Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 224

Wakati saluti kwa ufalme inapolia—ambao pia ni wakati sauti saba za radi zinanguruma—sauti hii inatetemesha mbingu na dunia, inatetemesha mbingu na kusababisha mishipa ya moyo wa kila binadamu kutetemeka. Wimbo wa taifa kwa ufalme unainuka kwa shangwe katika taifa la joka kuu jekundu, kuthibitisha kwamba Nimeliangamiza taifa la joka kuu jekundu na kisha kuanzisha ufalme Wangu. Hata la muhimu zaidi, ufalme Wangu unaanzishwa duniani. Wakati huu, Naanza kutuma malaika Wangu kwa kila mtu wa mataifa ya dunia ili waweze kuwachunga wanangu, watu Wangu; hili pia ni kukidhi mahitaji ya hatua ya pili ya kazi Yangu. Lakini Mimi binafsi Naenda mahali ambapo joka kuu jekundu limelala likiwa limejizongomeza, Nipigane nalo. Na wakati binadamu wote wanapata kunijua Mimi kutoka ndani ya mwili, na kuweza kuyaona matendo Yangu kutoka ndani ya mwili, wakati huo makazi ya joka kuu jekundu yatageuzwa kuwa jivu na kutoweka yasipatikane tena. Kama watu wa ufalme Wangu, kwa kuwa unalichukia joka kuu jekundu katika mifupa yako, ni lazima uuridhishe moyo Wangu na matendo yako na kwa njia hii uweze kuleta aibu juu ya joka. Je, unahisi kwamba joka kuu jekundu ni lenye chuki? Je, unahisi kweli kwamba yeye ndiye adui wa Mfalme wa ufalme? Je, una imani kwa kweli kwamba unaweza kuwa na ushuhuda wa ajabu Kwangu? Je, una imani kwa kweli ya kumshinda joka kuu jekundu? Haya ndiyo Ninayotaka kutoka kwako. Yote Ninayohitaji kutoka kwako ni kwamba uweze kufika mpaka hatua hii; je, utaweza kufanya hili? Je, una imani kwamba unaweza kufikia hili? Binadamu ana uwezo wa kufanya nini? Si ni afadhali Nifanye hivyo Mwenyewe? Mbona Ninasema kwamba Mimi binafsi Nateremka mahali ambapo vita hujiunga? Ninachotaka ni imani yako, sio matendo yako. Wanadamu hawana uwezo wa kupokea maneno Yangu kwa halisi, lakini wanachungulia tu kutoka kando. Na wewe umefikia malengo haya kwa njia hii? Umekuja kunijua kwa njia hii? Kwa kusema ukweli, kati ya wanadamu walio duniani, hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuniangalia Mimi moja kwa moja usoni, hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kupokea maana safi na nadhifu ya maneno Yangu. Na kwa hiyo Nimeweka mwendo wa kufaa usiokuwa wa kawaida wa kupanga mambo juu ya dunia, ili kufikia lengo Langu na kuanzisha mfano halisi Wangu mwenyewe katika mioyo ya watu, na kwa njia hii kutamatisha kipindi ambapo fikira huwa na mamlaka juu ya wanadamu.

Leo hii, Sishuki tu juu ya taifa la joka kuu jekundu, Mimi pia Nageuza uso Wangu kuelekea ulimwengu mzima, mpaka kila kitu cha mbingu kinatetemeka. Kunayo sehemu hata moja isiyopitia hukumu Yangu? Kunayo sehemu isiyo chini ya mateso Ninayovurumisha kuelekea chini? Kila Ninapoenda Nimesambaza “mbegu za maafa” ya kila aina. Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo. Nataka kufanya hata watu zaidi wapate kunijua Mimi, waweze kuniona Mimi, na kwa njia hii wapate kumcha Mungu ambaye wao hawajamwona kwa miaka mingi sana lakini ambaye, leo hii, ni halisi. Ni kwa sababu gani Niliumba dunia? Kwa sababu gani, wakati mwanadamu alipogeuka na kuwa mpotovu, Sikumwangamiza kabisa? Kwa sababu gani jamii ya wanadamu inaishi chini ya mateso? Ni kwa sababu gani Mimi Mwenyewe Niliuvaa mwili? Wakati Mimi Natekeleza kazi Yangu, binadamu haujui tu ladha ya uchungu pekee bali pia ya utamu. Kati ya watu wa dunia, ni nani asiyeishi ndani ya neema Yangu? Je, kama Sikuwapa wanadamu baraka yakinifu, nani angeweza kufurahia utoshelevu katika ulimwengu? Hakika, kuwaruhusu kuchukua nafasi kama watu Wangu si baraka pekee Niliyowapa, sivyo? Na kama msingekuwa watu Wangu na badala yake muwe watendaji-huduma, hamngekuwa mnaishi ndani ya baraka Zangu? Hapana mmoja kati yenu anayeweza kuelewa mahali ambapo maneno Yangu hutoka. Binadamu—mbali na kuthamini majina ambayo Nimeweka juu yenu, wengi wenu, mnapoitwa “watendaji-huduma,” mnaweka chuki katika nyoyo zenu, na wengi sana, wakiitwa “watu Wangu,” huzalisha upendo katika nyoyo zenu. Usijaribu kunidanganya—macho Yangu huona na kupenya kila mahali! Ni nani kati yenu hupokea kwa hiari, ni nani kati yenu hunipa utiifu kamilifu? Kama saluti kwa ufalme haingelia, je ungeweza kutii mpaka mwisho? Kile ambacho mwanadamu ana uwezo wa kufanya, kufikiria, anaweza kwenda umbali gani—haya yote Nimeyaamua kabla tangu kitambo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp