Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 193

03/10/2020

Wakati ambapo, katika Enzi ya Neema, Mungu alirudi kwa mbingu ya tatu, kazi ya Mungu ya kuwakomboa wanadamu wote ilikuwa kwa kweli tayari imeendelea katika tendo lake la kumaliza. Vyote vilivyobaki duniani vilikuwa msalaba ambao Yesu aliubeba, sanda ya kitani ambayo Yesu alifungiwa ndani, na taji ya miiba na joho la rangi nyekundu ambavyo Yesu alivaa (hivi vilikuwa vitu ambavyo Wayahudi walitumia kumdhihaki Yeye). Yaani, baada ya kazi ya kusulubiwa kwa Yesu isababishe mhemko mkubwa, mambo yalitulia tena. Tangu wakati huo na kuendelea, wanafunzi wa Yesu wakaanza kuendeleza kazi Yake, wakiyachunga na kunyunyizia katika makanisa kila mahali. Maudhui ya kazi yao yalikuwa haya: kuwafanya watu wote watubu, waungame dhambi zao, na wabatizwe; mitume wote wakieneza hadithi ya ndani ya kusulubiwa kwa Yesu na kile kilifanyika kwa kweli, kila mtu asiweze kujizuia kuanguka chini mbele za Yesu kuungama dhambi zake, na zaidi ya hayo mitume wakieneza kila mahali maneno yaliyonenwa na Yesu na sheria na amri Alizozianzisha. Kuanzia wakati huo ujenzi wa makanisa ulianza katika Enzi ya Neema. Kile ambacho Yesu alizungumzia wakati wa enzi hiyo pia kililenga maisha ya mwanadamu na mapenzi ya Baba wa mbinguni. Ni kwa sababu tu enzi hizo ni tofauti ndiyo nyingi za semi na matendo hayo yanatofautiana sana na ya leo. Lakini kiini cha vyote viwili ni sawa. Yote mawili kwa uhakika na usahihi ni takriban kazi ya Roho wa Mungu katika mwili kabisa. Aina hii ya kazi na matamko yameendelea wakati wote mpaka siku hii, na kwa hivyo kitu cha aina hii bado kinashirikiwa kati ya mashirika ya dini leo na hakijabadilika hata kidogo. Wakati ambapo kazi ya Yesu ilikamilishwa, na makanisa tayari yalikuwa yameingia kwenye njia sahihi ya Yesu Kristo, Mungu bado alianzisha mpango Wake wa hatua nyingine ya kazi Yake, jambo la kupata mwili katika siku za mwisho. Kwa mwanadamu, Mungu kusulubiwa kulihitimisha kazi ya Mungu kupata mwili, Aliwakomboa binadamu wote, na Akamruhusu kuteka ufunguo wa Kuzimu. Kila mtu anadhani kwamba kazi ya Mungu imekamilika kikamilifu. Kwa uhalisia, kwa Mungu, ni sehemu ndogo tu ya kazi Yake ndiyo imekamilika. Amemkomboa tu binadamu; Hajamshinda mwanadamu, wala kubadilisha ubaya wa Shetani kwa binadamu. Hiyo ndiyo maana Mungu Anasema, “Ingawa mwili Wangu ulipitia maumivu ya kifo, hilo sio lengo lote la Mimi kupata mwili. Yesu ni Mwana Wangu mpendwa na Alisulubishwa msalabani kwa ajili Yangu, lakini hakukamilisha kikamilifu kazi Yangu. Alifanya tu sehemu.” Hivyo Mungu Akaanza mpango wa mzunguko wa pili ili kuendeleza kazi ya Mungu kupata mwili. Lengo kuu la Mungu ni kumkamilisha na kumpata kila mmoja aokolewe kutoka katika mikono ya Shetani, hiyo ndiyo sababu Mungu Alijiandaa tena kujihatarisha kuja katika mwili. Maana ya “kupata mwili” ni Yule ambaye haleti utukufu (kwa sababu kazi ya Mungu bado haijamalizika), lakini yule anayeonekana katika utambulisho wa Mwana mpendwa, na Yeye ndiye Kristo, ambaye Mungu amependezwa naye. Ndiyo maana hili linasemekana kuwa “kujitayarisha kwa ajili ya hatari”. Mwili ni wenye nguvu kidogo sana na lazima utahadhari sana, na nguvu Yake ni tofauti sana na mamlaka ya Baba wa mbinguni; Yeye hutimiza tu huduma ya mwili, Akifanikisha kazi na agizo la Mungu Baba bila kujihusisha katika kazi nyingine. Yeye hufanikisha tu sehemu moja ya kazi. Hii ndiyo maana Mungu anaitwa “Kristo” alipokuja duniani. Hii ndiyo maana ya ndani. Sababu ya kusema kwamba kuja huko kunaandamana na majaribu ni kwa kuwa mradi wa kazi mmoja pekee ndio unafanikishwa. Zaidi ya hayo, sababu Mungu Baba humwita tu “Kristo” na “Mwana mpendwa” na Hajampa utukufu wote ni hasa kwa vile mwili uliokuwa mwili huja kufanya mradi wa kazi moja, sio kumwakilisha Baba aliye mbinguni, bali kutimiza huduma ya Mwana mpendwa. Mwana mpendwa atakapomaliza agizo lote Alilokubali kubeba juu ya mabega Yake, Baba atampa Yeye utukufu kamili pamoja na utambulisho wa Baba. Mtu anaweza kusema kwamba hii ni kanuni ya mbinguni. Kwa sababu Yule ambaye amekuja katika mwili na Baba aliye mbinguni wako katika hali mbili tofauti, hao wawili huonana tu katika Roho, Baba akimtazama kwa makini Mwana mpendwa lakini Mwana asiweze kumwona Baba kutoka mbali. Ni kwa sababu kazi ya mwili ni ndogo sana na Ana uwezo wa kuuawa wakati wowote, kwamba kuja huku kunasemekana kuambatana na hatari kuu. Hii ni sawa na Mungu mara tena kumwachilia Mwana Wake mpendwa na kumweka ndani ya mdomo wa chui mkubwa mwenye milia. Ni hatari kwa maisha kwamba Mungu alimweka Yeye mahali ambapo Shetani amekolea sana. Hata kwa kupata mashaka kama hayo, Mungu bado alimkabidhi Mwana Wake mpendwa kwa watu wa mahali pachafu, fisadi ili wao “wamlee.” Hii ni kwa sababu ni njia pekee ya kazi ya Mungu kuleta maana kabisa na njia pekee ya kutimiza mapenzi yote ya Mungu Baba na kufanikisha sehemu ya mwisho ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Yesu alifanikisha tu hatua moja ya kazi ya Mungu Baba. Kwa sababu ya kizuizi cha mwili uliopata mwili na tofauti katika kazi iliyofanikishwa, Yesu Mwenyewe hakujua kwamba kungekuwa na kurudi kwa pili kwa mwili. Kwa hivyo hakuna mfafanuaji au nabii wa Biblia aliyethubutu kutabiri wazi kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho, yaani, angekuja katika mwili tena ili kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake katika mwili. Kwa hivyo, hakuna aliyetambua kwamba Mungu tayari Alikuwa amejificha kwa muda mrefu katika mwili. Si ajabu, kwani ilikuwa tu baada ya Yesu kufufuka na kupaa mbinguni ndipo Akakubali agizo hili, kwa hiyo hakuna unabii ulio wazi kuhusu kupata mwili kwa Mungu mara pili, na ni jambo lisilofikirika na akili ya binadamu. Katika vitabu vyote vingi vya unabii ndani ya Biblia, hakuna maneno yanayotaja hili kwa dhahiri. Lakini Yesu alipokuja kufanya kazi, tayari kulikuwa na unabii wa wazi uliosema kwamba bikira atashika uja uzito, naye atamzaa mwana, kumaanisha kwamba mimba Yake ilipatikana kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hata hivyo, Mungu bado alisema hili lilifanyika kwa hatari ya kifo, hivyo hali ingekuwaje ya hatari katika hali ya leo? Si ajabu Mungu asema kwamba kupata mwili wakati huu kuna hatari mara elfu zaidi kuliko zile za wakati wa Enzi ya Neema. Katika maeneo mengi, Mungu Alitabiri kupata kundi la washindi katika nchi ya Sinimu. Ni katika Mashariki mwa ulimwengu ambapo washindi watapatwa, hivyo nchi ambapo Mungu anashukia katika kupata mwili Kwake mara ya pili bila shaka ni nchi ya Sinimu, mahali ambapo joka jekundu linaishi. Hapo Mungu Atawapata warithi wa joka kuu jekundu na litashindwa na kuaibishwa. Mungu Anataka kuwaamsha watu hawa walioteseka sana, kuwaamsha kabisa, na kuwafanya waondoke katika ukungu na kulikataa joka kuu jekundu. Mungu Anataka Awaamshe kutoka katika ndoto zao, kuwafanya waelewe tabia ya joka kuu jekundu, kuutoa moyo wao wote kwa Mungu, kuinuka kutoka katika nguvu kandamizi za giza, kusimama Mashariki mwa dunia, na kuwa uthibitisho wa ushindi wa Mungu. Baada ya hapo Mungu Atakuwa Amepata utukufu. Kwa sababu hii tu, kazi ambayo ilisitishwa Israeli Mungu Aliipeleka katika nchi ambapo linakaa joka kuu jekundu na, takribani miaka elfu mbili baada ya kuondoka, Amekuja tena katika mwili ili kuendeleza kazi ya Enzi ya Neema. Mwanadamu anashuhudia kwa macho yake, Mungu Akizindua kazi mpya katika mwili. Lakini kwa Mungu, Anaendeleza kazi ya Enzi ya Neema, kwa mwachano wa miaka elfu kadhaa, na badiliko tu la eneo la kufanyia kazi na mradi wa kazi. Ingawa taswira ya mwili ambayo Mungu Ameichukua katika kazi ya leo ni mtu mwingine tofauti na Yesu, Wanashiriki hulka na mzizi mmoja, na wanatoka katika chanzo kimoja. Pengine wana tofauti za umbo la nje, lakini kweli za ndani za kazi Zao zinafanana kabisa. Hata hivyo, enzi zenyewe, ni tofauti kama ilivyo usiku na mchana. Inawezekanaje kazi ya Mungu isibadilike? Au inawezekanaje kazi ziingiliane?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp