Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 354

Mwanzoni, Nilitaka kuwapa ukweli zaidi, lakini kwa sababu mtazamo wenu kwa ukweli ni baridi sana na usiojali, Nimesalimu amri. Sipendi kuona jitihada Zangu zikipotea bure, na pia Sipendi kuona watu wakishika maneno Yangu na ilhali katika kila sehemu wanafanya yale ya Kunipinga Mimi, kunidhuru Mimi, na kunikufuru. Kwa sababu ya mtazamo wenu na utu wenu, Ninawapa sehemu kidogo tu ya maneno yaliyo muhimu zaidi kwenu kama jaribio Langu kwa wanadamu. Ni mpaka sasa ndiyo Naweza thibitisha kwa hakika kwamba uamuzi na mipango Niliyoweka ni kulingana na yale mnayohitaji na kuwa mtazamo Wangu kwa wanadamu uko sawa. Miaka yenu mingi ya matendo mbele Yangu imenipa jibu ambalo Sijawahi kupata hapo awali. Na swali la jibu hili ni: “Mtazamo wa mwanadamu mbele ya ukweli na Mungu wa ukweli ni upi?” Juhudi ambazo Nimemwagia mwanadamu ni dhihirisho la kiini Changu cha kumpenda mwandamu, na vitendo na matendo ya mwanadamu mbele Yangu pia yamedhihirisha kiini cha mwanadamu cha kuchukia ukweli na kunipinga Mimi. Katika wakati wote Mimi hujali wale wote ambao wamenifuata, lakini hakuna wakati ambao wale wanaonifuata wameweza kupokea neno Langu; hawana uwezo kabisa wa kukubali hata maoni yanayotoka Kwangu. Hili ndilo hunihuzunisha zaidi ya yote. Hakuna anayeweza kunielewa na, zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kunikubali, hata ingawa mtazamo Wangu ni wa kweli na maneno Yangu ni ya upole. Wote wanafanya kazi Niliyowaaminia kuifanya kulingana na nia yao ya asili; hawatafuti nia Zangu, wala kuuliza maombi Yangu. Bado wanadai kuwa Wananihudumia kwa uaminifu, wakati huu wote wakiwa wananiasi. Wengi wanaamini kuwa ukweli usiokubalika nao au ukweli ambao hawawezi kutia vitendoni sio ukweli. Kwa watu kama hawa, ukweli Wangu unakuwa kitu cha kukataliwa na kutupiliwa kando. Kwa wakati uo huo Ninakuwa mmoja anayetambuliwa na mwanadamu kwa neno tu kama Mungu, lakini pia kuchukuliwa kama mtu wa nje asiyekuwa ukweli, njia na uhai. Hakuna anyejua ukweli huu: Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye msambazaji wa binadamu na kiongozi wa pekee wa mwanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni ya ukweli, na kuwa ni yale ambayo mwanadamu lazima apewe, na, zaidi ya yote, yale ambayo mwanadamu anafaa akubali. Nitawaruhusu wote wanaonifuata wajue ukweli huu: Wote wasioyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale wasioyaweka maneno Yangu katika vitendo, wale wasiopata sababu ndani ya maneno Yangu, na wale wasiopata wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp