Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 220

Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu. Na hivyo kila hatua ya kazi Yake inafanywa na Mungu Mwenyewe. Leo, watu wanatamani utokeaji wa kweli, wanajaribu kuona ishara na maajabu, na kuna uwezekano mkubwa watu wa namna hiyo kutelekezwa, maana kazi ya Mungu inazidi kuwa halisi. Hakuna anayejua kwamba Mungu ameshuka kutoka mbinguni, bado hawajui kwamba Mungu ametuma chini chakula na maji ya kutia nguvu kutoka mbinguni, lakini Mungu kimsingi yupo, na mazingira mazuri ya Ufalme wa Milenia ambao watu wanaufikiria pia ni matamshi ya Mungu Mwenyewe. Huu ni ukweli, ni huu tu ndio unaotawala pamoja na Mungu duniani. Kutawala na Mungu duniani kunarejelea mwili. Kile ambacho si cha mwili hakipo duniani, na hivyo wale wote wanaojikita katika kusonga mbele katika mbingu ya tatu wanafanya hivyo bure. Siku moja, ambapo ulimwengu mzima utarudi kwa Mungu, kitovu cha kazi Yake katika ulimwengu wote kitafuata sauti ya Mungu; kwingineko watu watapiga simu, wengine watapanda ndege, wengine watapanda boti na kupita baharini, na wengine watatumia leza kupokea matamshi ya Mungu. Kila mmoja atakuwa anatamani na mwenye shauku, wote watakuja karibu na Mungu, na kukusanyika kwa Mungu, na wote watamwabudu Mungu—na yote haya yatakuwa matendo ya Mungu. Kumbuka hili! Mungu hawezi kuanza tena kwingineko. Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini inakufa kwa njaa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea. Huo ndio utakuwa muda ambapo matendo ya Mungu yatafichuliwa, na Mungu atatukuzwa; watu wote katika ulimwengu wote watakuja na kumwabudu “mtu” asiyekuwa wa kawaida. Je, hii haitakuwa siku ya utukufu wa Mungu? Siku moja, wachungaji wa zamani watatuma ujumbe wakitafuta maji kutoka katika chemchemi za maji ya uzima. Watakuwa wazee, lakini watakuja kumwabudu mtu huyu ambaye walimdharau. Katika vinywa vyao watakiri na katika mioyo yao wataamini—je, hii si ishara na maajabu? Siku ambapo ufalme wote utafurahia ni siku ya utukufu wa Mungu, na mtu yeyote atakayewajia, na kupokea habari njema za Mungu atabarikiwa na Mungu, na nchi hizi na watu hawa watabarikiwa na kulindwa na Mungu. Mwelekeo wa maisha yajayo utakuwa hivi: Wale ambao watapata matamshi kutoka katika kinywa cha Mungu watakuwa na njia ya kutembea duniani, na wawe wafanya biashara au wanasayansi, au waelimishaji au wataalamu wa viwandani, wale ambao hawana maneno ya Mungu watakuwa na wakati mgumu wa kuchukua hata hatua moja, na watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Hiki ndicho kinamaanishwa na, “Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote.” Ukweli ni huu: Mungu atatumia Njia (ikiwa na maana kwamba maneno Yake yote) kuuamuru ulimwengu wote na kumwongoza na kumshinda mwanadamu. Watu siku zote wanatarajia kuwa na mabadiliko makubwa katika namna ambayo Mungu anafanya kazi. Kuzungumza kwa wazi, ni kupitia maneno ndipo Mungu anawadhibiti watu, na unapaswa kufanya kile Anachokisema haijalishi kama unataka au hutaki; huu ni ukweli halisi, na unapaswa kutiiwa na watu wote, na hivyo haubadiliki, na kujulikana kwa wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp