Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Recital-latest-expression
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Maneno Yaliyo Bora Kabisa Kutoka kwa Mungu (Dondoo)
Maneno Yaliyo Bora Kabisa Kutoka kwa Mungu (Dondoo)

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipia gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung'aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Maisha ya Mungu, huishi milele bila kubadilika katika kusumbuka kwa mbingu na nchi. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.

Umetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ni Mungu tu Ana Njia ya Uzima

1 Njia ya uzima si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuwa nacho; si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuipata kwa urahisi. Kwani uzima unatoka tu kwa Mungu, ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima, ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima. Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima, na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele. Tangu uumbaji wa dunia, Mungu amefanya kazi nyingi ambazo zinahusisha umuhimu wa maisha, zinazoletea mwanadamu uzima; Amelipa gharama kubwa ili mwanadamu apate uzima. Kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele; Yeye ndiye njia ambayo kwayo mwanadamu hupata ufufuo.

2 Mungu hajakosa kamwe kuwa katika moyo wa mwanadamu, Kila wakati Anaishi kati ya mwanadamu. Yeye ni nguvu inayoendesha kuishi kwao, na msingi wa uwepo wao; Yeye ni amana tajiri kwa mwanadamu kuishi kwa kumtegemea. Anafanya mwanadamu kuzaliwa tena, na kuwafanya waishi kwa nguvu katika majukumu yao tofauti. ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima, ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima. Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima, na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele. Kwa sababu ya mamlaka Yake na nguvu Yake ya maisha isiokosa, mwanadamu ameishi kizazi baada ya kizazi. Mamlaka ya maisha ya Mungu yanamsaidia mwanadamu bila kukoma; Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida amewahi kulipa.

3 Nguvu ya maisha ya Mungu inatawala juu ya mamlaka yote; na inazidi nguvu zote. Maisha Yake ni ya milele, mamlaka Yake ni ya ajabu. Hakuna kiumbe yeyote aliyeumbwa anayeweza kushinda nguvu ya maisha Yake, ambayo ipo na inaangaza nuru inayong’aa wakati wowote ama mahali, wakati wowote ama mahali. ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima, ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima. Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima, na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele. Mbingu, dunia inaweza kubadilika sana, maisha ya Mungu hayabadiliki kamwe. Vitu vyote vimeenda, lakini maisha ya Mungu bado ipo, kwani Mungu ni chanzo na asili ya uwepo wa vitu vyote, kwani Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele.

4 Maisha ya Mungu yanatoka kwa Mungu, mbingu ipo kwa sababu ya Mungu, na dunia ipo kwa sababu ya nguvu ya maisha ya Mungu. Hakuna kitu kilicho na umuhimu kinachoweza kuvuka mipaka ya mamlaka ya Mungu, na hakuna kitu kilicho na nguvu kinaweza kujiweka huru kutoka kwa mipaka ya mamlaka ya Mungu. ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima, ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima. Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima, na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele. Katika njia hii, haijalishi wao ni nani, wanadamu wote lazima watii, lazima watii utawala wa Mungu, aishi chini ya amri Yake. Hakuna anayeweza kuepuka, hakuna anayeweza kuepuka, kuepuka kutoka kwa udhibiti Wake.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji