Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 204

Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kupona kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba “siku za mwisho” ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria. Kazi ya siku za mwisho haifanyiki katika taifa la Israeli, lakini kati ya mataifa; ni ushindi mbele ya kiti Changu cha enzi cha watu kutoka mataifa yote na makabila yote nje ya Israeli, ili utukufu Wangu katika ulimwengu wote uweze kujaza dunia nzima. Iko hivyo ili Niweze kupata utukufu mkuu, ili viumbe vyote duniani viweze kupitisha utukufu Wangu kwa mataifa yote, milele katika vizazi vyote, na viumbe vyote mbinguni na duniani viweze kuuona utukufu wote ambao Nimepata duniani. Kazi inayofanyika katika siku za mwisho ni kazi ya ushindi. Sio uongozi wa maisha ya watu wote duniani, lakini hitimisho la maisha ya milenia ya mwanadamu yasiyoangamia, ya mateso katika dunia. Matokeo yake ni kwamba kazi ya siku za mwisho haiwezi kuwa kama miaka elfu kadhaa ya kazi katika Israeli, wala kama muongo mmoja wa kazi katika Yuda ambayo kisha iliendelea kwa miaka elfu kadhaa mpaka kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu katika mwili. Watu wa siku za mwisho hukutana tu na kuonekana tena kwa Mkombozi katika mwili, na kupokea kazi binafsi na maneno ya Mungu. Haitakuwa miaka elfu mbili kabla ya siku za mwisho hazijafika ukingoni; zi fupi, kama wakati ambao Yesu alifanya kazi ya Enzi ya Neema katika Yuda. Hii ni kwa sababu siku za mwisho ni hitimisho la nyakati nzima. Ni ukamilisho na tamatisho la mpango wa miaka elfu sita wa usimamizi wa Mungu, na kuhitimisha safari ya maisha ya mateso ya mwanadamu. Hazichukui binadamu wote hadi katika enzi mpya au kuruhusu maisha ya mwanadamu kuendelea. Hiyo haitakuwa na umuhimu wowote kwa ajili ya mpango Wangu wa usimamizi au kuwepo kwa mwanadamu. Kama mwanadamu angeendelea kwa namna hii, basi hivi karibuni wao wangeangamizwa kabisa na ibilisi, na zile nafsi za wale walio Wangu hatimaye zingetwaliwa na mikono yake. Kazi Yangu inadumu kwa miaka elfu sita tu, na Mimi niliahidi kwamba udhibiti wa yule mwovu juu ya wanadamu wote utakuwa pia si zaidi ya miaka elfu sita. Na kwa hivyo, wakati umeisha. Nami wala Sitaendelea wala kuchelewa tena: Katika siku za mwisho Nitamshinda Shetani, nami Nitaumiliki tena utukufu Wangu wote, na kurudisha nafsi zile zote zilizo Zangu duniani ili nyoyo hizi za dhiki ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso, na hivyo Nitakuwa nimetimiza kazi Yangu nzima duniani. Kutoka siku hii na kuendelea, kamwe Sitawahi kuwa mwili duniani, na kamwe Roho Wangu wa kudhibiti yote Hatafanya kazi tena duniani. Lakini Nitafanya jambo moja duniani: Nitamfanya tena mwanadamu, mwanadamu aliye mtakatifu, na aliye mji Wangu mwaminifu duniani. Lakini ujue kwamba Sitaiangamiza dunia nzima, wala kuangamiza ubinadamu mzima. Nitahifadhi theluthi moja iliyobaki—theluthi moja inayonipenda na imeshindwa kabisa na Mimi, na Nitaifanya theluthi hii iwe yenye kuzaa matunda na kuongezeka duniani kama Israeli walivyofanya chini ya sheria, kuwalisha kwa kondoo wengi mno na mifugo, na utajiri wote wa dunia. Mwanadamu huyu atabaki na Mimi milele, hata hivyo si mwanadamu mchafu wa kusikitisha wa leo, lakini mwanadamu ambaye ni mkusanyiko wa wale wote ambao wamepatwa na Mimi. Mwanadamu wa aina hii hataharibiwa, kusumbuliwa, au kuzungukwa na Shetani, na atakuwa mwanadamu wa pekee anayepatikana duniani baada ya ushindi Wangu juu ya Shetani. Ni wanadamu ambao leo wameshindwa na Mimi na wamepata ahadi Yangu. Na hivyo, wanadamu ambao wameshindwa katika siku za mwisho pia ndio watakaosamehewa na kupata baraka Zangu za milele. Huu utakuwa ushahidi wa pekee wa ushindi Wangu dhidi ya Shetani, na nyara za pekee za vita Vyangu na Shetani. Hizi nyara za vita zimeokolewa nami kutoka utawala wa Shetani, na ni thibitisho la pekee na matunda ya mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita. Wao huja kutoka kila taifa na dhehebu, na kila mahali na nchi ulimwenguni mwote. Ni wa jamii tofauti, na wana lugha mbalimbali, mila na rangi ya ngozi, na huenea katika kila taifa na dhehebu la duniani, na hata kila pembe ya dunia. Hatimaye, watakuja pamoja na kuunda ubinadamu kamili, mkusanyiko wa binadamu usiofikiwa na majeshi ya Shetani. Wale miongoni mwa wanadamu ambao hawajaokolewa na kushindwa na Mimi watazama kwa kimya mpaka chini ya bahari, na watachomwa kwa moto wa kuteketeza milele. Nitamwangamiza mwanadamu huyu mzee aliye mchafu sana, kama tu vile Nilivyoangamiza wazaliwa wa kwanza na ng’ombe wa Misri, na kuacha tu Waisraeli, waliokula nyama ya mwanakondoo, kunywa damu ya mwanakondoo, na kutia alama vizingitini mwa milango yao kwa damu ya mwanakondoo. Si watu ambao wameshindwa na Mimi na ni wa jamii Yangu ndio wale pia wanaokula nyama Yangu, Mwanakondoo na kunywa damu Yangu, Mwanakondoo, na wamekombolewa na Mimi na kuniabudu Mimi? Si watu wa namna hiyo kila mara huandamwa na utukufu Wangu? Si hao wasio na nyama Yangu, Mwanakondoo tayari wamezama kimya kwa kina cha bahari? Leo wao wananipinga, na leo maneno Yangu ni kama tu yale yaliyosemwa na Yehova kwa wana na wajukuu wa Israeli. Lakini ugumu katika kina cha nyoyo zenu unahifadhi tu ghadhabu Yangu, na kuleta mateso zaidi juu ya miili yenu, hukumu zaidi juu ya dhambi zenu, na ghadhabu zaidi juu ya udhalimu wenu. Ni nani atakayeweza kusamehewa katika siku Yangu ya ghadhabu, mnaponitendea kwa namna hii leo? Udhalimu wa nani utaweza kuepuka macho Yangu ya kuadibu? Dhambi za nani zinaweza kuepuka mikono Yangu, Mwenyezi? Uasi wa nani unaweza kuepuka hukumu Yangu, Mwenyezi? Mimi, Yehova, Nasema hivyo kwenu, kizazi cha jamii ya Mataifa, na maneno Ninayosema nanyi yanashinda matamko yoyote yale ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, ilhali bado nyinyi ni wagumu kuliko watu wote wa Misri. Je, si mnahifadhi ghadhabu Yangu Ninapofanya kazi kwa utulivu? Jinsi gani mnaweza kuepuka salama bila ya madhara kutoka siku Yangu, Mwenyezi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp