Filamu ya Injili | “Kubisha Hodi Mlangoni” | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

03/06/2018

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alitabiri, "Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki" (Mathayo 25:6).“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20). Kwa miaka elfu mbili iliyopita, waumini katika Bwana wamekuwa makini na wakingoja Bwana abishe mlango, kwa hivyo, Atabishaje mlango wa binadamu Atakaporudi? Katika siku za mwisho, baadhi ya watu wameshuhudia kwamba Bwana Yesu amerudi-Mwenyezi Mungu mwenye mwili-na kwamba Anafanya kazi ya siku za mwisho ya hukumu. Habari hii imetikisa dunia yote ya kidini. Yang Aiguang, mhusika mkuu wa filamu hiyo, amemwamini Bwana kwa miongo na daima amekuwa akihusika na kazi ya kuhubiri, akingoja kukaribisha kurudi kwa Bwana. Siku moja, watu wawili walikuja na kubisha mlango, wakamwambia Yang Aiguang na mume wake kuwa Bwana Yesu amerudi, na kushiriki maneno ya Mwenyezi Mungu na wao. Waliguswa sana na maneno ya Mwenyezi Mungu, lakini kwa sababu Yang Aiguang ameona uasi, udanganyifu na vizuizi vya wachungaji na wazee wa kanisa, anawafukuza mashahidi wa Kanisa La Mwenyezi Mungu kutoka nyumbani kwake. Baada ya hilo, mashahidi wanabisha mara nyingi na kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu kwa Yang Aiguang na kutoa ushuhuda wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Wakati huu, mchungaji anamvuruga na kumzuia Yang Aihuang, muda baada ya muda, na anaendelea kuyumbayumba. Hata hivyo, kwa kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu, Yang Aiguang anakuja kuelewa ukweli na kupata ufahamu kuhusu uvumi na udanganyifu unaoenezwa na wachungaji na wazee wa kanisa. Hatimaye anaelewa jinsi Bwana anavyobisha kwenye milango ya watu wakati wa kurudi Kwake katika siku za mwisho, na jinsi tunavyopaswa kumkaribisha Yeye. Wakati ukungu unapotanzuka Yang Aiguang hatimaye anasikia sauti ya Mungu na anakiri kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni kurudi kwa Bwana Yesu!

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp