Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 189

27/06/2020

Katika mpango wa Mungu wa miaka elfu kadhaa, kazi inayofanywa ndani ya mwili ni katika sehemu mbili: Kwanza ni kazi ya kusulubiwa, ambayo kwayo anatukuzwa; nyingine ni kazi ya ushindi na ukamilifu katika nyakati za mwisho, ambayo kwayo pia Atapokea utukufu. Huu ni usimamizi wa Mungu. Hivyo basi, usichukulie kazi ya Mungu au agizo Lake kwako kuwa rahisi sana. Ninyi ndinyi warithi wa uzito wa milele wa utukufu wa Mungu, hili liliteuliwa na Mungu. Katika sehemu hizo mbili za utukufu wa Mungu, moja inafichuliwa ndani yako; ukamilifu wa sehemu moja ya utukufu Wake umepewa ili uwe urithi wako. Huku ndiko kutukuzwa kutoka kwa Mungu na mpango wake uliopangwa kitambo. Kutokana na ukuu wa kazi aliyoifanya Mungu katika nchi ambako joka kuu jekundu linaishi, kazi kama hii, ikipelekwa katika sehemu nyingine, ingezaa tunda zuri kitambo na ingekubaliwa na mwanadamu kwa urahisi. Na kazi kama hii ingekuwa rahisi sana kukubaliwa na viongozi wa dini wa Magharibi wanaomwamini Mungu, kwani kazi ya Yesu ni kama kielelezo. Ndio maana Hawezi kutekeleza hatua hii ya kazi ya utukufu mahali pengine; yaani, kwa kuwa kuna uungaji mkono kwa watu wote na utambulisho wa mataifa yote, hamna mahali ambapo utukufu wa Mungu unaweza “kupumzikia.” Na huu ndio umuhimu wa kipekee wa hatua hii ya kazi katika nchi hii. Kati yenu, hamna mtu mmoja anayepokea ulinzi wa sheria; badala yake, unaadhibiwa na sheria, na ugumu mkubwa zaidi ni kuwa hapana mtu anayekuelewa, awe ni jamaa yako, wazazi wako, marafiki wako, ama watendakazi wenzako. Hakuna anayekuelewa. Mungu “Anapokukataa,” hapana uwezekano wako kuendelea kuishi duniani. Hata hivyo, watu hawawezi kumwacha Mungu; huu ndio umuhimu wa ushindi wa Mungu kwa watu, na huu ni utukufu wa Mungu. Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa ajili ya Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la Mungu la mwisho, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili. Anapokukarimia mengi, anakutaka wewe badala yake na kukufanyia matakwa yanayokufaa. Kwa hiyo, kazi yote ya Mungu haipo bila sababu, na kutokana na hili inaonekana ni kwa nini Mungu kila mara hufanya kazi ya hali ya juu na yenye mahitaji makali. Ndiyo maana unafaa kujawa na imani katika Mungu. Kwa ufupi, kazi yote ya Mungu hufanywa kwa ajili yako, ili kwamba uweze kupokea urithi Wake. Hii sio kwa ajili ya utukufu wa Mungu bali ni kwa ajili ya wokovu wako na kufanya kundi hili la watu walioteswa na nchi najisi kuwa wakamilifu. Sharti uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo Nawahimiza wale wote wasiojua, wasio na hisia na ufahamu: Usimjaribu Mungu wala kumpinga tena. Mungu Ameshavumilia mateso yote ambayo mwanadamu hajaweza kupitia, na hapo awali Ameteseka na kudhihakiwa kwa niaba ya mwanadamu. Je, nini kingine ambacho huwezi kukiachilia? Je, ni nini muhimu zaidi kuliko mapenzi ya Mungu? Ni nini zaidi kuliko upendo wa Mungu? Ni kazi ambayo ina ugumu mara mbili zaidi kwa Mungu kufanya katika nchi najisi. Ikiwa mtu atatenda dhambi kimakusudi na akifahamu, kazi ya Mungu itaendelezwa kwa muda mrefu zaidi. Katika tukio lolote, hili silo pendeleo la yeyote wala si la maana kwa yeyote. Mungu Hafungwi na wakati; kazi Yake na utukufu Wake huchukua mstari wa mbele. Kwa hiyo, hata ikichukua muda mrefu, Hataacha kutoa dhabihu yoyote ikiwa ni kazi Yake. Hii ndiyo silika ya Mungu: Hatapumzika hadi pale kazi Yake itakapokamilika. Ni pale tu ambapo wakati unapowadia na anapokea sehemu ya pili ya utukufu wake ndipo kazi Yake itakapokwisha. Mungu Asipokamilisha sehemu ya pili ya utukufu wake ulimwenguni, Siku Yake haitawadia, mkono wake hauwezi kuwaachilia wateule wake, utukufu wake hautashuka juu ya Israeli na mpango wake kamwe hauwezi kukamilishwa. Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayvodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake. Huu ndio undani wa hadithi ya hatua hii ya kazi ya Mungu. Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine. Uzuri wake hauwezi kutambuliwa na akili za mwanadamu wala hekima Yake kupatikana vile. Mungu Haumbi kila kitu wala kuharibu kila kitu. Bali, Anabadilisha viumbe vyote na kutakasa vyote vilivyonajisiwa na Shetani. Kwa hiyo, Mungu Ataanzisha kazi kuu, na huu ndio umuhimu wa kazi ya Mungu. Baada ya kusoma maandishi haya, je, unaamini kuwa kazi ya Mungu ni rahisi vile?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp