Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 142

Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika maisha ya mwanadamu, kuonyesha yale ambayo mwanadamu anapaswa kuingia kwayo, kumwonesha mwanadamu matendo ya Mungu, na kumwonesha mwanadamu hekima, uweza na uajabu wa Mungu. Kupitia njia nyingi ambazo Mungu Anazungumza, mwanadamu anatazama ukuu wa Mungu, aidha, unyenyekevu na usiri wa Mungu. Mwanadamu anatazama kwamba Mungu ni mkuu, lakini ni mnyenyekevu na msiri, na Anaweza kuwa mdogo kuliko vitu vyote. Baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa Roho, baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu, na baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu. Katika hili inaweza kuonekana kwamba namna ya kazi ya Mungu inatofautiana kwa kiasi kikubwa na ni kwa njia ya maneno ndipo Anamruhusu mwanadamu kuiona. Kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho ni ya kawaida na halisi, na hivyo kundi la watu wa siku za mwisho wanakumbwa na majaribu makubwa kuliko yote. Kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu, watu wote wameingia katika majaribu hayo; kwamba mwanadamu ameingia katika majaribu ya Mungu ni kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu. Wakati wa enzi ya Yesu, hakukuwa na dhana au majaribu. Kwa sababu kazi kubwa iliyofanywa na Yesu ilikuwa ni kulingana na dhana za mwanadamu, watu walimfuata, na hawakuwa na dhana juu Yake. Majaribu ya leo ni makubwa sana ambayo yamewahi kukabiliwa na mwanadamu, na inaposemwa kwamba watu hawa wametoka katika dhiki kuu, hii ndiyo dhiki inayoongelewa. Leo, Mungu Ananena ili kusababisha imani, upendo, ustahimilivu na utii kwa watu hawa. Maneno yaliyozungumzwa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutokana na hulka ya asili ya mwanadamu, kulingana na tabia ya mwanadamu, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia kwacho leo. Mbinu Yake ya kuzungumza ni halisi na ya kawaida: Hazungumzi juu ya kesho, wala Haangalii nyuma, jana; Anazungumza kile tu ambacho kinapaswa kuingiwa kwacho, kuwekwa katika vitendo, na kueleweka leo. Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na ana uwezo wa kutoa mapepo, na kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine; mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Unapaswa kuelewa vizuri mambo haya. Kwa nini kazi ya Mungu leo ni tofauti na kazi ya Yesu? Kwa nini Mungu leo Haonyeshi ishara na maajabu, Hatoi mapepo, na Haponyi wagonjwa? Ikiwa kazi ya Yesu ingekuwa sawa na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Sheria, je, Angekuwa Amemwakilisha Mungu wa Enzi ya Neema? Je, Yesu Angekuwa Amemaliza kazi ya msalaba? Ikiwa, kama katika Enzi ya Sheria, Yesu Angeingia hekaluni na kuitunza Sabato, basi Asingeteswa na mtu yeyote na Angekumbatiwa na wote. Kama ingekuwa hivyo, je, Angesulubiwa? Je, Angekuwa Amemaliza kazi ya ukombozi? Je, ingekuwa na maana gani ikiwa Mungu katika mwili wa siku za mwisho Angeonyesha ishara na maajabu kama Yesu? Ikiwa tu Mungu Atafanya sehemu nyingine ya kazi Yake wakati wa siku za mwisho, kazi inayowakilisha sehemu ya mpango wa usimamizi Wake, ndipo mwanadamu anaweza kupata maarifa ya kina ya Mungu, na baada ya hapo tu ndipo mpango wa usimamizi wa Mungu unaweza kukamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp