Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 552

02/11/2020

Kunao mpangilio wa kutimizwa kama itabidi ufanywe kuwa mtimilifu. Kupitia kwa utatuzi wako, ustahimilivu wako, na dhamiri yako, na kupitia ufuatiliaji wako, utaweza kupitia maisha na kutimiza mapenzi ya Mungu. Haya ndiyo kuingia kwako na kile kinachohitajika kwenye njia ya kuwa mtimilifu. Kazi ya kuwa mtimilifu inaweza kufanywa kwa watu wote. Yeyote anamyetafuta Mungu anaweza kufanywa kuwa mtimilifu na anayo fursa na sifa za kufanywa kuwa mtimilifu. Hakuna sheria ngumu na ya haraka hapo. Kufanywa kuwa mtimilifu kimsingi kunategemea kile ambacho mtu hutafuta. Watu wanaopenda ukweli na walio na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli bila shaka wanaweza kufanywa kuwa watimilifu. Na watu wasiopenda ukweli na hawatajwi na Mungu hawamiliki maisha ambayo Mungu anataka. Watu hawa hawawezi kufanywa kuwa timilifu. Kazi ya kufanywa kuwa mtimilifu ni kwa minajili tu ya kuwamiliki watu, na wala si hatua ya kupigana na Shetani; kazi ya ushindi ipo tu kwa minajili ya kupigana na Shetani, kumaanisha kwamba kutumia ushindi kwa binadamu ili kumshinda Shetani. Sehemu hii ya nyuma ndiyo kazi kuu, kazi mpya zaidi ambayo haijawahi kufanywa katika enzi zote. Mtu anaweza kusema kwamba shabaha ya awamu hii ya kazi kimsingi ni kuwashinda watu wote ili kuweza kumshinda Shetani. Kazi ya kufanya watu kuwa watimilifu—hiyo si kazi mpya. Kazi yote katika kipindi hiki ambapo Mungu anafanya katika kwa mwili inayo shabaha lake kuu katika ushindi wa watu. Hii ni sawa na ile Enzi ya Neema. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubishwa ndiyo iliyokuwa kazi kuu. “Kuwapata watu” kulikuwa nyongeza katika kazi ya mwili na kulifanywa tu baada ya kusulubishwa. Wakati Yesu alipokuja na kufanya kazi Yake, shabaha Yake ilikuwa kimsingi kutumia kusulubishwa Kwake katika kushinda uchungu na utumwa wa kifo na Kuzimu, kuweza kushinda ushawishi wa Shetani, kumaanisha kumshinda Shetani. Ilikuwa tu baada ya kusulubishwa kwa Yesu ndipo Petro alipoanza hatua kwa hatua kushika njia ya kuwa utimilifu. Bila shaka alikuwa miongoni mwa wale waliomfuata Yesu wakati Yesu alipokuwa akifanya kazi, lakini hakufanywa kuwa mtimilifu wakati huo. Badala yake, ilikuwa ni baada ya Yesu kumaliza kazi Yake ndipo Petro alipoanza kuelewa taratibu ukweli wa mambo na kisha akafanywa kuwa mtimilifu. Mungu mwenye mwili na huja ulimwenguni tu kukamilisha awamu muhimu na ya kipekee ya kazi kwenye kipindi kifupi cha muda, na wala si kuishi kwa kipindi kirefu miongoni mwa watu hapa ulimwenguni na kuwa na kusudio la kuwafanya kuwa watimilifu. Huwa hafanyi kazi hiyo. Hasubirii mpaka wakati ule ambao binadamu amefanywa kuwa mtimilifu kabisa ili kuhitimisha kazi Yake. Hiyo siyo shabaha na umuhimu wa kupata mwili Kwake. Yeye huja tu ili kufanya kazi ya kipindi kifupi ya kuwaokoa binadamu, na wala si kufanya ile kazi ya kipindi kirefu sana ya kuwafanya binadamu kuwa watimilifu. Kazi ya kuwaokoa binadamu ni wakilishi, inayoweza kuzindua enzi mpya na inaweza kukamilishwa kwenye kipindi kifupi cha muda. Lakini kuwafanya binadamu kuwa watimilifu kunahitaji kuwaleta binadamu hadi kiwango fulani na ni kazi inayoweza kuchukua muda mrefu. Kazi hii lazima ifanywe na Roho wa Mungu, lakini inafanywa kwa msingi wa ukweli unaozungumzwa wakati wa kazi Yake akiwa mwili. Au aidha huwainua mitume kufanya kazi ya uchungaji ya kipindi kirefu, ili kufikia shabaha Yake ya kuwafanya binadamu kuwa watimilifu. Mungu mwenye mwili hafanyi kazi hii. Huongea tu kuhusu njia ya maisha ili watu waweze kuelewa na kuwapatia tu binadamu ukweli, badala ya kuandamana na binadamu bila kusita katika kuendeleza ukweli kwani kufanya hivyo hakumo ndani ya huduma Yake. Kwa hivyo Hatakuwa akiandamana na binadamu mpaka siku ile ambayo binadamu ataelewa kabisa ukweli na kupata kung’amua kabisa ukweli. Kazi Yake akiwa mwili inahitimishwa wakati binadamu anapoingia rasmi kwenye njia iliyo sawa ya ukweli wa maisha, wakati binadamu anapoingia kwenye njia iliyo sawa ya kufanywa kuwa mtimilifu. Hapa, bila shaka ndipo pia ambapo atakuwa Ameshinda Shetani kabisa na kuutawala ulimwengu. Hajali kama binadamu ameingia kimsingi kwenye ukweli wakati huo, wala kujali kuhusu kama maisha ya binadamu ni makubwa au madogo. Vyote hivi si vile ambavyo Yeye akiwa katika mwili anafaa kusimamia; vyote hivi havimo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili. Punde anakapomaliza kazi aliyonuia, huhitimisha kazi Yake katika mwili. Kwa hiyo, kazi ambayo Mungu mwenye mwili anafanya ni kazi ile tu ambayo Roho wa Bwana hawezi kufanya moja kwa moja. Aidha, ni ile kazi ya wokovu ya kipindi kifupi, na wala si kazi ya kipindi kirefu hapa ulimwenguni.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp