Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 159

Wakati wowote Shetani anampotosha mwanadamu ama anashughulika na madhara yasiyodhibitiwa, Mungu hasimami bila kazi, wala haweki kando ama kupuuza wale ambao amechagua. Yote ambayo Shetani anafanya ni wazi kabisa na yanaeleweka na Mungu. Haijalishi anachofanya Shetani, haijalishi mwenendo anaosababisha kuibuka, Mungu anajua yote ambayo Shetani anajaribu kufanya, na Mungu hawawachi wale ambao amechagua. Badala yake, bila kuvuta macho hata kidogo, kwa siri, kwa ukimya, Mungu anafanya yote yanayohitajika. Mungu Anapoanza kufanya kazi kwa mtu, wakati amemchagua mtu, Haambii yeyote, wala Hamwambii Shetani, wala hata kufanya maonyesho makubwa. Anafanya tu kwa ukimya, kwa asili kile ambacho kinahitajika. Kwanza, Anakuchagulia familia; usuli ambao hiyo familia inao, wazazi wako ni nani, mababu zako ni nani—haya yote tayari yaliamuliwa na Mungu. Kwa maneno mengine, haya hayakuwa uamuzi wa mvuto wa ghafla yaliyofanywa na Yeye, lakini badala yake hii ilikuwa kazi iliyoanza kitambo. Baada ya Mungu kukuchagulia familia, pia Anachagua tarehe ambayo utazaliwa. Kwa sasa, Mungu anaangalia unapozaliwa katika dunia hii ukilia, Anatazama kuzaliwa kwako, Anatazama unapotamka maneno yako ya kwanza, Anatazama unapoanguka na kutembea hatua zako za kwanza, ukijifunza kutembea. Kwanza unachukua hatua moja na kisha unachukua nyingine … sasa unaweza kukimbia, sasa unaweza kuruka, sasa unaweza kuongea, sasa unaweza kuonyesha hisia zako. Mwanadamu anavyokuwa, macho ya Shetani yamewekwa kwa kila mmoja wao, kama chui mkubwa mwenye milia anavyomwangalia nyara wake. Lakini kwa kufanya kazi Yake, Mungu hajawahi kuteseka mapungufu yoyote ya watu, matukio ama mambo, ya nafasi ama wakati; Anafanya kile anachopaswa kufanya na Anafanya kile Anacholazimika kufanya. Katika mchakato wa kukua, unaweza kukutana na mambo mengi ambayo hupendi, kukutana na magonjwa na kuvunjika moyo. Lakini unapotembea njia hii, maisha yako na bahati zako ziko chini ya ulinzi wa Mungu kabisa. Mungu anakupa hakikisho halisi litakalodumu maisha yako yote, kwani Yeye yuko kando yako, anakulinda na kukutunza. Bila kujua haya, unakua. Unaanza kukutana na mambo mapya na unaanza kujua dunia hii na wanadamu hawa. Kila kitu ni kipya kwako. Unapenda kufanya mambo yako na unapenda kufanya kile unachopenda. Unaishi katika ubinadamu wako mwenyewe, unaishi katika nafasi yako ya kuishi na huna hata kiasi kidogo cha mtazamo kuhusu kuwepo kwa Mungu. Lakini Mungu anakulinda katika kila hatua ya njia unapokua, na Anakutazama unapoweka kila hatua mbele. Hata unapojifunza maarifa, ama kusoma sayansi, Mungu hajawahi toka upande wako kwa hatua hata moja. Wewe ni sawa na watu wengine kwamba, katika harakati za kuja kujua na kukutana na dunia, umeanzisha mawazo yako mwenyewe, una mambo yako mwenyewe ya kupitisha muda, mambo unayopenda mwenyewe, na pia unayo matamanio ya juu. Wakati mwingi unafikiria siku zako za baadaye, wakati mwingi ukichora muhtasari wa jinsi siku zako za baadaye zinapaswa kuwa. Lakini haijalishi kitakachofanyika njiani, Mungu anaona vyote na macho wazi. Labda wewe mwenyewe umesahau siku zako za nyuma, lakini kwa Mungu, hakuna anayeweza kukuelewa bora kuliko Yeye. Unaishi chini ya macho ya Mungu, unakua, unapevuka. Wakati huu, jukumu muhimu la Mungu ni kitu ambacho hakuna yeyote kamwe hufahamu, kitu ambacho hakuna yeyote anajua. Mungu hakika hakuambii kukihusu. Hiki kitu muhimu ni nini? Mtu anaweza kusema kwamba ni hakikisho kuwa Mungu atamwokoa mtu. Hii inamaanisha kwamba Mungu anataka kumwokoa mtu huyu, kwa hivyo lazima Afanye hivi, na kazi hii ni muhimu sana kwa mwanadamu na Mungu. Je, mnajua hili? Inaonekana kwamba hamna hisia yoyote kuhusu hili, ama dhana yoyote kuhusu hili, kwa hivyo nitawaambia. Kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu amefanya kazi nyingi sana kwako, lakini Hakupi maelezo moja baada ya nyingine ya kila kitu Amefanya. Mungu hakukuruhusu kujua, na Hakukwambia sivyo? Hata hivyo, kwa mwanadamu, kila kitu anachofanya Mungu ni muhimu. Kwa Mungu, ni kitu ambacho lazima Afanye. Katika moyo wake kuna kitu muhimu Anapaswa kufanya ambacho kinazidi yoyote ya mambo haya. Yaani, kutoka alipozaliwa mwanadamu hadi sasa, Mungu lazima ahakikishe usalama wa kila mmoja wao. Baada ya kusikia maneno haya, mnaweza kuhisi kana kwamba hamwelewi kikamilifu, kusema “usalama huu ni muhimu sana?” Kwa hivyo ni nini maana halisi ya “usalama”? Labda mnauelewa kumaanisha amani ama pengine mnauelewa kumaanisha kutopitia maafa ama msiba wowote, kuishi vyema, kuishi maisha ya kawaida. Lakini katika mioyo yenu lazima mjue kwamba si rahisi hivyo. Kwa hivyo ni nini hasa kitu hiki ambacho Nimekuwa nikizungumzia, ambacho Mungu anapaswa kufanya? Usalama unamaanisha nini kwa Mungu? Kuna hakikisho lolote la usalama wenu? La. Kwa hivyo ni nini hiki ambacho Mungu anafanya? Usalama huu unamaanisha humezwi na Shetani. Je, jambo hili ni muhimu? Wewe humezwi na Shetani, kwa hivyo hili linahusisha usalama wako, au la? Hili linahusisha usalama wako binafsi, na hakuwezi kuwa na lolote muhimu zaidi. Baada ya wewe kumezwa na Shetani, nafsi yako wala mwili wako si vya Mungu tena. Mungu hatakuokoa tena. Mungu huacha nafsi kama hiyo na huacha watu kama hao. Kwa hivyo Nasema kitu muhimu sana ambacho Mungu anapaswa kufanya ni kuhakikishia usalama wako, kuhakikisha kwamba hutamezwa na Shetani. Hili ni muhimu kiasi, silo? Kwa hivyo mbona hamwezi kujibu? Inaonekana kwamba hamwezi kuhisi wema mkubwa wa Mungu!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp