kwa ajili tu ya kuendeleza maisha ya kawaida ya mwili Wake ili uungu Wake uweze kufanya kazi kama kawaida katika mwili; ni uungu ndio unaoongoza kazi Yake kwa ukamilifu. Wakati Anapomaliza kazi Yake, Atakuwa Ametimiza mujibu wa huduma Yake. Wanachopaswa kujua wanadamuni ni ukamilifu wa kazi Yake, na ni kwa njia ya kazi Yake kuwa Yeye Humwezesha binadamu kumjua Yeye. Katika kipindi cha kazi Yake, Yeye huonyeshakikamilifu kabisa nafsi ya uungu Wake, ambayo si tabia iliyochafuliwa na ubinadamu, au nafsi iliyochafuliwa na mawazo na tabia za binadamu. Wakati utakapokuja ambapo huduma Yake yote imefika mwisho, Atakuwa tayari kwa kikamilifu na kikamilifu Amekwishaonyesha tabia hiyo Anayopaswa kueleza. Kazi Yake haifundishwi na mwanadamu yeyote; maonyesho ya tabia Yake pia ni huru kabisa, haudhibitiwi na akili au kutengenezwa na mawazo, bali hujitokeza kiasili. Hili haliwezi kutimizwa na binadamu yeyote. Hata kama mazingira ni magumu au hali haziruhusu, Yeye Anao uwezo wa kuonyesha tabia Yake kwa wakati muafaka. Yule Ambaye ni Kristo Anaonyesha nafsi ya Kristo, ilhali wale ambao sio hawana tabia za Kristo. Kwa hivyo, hata kama wote watampinga Yeye au kuwa na fikira Kwake, hakuna anayeweza kukana kwa misingi ya fikira ya mwanadamu kwamba tabia iliyoonyeshwa na Kristo ni ile ya Mungu. Wale wote ambao humfuata Kristo kwa moyo wa kweli au kumtafuta Mungu kwa nia watakubali kwamba Yeye ni Kristo kulingana na maonyesho ya uungu Wake. Wao kamwe hawangewahi kumkataa Kristo kwa misingi ya kipengele chochote Chake ambacho hakipatani na fikira za mwanadamu. Ingawa binadamu ni wapumbavu sana, wote wanajua hasa ni nini mapenzi ya binadamu na kile kitokacho kwa Mungu. Ni kwamba tu watu wengi kwa makusudi humpinga Kristo kutokana na makusudi yao wenyewe. Kama si kwa ajili ya haya, hakuna hata mwanadamu mmoja angekuwa na sababu ya kukataa kuwepo kwa Kristo, kwa kuwa uungu uliodhihirishwa na Kristo kwa hakika upo, na kazi Yake inaweza kushuhudiwa kwa macho ya wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp