Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 124

Uhuru: Awamu ya Tatu

Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuuaga kabisa ule ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na viungo mbalimbali katika msururu wa hatima yake. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.

1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba

Kama kuzaliwa kwa mtu na kulelewa kwake ni “kipindi cha matayarisho” katika safari ya mtu maishani, kuweka lile jiwe la msingi katika hatima ya mtu, basi uhuru wa mtu ndio mazungumzo nafsi ya kufungua hatima ya maisha ya mtu. Kama kuzaliwa na kukua kwa mtu ni utajiri ambao wameweza kulimbikiza kwa minajili ya hatima yao maishani, basi uhuru wa mtu huyo unaanza wakati ule wanaanza kutumia au kuongeza utajiri huo. Wakati mtu anawaacha wazazi na kuwa huru, masharti ya kijamii ambayo anakabiliana nayo, na aina ya kazi na ajira inayopatikana kwa mtu, vyote vinaamriwa na hatima na havina uhusiano wowote na wazazi wa mtu. Baadhi ya watu huchagua kozi nzuri katika chuo na huishia kupata kazi ya kutosheleza baada ya kuhitimu, na hivyo basi kupiga hatua ya kwanza ya mafanikio katika safari yao ya maisha. Baadhi ya watu hujifunza na kumiliki mbinu nyingi tofauti na ilhali hawapati kazi katu ambayo inawafaa au hawapati cheo chao, bila kutaja kwamba hawana ajira yoyote; wakati wa safari ya maisha yao wanajipata wakiwa wamekwazwa katika kila kona, wameandamwa na matatizo, matumaini yao madogo na maisha yao hayana uhakika. Baadhi ya watu wanatia bidii katika masomo yao, ilhali wanakosa kwa karibu sana fursa zao zote za kupokea elimu ya juu zaidi, na wanaonekana kuwa na hatima ya kutotimiza fanisi, matamanio yao ya kwanza kabisa katika safari yao ya maisha yanatowekea tu hewani. Bila kujua kama barabara iliyo mbele ni laini au yenye miamba, wanahisi kwa mara ya kwanza namna ambavyo hatima ya binadamu imejaa vitu vya kubadilikabadilika, na wanachukulia maisha kwa tumaini na hofu. Baadhi ya watu, licha ya kutokuwa na elimu nzuri sana, huandika vitabu na kutimiza kiwango cha umaarufu; baadhi, ingawaje hawajui kusoma na kuandika sana, huunda pesa katika biashara na hivyo basi wanaweza kujikidhi…. Kazi anayochagua mtu, namna mtu anavyozumbua riziki: je, watu wanao udhibiti wowote kuhusu, kama wanaweza kufanya uchaguzi mzuri au uchaguzi mbaya? Je, yanapatana na matamanio na uamuzi wao? Watu wengi zaidi hutamani wangeweza kufanya kazi kidogo na kupata mapato mengi zaidi, wasitie bidii sana katika jua na mvua, wavalie vyema, wametemete na kung’aa wakiwa kila pahali, kuwapita sana wengine kwa uwezo, na kuleta heshima kwa mababu zao. Matamanio ya watu ni timilifu kweli, lakini watu wanapochukua hatua zao za kwanza katika safari ya maisha yao, wanaanza kwa utaratibu kutambua namna ambavyo hatima ya binadamu ilivyo na hali ya kutokuwa timilifu, na kwa mara ya kwanza wanang’amua kwa kweli hoja hii kwamba, ingawaje mtu anaweza kufanya mipango thabiti kwa minajili ya mustakabali wake, ingawaje mtu anaweza kuhodhi mawazoni ndoto shupavu, hakuna yule aliye na uwezo au nguvu za kutambua ndoto zake mwenyewe, hakuna yule aliye katika hali ya kudhibiti mustakabali wake. Siku zote kutakuwepo na kitalifa fulani kati ya ndoto za mtu na uhalisia ambao lazima mtu akabiliane nao; mambo siku zote hayawi vile ambavyo mtu angetaka yawe, na watu wanapokumbwa na uhalisi kama huu hawawezi kutimiza hali ya kutosheka au kuridhika. Baadhi ya watu wataenda hadi kiwango chochote cha kufikirika, wataweza kutia bidii za kipekee na kujitolea pakubwa kwa minajili ya riziki na mustakabali wao, katika kujaribu kubadilisha hatima yao wenyewe. Lakini hatimaye, hata kama wataweza kutambua ndoto na matamanio yao kupitia kwa njia ya bidii yao wenyewe, hawawezi kubadilisha hatima zao, na haijalishi watajaribu vipi kwa njia ya ukaidi hawatawahi kuzidi kile ambacho hatima yao imewapangia. Licha ya tofauti katika uwezo, kiwango cha akili, na hiari ya kutenda, watu wote ni sawa mbele ya hatima, jambo ambalo halileti utofauti kati ya wakubwa na wadogo, wale wa kiwango kile cha juu na cha chini, wanaotukuzwa na wakatili. Ile kazi ambayo mtu anafuatilia, kile anachofanya mtu ili kuzumbua riziki, na kiwango kipi cha utajiri ambacho mtu amelimbikiza katika maisha yake vyote haviamuliwi na wazazi wa mtu, vipaji vya mtu, jitihada za mtu au malengo ya mtu, vyote vinaamuliwa kabla na Muumba.

2. Kuwaacha Wazazi wa Mtu na Kuanza kwa Bidii Kuendeleza Wajibu Wako Kwenye Ukumbi wa Sanaa wa Maisha

Wakati mtu anapofikia ukomavu, mtu anaweza kuacha wazazi wake na kulikanyaga guu lake nje kivyake, na ni katika wakati huu ambapo mtu huanza kwa kweli kuonyesha wajibu wake binafsi, kwamba kazi maalum ya mtu maishani husita kutoeleweka na polepole kuanza kuwa wazi. Kimsingi mtu huyo bado huonyesha uhusiano wa karibu na wazazi wake, lakini kwa sababu kazi yake maalum na wajibu anaoendeleza katika maisha huwa hauna uhusiano wowote na mama na baba wa mtu huyo, kwa hakika uhusiano huu wa karibu huvunjika polepole kwa kadiri ambavyo mtu anazidi kuendelea kuwa huru. Kutoka katika mtazamo wa kibiolojia, watu bado hawana budi kutegemea wazazi katika njia za kufichika akilini, lakini kama tutaongea kwa malengo, mara baada ya kukua huwa na maisha tofauti kabisa na yale ya wazazi wao, na wataweza kutekeleza wajibu watakaoamua kufanya kwa uhuru wao. Mbali na kuzaliwa na kulea watoto, jukumu la kila mzazi katika maisha ya mtoto ni kuweza kuwapatia tu mazingira rasmi ya kukulia ndani, bila malipo yoyote isipokuwa kule kuamuliwa kabla kwa Muumba ambako kunachukua mwelekeo katika hatima ya mtu huyu husika. Hakuna anayeweza kudhibiti ni mustakabali gani ambao mtu atakuwa nao; huwa umeamuliwa kabla na mapema sana, na hata wazazi wa mtu hawawezi kubadilisha hatima yake. Kulingana na mambo ya hatima, kila mtu yuko huru na kila mtu anayo hatima yake. Kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote wanaweza kuiondoa hatima ya mtu katika maisha au kusisitizia ushawishi wowote ule mdogo katika wajibu ambao mtu huendeleza maishani. Inaweza kusemekana kwamba, familia ambayo mtu ameamuliwa kuzaliwa ndani, na mazingira ambayo mtu atakulia ndani, ni yale masharti ya awali ya kutimiza kazi maalum ya mtu maishani. Yote haya hayaamui kwa vyovyote vile hatima ya mtu katika maisha au aina ya hatima ambayo mtu huyo atatimiza katika kazi yake maalum. Na kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote yule wanaweza kusaidia katika kutimiza kazi hii maalum katika maisha, hakuna watu wowote wa ukoo wanaweza kusaidia mtu kuchukua wajibu huu katika maisha. Vile ambavyo mtu hutimiza kazi yake maalum na katika aina gani ya mazingira ya kuishi ambayo mtu hutekeleza wajibu wake, vyote vinaamuliwa na hatima ya mtu maishani. Kwa maneno mengine, hakuna masharti yoyote mengine yenye malengo yanaweza kuathiri kazi maalum ya mtu, ambayo imeamuliwa kabla na Muumba. Watu wote hukomaa katika mazingira yao binafsi ya kukulia, na kisha kwa taratibu, hatua kwa hatua, huanza safari katika barabara zao binafsi za maisha, hutimiza hatima walizopangiwa na Muumba, kwa kawaida, bila hiari wao huingia katika bahari kuu ya binadamu na kuchukua nafasi zao binafsi katika maisha, pale ambapo wao huanza kutimiza majukumu yao kama viumbe vilivyoumbwa kwa minajili ya kuamuliwa kabla kwa Muumba, kwa minajili ya ukuu Wake.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp