Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 167

23/07/2020

Hadithi ya 1. Mbegu, Ardhi, Mti, Mwanga wa Jua, Chiriku, na Mwanadamu

Mbegu ndogo ilidondoka ardhini. Baada ya mvua kubwa kunyesha, mbegu ilianza kuchipuka na mizizi yake ikamea taratibu kwenda ardhini. Chipuko lilirefuka kadri muda ulivyozidi kwenda, yakivumilia upepo mkali na mvua kubwa, yakiangalia mabadiliko ya misimu kadri mwezi unavyopevuka na kufifia. Wakati wa kiangazi ardhi ilileta zawadi ya maji ili kwamba chipuko liweze kuhimili joto kali. Na kwa sababu ya ardhi, chipuko halikuhisi joto na hivyo lilihimili joto la kiangazi. Msimu wa baridi ulipokuja, ardhi ililifunika chipuko katika kumbatio la vuguvugu lake na kushikamana kwa nguvu. Na kwa sababu ya vuguvugu la ardhi, chipuko lilihimili baridi kali, likivuka bila kudhurika katika dhoruba ya msimu wa baridi na barafu za msimu. Likivikwa na ardhi, chipuko lilikua kwa ujasiri na lilikuwa na furaha. Lilirefuka na kujivunia malezi yasiyokuwa ya ubinafsi ambayo ardhi iliyatoa. Chipuko lilikua kwa furaha. Liliimba wakati mvua ilipokuwa ikinyesha na kucheza na kuyumba kadri upepo ulivyokuwa ukivuma. Na hivyo, chipuko na ardhi hutegemeana …

Miaka ilipita, na chipuko sasa lilikuwa mnara wa mti. Lilikuza matawi manene juu yake yaliyokuwa na majani yasiyohesabika na kusimama imara juu ya nchi. Mizizi ya mti ilimea aridhini kama ilivyomea hapo kabla, lakini sasa ilizama kabisa ardhini chini kabisa. Kile ambacho mwanzo kilililinda chipuko sasa kilikuwa msingi wa mti mkubwa sana.

Mwale wa mwanga wa jua ulimulika mti na shina likatikisika. Mti ulitoa nje matawi yake kwa upana na kufaidi sana kutoka kwenye mwanga. Ardhi chini ilipumua kwa wizani pamoja na mti, na ardhi ilihisi kufanywa upya. Baada ya hapo tu, upepo mwanana ulivuma katika matawi, na mti ulifurahia sana, ukiwa na nguvu. Na hivyo, mti na mwanga wa jua vinategemeana …

Watu walikaa katika kivuli tulivu cha mti na wakafurahia hewa changamfu inayonukia vizuri. Hewa ilitakasa mioyo na mapafu yao, na ilitakasa damu ndani yao. Watu hawakuhisi tena kuchoka au kuelemewa. Na hivyo, watu na miti wanategemeana …

Kundi la chiriku waliimba kwa uchangamfu walivyokuwa wakitua kwenye matawi ya mti. Pengine walikuwa wanamwepuka adui fulani, au walikuwa wanazaliana na kuwalea watoto wao, au pengine walikuwa wanapata pumziko fupi. Na hivyo, ndege na mti wanategemeana …

Mizizi ya mti, ikiwa imesokotana na kusongamana, ilijikita chini kabisa ardhini. Shina lake liliifunika ardhi dhidi ya upepo na mvua na kuyatoa nje matawi yake makubwa na kuilinda ardhi chini yake, na mti ulifanya hivi kwa sababu ardhi ni mama yake. Yanaishi pamoja, yanategemeana, na kamwe hayatatengana …

Mambo yote Niliyoyazungumzia ni mambo ambayo mmeshawahi kuyaona hapo awali, kama vile mbegu, mnajua kuhusiana na hili, sio? Mbegu kukua na kuwa mti unaweza usiwe mchakato unaouangalia katika maelezo ya kina, lakini unajua kwamba ni ukweli, sio? Unajua kuhusu ardhi na mwanga wa jua. Taswira ya chiriku wakitua mtini ni kitu ambacho watu wote wamekwishakiona, sio? (Ndiyo.) Na watu kutuliza joto chini ya kivuli cha mti, wote mmekwishawahi kuona, sio? (Tumeona hilo.) Sasa, mnapata hisia gani mnapoona mifano yote hii katika taswira moja? (Upatanifu.) Je, mifano yote hii iliyopo katika taswira hii inatoka kwa Mungu? (Ndiyo.) Kwa kuwa inatoka kwa Mungu, Mungu anajua thamani na umuhimu wa mifano hii kadhaa inayokaa pamoja ardhini. Mungu alipoviumba vitu vyote, Alikuwa na mpango kwa kila kitu, na kila kitu Alichokiumba huonesha makusudi Yake na Yeye Hujaza uhai ndani yao. Alitengeneza mazingira hai kwa ajili ya binadamu, ambayo yamejadiliwa katika hadithi tuliyoisikia. Imejadili hali ya kutegemeana baina ya mbegu na ardhi; ardhi inastawisha mbegu na mbegu inafungamana na ardhi. Uhusiano kati ya hivi vitu viwili uliamuliwa kabla na Mungu kuanzia mwanzoni kabisa, sio? (Ndiyo.) Mti, mwanga wa jua, chiriku, na mwanadamu katika taswira hii, je, ni mifano ya mazingira hai ambayo Mungu aliyaumba kwa ajili ya mwanadamu? (Ndiyo.) Kwanza, je, mti unaweza kuiacha ardhi? (Hapana.) Je, mti unaweza kuishi bila mwanga wa jua? (Hapana.) Basi kusudi la Mungu la kuumba mti lilikuwa ni nini? Je, tunaweza kusema kuwa ilikuwa tu ni kwa ajili ya ardhi? Je, tunaweza kusema ilikuwa tu ni kwa ajili ya chiriku? Je, tunaweza kusema ilikuwa tu ni kwa ajili ya watu? (Hapana.) Kuna uhusianao gani kati yao? Uhusianao kati yao ni wa kutegemeana ambapo haviwezi kutengana. Yaani, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku, na watu wanategemeana kwa ajili ya kuishi na wanaleana. Mti unailinda ardhi wakati ardhi inaulea mti; mwanga wa jua unatoa huduma kwa mti, wakati mti unatengeneza hewa nzuri kutoka katika mwanga wa jua, na husaidia kuituliza ardhi kutokana na joto la mwanga wa jua. Nani anayefaidika mwishoni? Mwanadamu ndiye anayefaidika, siyo? Na hii ndiyo kanuni juu ya kwa nini Mungu alifanya mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu na ambaye ndiye lengo kuu kwa ajili yake. Ingawa hii ni taswira rahisi, tunaweza kuona hekima za Mungu na nia yake. Binadamu hawezi kuishi bila ardhi, au bila miti, au bila chiriku na mwanga wa jua, sio? Ingawa ilikuwa ni hadithi, ni mfano mdogo wa uumbaji wa Mungu wa ulimwengu na fadhili Zake za mazingira ya kuishi kwa mwanadamu.

Mungu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote kwa ajili ya mwanadamu na pia akafanya mazingira ya kuishi. Kwanza, hoja kuu tuliyoijadili katika hadithi ni mwingiliano wa mahusiano na hali ya kutegemeana ya vitu vyote. Chini ya kanuni hii, mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu yamelindwa, yanaendelea kuishi na kudumu; kwa sababu ya uwepo wa mazingira haya hai, mwanadamu anaweza akastawi na kuzaliana. Tuliona mti, ardhi, mwanga wa jua, na chiriku, na watu katika tukio. Mungu alikuwepo pia? Watu wanaweza wakose kuiona, sio? Lakini watu wanaweza kuona kanuni za mahusiano ya kuingiliana kati ya vitu katika tukio; ni kupitia kanuni hizi ndipo watu wanaweza kuona kwamba Mungu yupo na kwamba ni Mtawala. Mungu anatumia kanuni hizi na sheria kulinda uhai na uwepo wa vitu vyote. Ni kwa njia hii ndipo Anavikimu vitu vyote na Anamkimu binadamu. Je, hadithi hii ina uhusiano wowote na dhamira tuliyoijadili? Kwa juujuu inaonekana kama hakuna uhusiano, lakini kwa uhalisia, kanuni ambazo Mungu anazifanya kama Muumbaji na utawala Wake juu ya vitu vyote zinahusiana kwa karibu sana na Yeye kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote na zimeunganika bila kuachana. Sio? (Ndiyo.) Umejifunza angalau kidogo, sio?

Mungu ni Bwana wa kanuni zinazoudhibiti ulimwengu, Anadhibiti kanuni zinazoongoza kuishi kwa vitu vyote, na pia Anadhibiti ulimwengu na vitu vyote kiasi kwamba vinaweza kuishi pamoja; Anaifanya ili kwamba visikwishe au kutoweka ili kwamba binadamu aendelee kuishi, binadamu anaweza kuishi katika mazingira hayo kupitia uongozi wa Mungu. Kanuni hizi zinazoongoza vitu vyote zipo chini ya utawala wa Mungu, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia. Ni lini miti itachipuka, ni lini mvua itanyesha, ni maji kiasi gani na virutubisho kiasi gani ardhi itaipatia mimea, ni katika msimu gani majani yatapukutika, ni katika msimu gani miti itazaa matunda, ni nishati kiasi gani jua litaipatia miti, miti itatoa nini kutoka katika nishati inayopata kutoka juani—haya ni mambo yote ambayo Mungu alikuwa amekwishayapangilia tayari Alipouumba ulimwengu na ni sheria ambazo haziwezi kuvunjwa na mwanadamu. Vitu vilivyoumbwa na Mungu—ama ni hai au vinaonekana kwa watu si hai—vyote vipo mikononi mwa Mungu na chini ya utawala Wake. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuvunja kanuni hii. Hii ni kusema, Mungu alipoviumba vitu vyote Aliweka kanuni ya jinsi vinavyopaswa kuwa. Miti isingeweza kuzamisha mizizi, kuchipua na kukua bila ardhi. Ardhi isingekuwa na miti, ingekauka. Sio? Pia, mti ni makazi ya chiriku, ni sehemu ambapo wanapata kujikinga dhidi ya upepo. Je, ingekuwa sawa ikiwa miti ingekuwa bila mwanga wa jua? (Isingekuwa sawa.) Ikiwa miti ingekuwa na ardhi peke yake hiyo isingefanya kazi. Hii yote ni kwa ajili ya mwanadamu na kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Mwanadamu anapokea hewa safi kutoka kwenye miti, na anaishi katika ardhi inayomlinda. Mwanadamu hawezi kuishi bila mwanga wa jua, mwanadamu hawezi kuishi bila viumbe hai mbalimbali. Ingawa uhusiano baina ya vitu hivi ni changamani, mnapaswa kukumbuka kwamba Mungu alitengeneza kanuni ambazo zinaongoza vitu vyote ili kwamba viweze kuishi kwa kuhusiana na kutegemeana; kila kitu alichokiumba kina thamani na umuhimu. Ikiwa Mungu aliumba kitu bila kuwa na umuhimu, Mungu angeacha kipotee. Hii ni njia mojawapo Aliyoitumia katika kuvikimu vitu vyote. “Kukimu” kuna maana gani katika hadithi hii? Je, Mungu kila siku anatoka na kwenda kumwagilia mti maji? Je, mti unahitaji msaada wa Mungu ili uweze kupumua? (Hapana.) “Kukimu” hapa ina maana ya usimamizi wa Mungu wa vitu vyote baada ya uumbaji; Alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni sheria ili kufanya vitu kwenda vizuri. Mti ulikuwa wenyewe kwa kupandwa ardhini. Masharti ili uweze kukua yote yalitengenezwa na Mungu. Alitengeneza mwanga wa jua, maji, udongo, hewa, na mazingira, upepo, umande, barafu, na mvua, na misimu minne; haya ndiyo masharti ambayo mti huyahitaji ili uweze kukua, hivi ni vitu ambavyo Mungu aliviandaa. Kwa hiyo, Mungu ni chanzo cha mazingira haya hai? (Ndiyo.) Je, Mungu analazimika kwenda kila siku na kuhesabu kila jani kwa miti? Hakuna haja, sio? Mungu pia hahitaji kuusaidia mti ili uweze kupumua. Mungu pia hahitaji kuuamsha mwanga wa jua kila siku kwa kusema, “Ni muda wa kuiangazia miti sasa.” Hana haja ya kufanya hivyo. Mwanga wa jua humulika wenyewe kama ulivyoamriwa na kanuni: inapohitajika, miti huufyonza huo mwanga na wakati mwanga hauhitajiki, mti huo bado huishi ndani ya kanuni. Pengine hamwezi kuelezea jambo hili kwa uwazi, lakini ni ukweli ambao kila mtu anaweza kuona na kuukubali. Chote unachopaswa kufanya ni kutambua kwamba kanuni kwa ajili ya uwepo wa vitu vyote inatoka kwa Mungu na jua kwamba ukuaji na kuishi kwao kupo chini ya utawala wa Mungu. Unaelewa, sio?

Je, istiari imetumika katika hadithi hii, kama watu wanavyoiita? (Hapana.) Je, ni hadithi iliyopewa sifa za kibinadamu? (Hapana.) Kile Nilichokizungumza ni ukweli. Kila kitu ambacho ni hai, kila kitu ambacho kina uhai kipo chini ya utawala wa Mungu. Kila kitu kilipewa uhai baada ya Mungu kukiumba; ni uhai uliotolewa kutoka kwa Mungu na unafuata sheria na njia Alizozitengeneza kwa ajili yake. Hii haihitaji kubadilishwa na mwanadamu, na haihitaji msaada kutoka kwa mwanadamu; hivi ndivyo Mungu anavyokimu vitu vyote. Unaelewa, sio? Je, unadhani ni lazima watu watambue hili? (Ndiyo.) Hivyo, hadithi hii ina uhusiano wowote na biolojia? Je, ina uhusiano wowote na uwanja wowote wa maarifa au sayansi? (Hapana.) Hatujadili biolojia hapa na hakika hatufanyi utafiti wa kibiolojia. Je, hoja kuu tunayoizungumzia hapa ni ipi? (Kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Hii ndiyo hoja muhimu. Mnaona nini miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji? Mmeiona miti? Mmeiona ardhi? (Ndiyo.) Mmeuona mwanga wa jua, sio? Mmewaona ndege wakikaa mtini? (Ndiyo.) Je, mwanadamu anafurahia kuishi mazingira kama hayo? (Anafurahia.) Yaani, Mungu anatumia vitu vyote—vitu alivyoviumba—kudumisha makazi ya binadamu kwa ajili ya kuishi na kulinda makazi ya binadamu, na hivi ndivyo Anavyomkimu mwanadamu na anavyokimu vitu vyote.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp