Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 429

16/10/2020

Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kwa uwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi—mambo si rahisi kama ulivyoweza kufikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake, inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hili tu ndilo linalochukuliwa kama uhalisi, na hili tu ndilo linachukuliwa kama wewe kumiliki uelewa na kimo cha kweli. Lazima uwe na uwezo wa kuhimili uchunguzi kwa muda mrefu, na lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kuidhihirisha sura ambayo inahitajika kwako na Mungu; isiwe mkao tu, lakini ni lazima ibubujike kwa kawaida kutoka ndani mwako. Hapo tu ndipo basi utakapokuwa na uhalisi kikweli, na ndipo tu basi utakapopata maisha. Wacha Nitumie mfano wa jaribio la watendaji huduma ambao kila mtu ana uzoefu nao. Mtu yeyote anaweza kuzungumzia nadharia zenye fahari sana kuhusu watendaji huduma, na kila mtu ana ufahamu unaofaa wa mada hii; wanazungumza juu yake na kila usemi unazidi ule wa awali, kana kwamba kuna mashindano. Hata hivyo, kama mwanadamu hajapitia jaribio kubwa, ni vigumu kusema ana ushahidi mzuri. Kwa ufupi, kuishi kwa kudhihirisha kwa mwanadamu bado kuna upungufu mwingi, na hii inatofautiana na uelewa wake. Kwa hiyo, bado hakijakuwa kimo halisi cha mwanadamu, na bado hayajakuwa maisha ya mwanadamu. Kwa sababu uelewa wa mwanadamu haujaletwa katika uhalisi, kimo chake bado ni kama ngome iliyojengwa kwenye mchanga, ikiyumbayumba na ikiwa karibu kuanguka. Mwanadamu anao uhalisi kidogo mno—ni vigumu kuupata uhalisi wowote katika mwanadamu. Kunao uhalisi kidogo mno unaobubujika kwa asili kutoka kwa mwanadamu na uhalisi wote katika maisha yake umelazimishwa, ndiyo maana nasema kwamba mwanadamu hamiliki uhalisi wowote. Usiweke hisa nyingi sana katika wanadamu wakisema kwamba upendo wao wa Mungu haubadiliki kamwe—hiki tu ndicho kile wao husema kabla ya kukabiliwa na majaribu. Mara tu wanapokabiliwa na majaribu kwa ghafla, mambo ambayo wao hunena kwa mara nyingine tena hayalingani na uhalisi, na kwa mara nyingine yatathibitisha kwamba wanadamu hawana uhalisi. Inaweza kusemwa kwamba wakati wowote unapokumbana na mambo ambayo hayalingani na dhana zako nayo yanakuhitaji kujiweka kando, haya ni majaribu yako. Kabla mapenzi ya Mungu kufichuliwa, kuna mtihani mkali kwa kila mwanadamu, jaribio kubwa kwa kila mtu—je, waweza kuliona wazi jambo hili? Wakati Mungu anapotaka kuwajaribu wanadamu, Yeye daima huwaacha kufanya maamuzi yao kabla ya ukweli wa uhalisi kufichuliwa. Yaani wakati Mungu anamweka mwanadamu katika majaribu, kamwe Yeye hatakwambia ukweli, na hivyo ndivyo wanadamu wanaweza kufichuliwa. Hii ni njia mojawapo ambayo Mungu huifanya kazi yake, ili kuona kama unamwelewa Mungu wa leo, na ili kuona kama unaumiliki uhalisi wowote. Je, kweli wewe huna shaka yoyote kuhusu kazi ya Mungu? Je, utaweza kusimama imara wakati jaribio kuu linakujia? Ni nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Nahakikisha hakutakuwa na matatizo”? Nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Wengine wanaweza kuwa na mashaka, lakini Mimi sitakuwa na shaka kamwe”? Kama vile nyakati Petro alipitia majaribu—alikuwa siku zote akizungumza maneno makubwa kabla ukweli haujafichuliwa. Huu sio udhaifu wa kibinafsi wa kipekee kwa Petro; hii ni shida kubwa zaidi inayomkabili kila mwanadamu sasa. Kama ningetembelea maeneo kadhaa, au kama ningewatembelea ndugu na dada kadhaa, kuuangalia uelewa wenu wa kazi ya Mungu ya leo, hakika mngeweza kweli kuzungumza kuhusu mengi ya uelewa wenu, nayo ingeonekana kwamba ninyi hamna mashaka yoyote. Kama ningewauliza: “Je, kweli waweza kutabainisha kwamba kazi ya leo inatekelezwa na Mungu Mwenyewe? Bila shaka yoyote”? ungejibu bila shaka: “Bila shaka yoyote, ni kazi inayotekelezwa na Roho wa Mungu.” Mara tu unapojibu kwa namna hiyo, kwa hakika usingekuwa hata na chembe cha shaka na unaweza hata kuhisi starehe kubwa—unaweza kuhisi kuwa umepata uhalisi kiasi kidogo. Wale ambao mara nyingi huelewa mambo kwa njia hii ni wale ambao wanamiliki uhalisi kidogo zaidi; kadri mtu anavyodhani kwamba amelipata, ndivyo atakavyokosa uwezo wa kusimama imara katika majaribio. Ole wao walio na kiburi na wenye maringo, na ole wao wasio na maarifa ya wao wenyewe. Watu kama hawa ni hodari katika kuzungumza ilhali huendelea vibaya zaidi katika matendo yao. Wakati kuna dalili ndogo zaidi ya matatizo, watu hawa wataanza kuwa na mashaka na mawazo ya kukata tamaa huingia akilini mwao. Hawana umiliki wa uhalisi wowote; yote waliyo nayo ni nadharia zenye fahari zaidi kuliko zile za dini, bila ya hali halisi ambazo Mungu anadai sasa. Nachukizwa zaidi na wale wanaosema kuhusu nadharia tu nao hawana uhalisi. Wao kufanya kilio kikubwa zaidi wanapoitenda kazi yao, lakini wao husambaratika punde tu wanapokabiliwa na uhalisi. Je, si inaonyesha kwamba watu hawa hawana uhalisi? Haijalishi jinsi upepo na mawimbi yalivyo kali, kama unaweza kubaki umesimama bila hata dalili ya shaka kuingia mawazoni mwako, na unaweza kusimama imara na usiwe kati hali ya kukana hata kama hakuna mtu mwingine aliyebaki, basi hili linachukuliwa kama wewe kuwa na uelewa wa kweli na wewe kuwa na umiliki wa uhalisi. Ukifuata njia yoyote ambayo upepo unavuma, ukiwafuata walio wengi na kujifunza kusema yale ambayo wengine wanasema, haijalishi jinsi gani unavyosema mambo hayo vizuri, sio thibitisho kwamba unao umiliki wa uhalisi. Kwa hiyo, napendekeza kwamba usiwe na haraka ya kupiga kelele kwa maneno matupu. Je, unaijua kazi ambayo Mungu ataitekeleza? Usitende kama Petro mwingine usije ukajiletea aibu na usiweze tena kutembea bila haya—hii haimfaidi mtu yeyote. Wanadamu wengi hawana kimo cha kweli. Mungu ametekeleza kazi kubwa sana lakini hajafanya uhalisi kuwajia watu; kwa kuwa sahihi zaidi, Mungu hajawahi kumwadibu yeyote binafsi. Baadhi ya watu wamefichuliwa na majaribio kama haya, na minyiri yao ya dhambi ikitambaa nje zaidi na zaidi, wakifikiri kwamba ni rahisi kumhadaa Mungu, wanaweza kumchukulia Mungu kwa kutojali, na kufanya chochote wanachotaka. Kwa kuwa hawawezi hata kustahimili majaribu ya aina hii, kadri majaribio yenye changamoto yasivyowezekana, na uhalisi pia hauwezekani. Je, si hii ni kujaribu kumpumbaza Mungu? Kuwa na uhalisi si kitu ambacho kinaweza kubuniwa, na wala si kitu ambacho unaweza kukipata kutokana na maarifa yako kukihusu. Unalingana na kimo chako cha ukweli, na unalingana na kama unao uwezo wa kuhimili majaribu yote. Je, unaelewa sasa?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp