Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 127

Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana. Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu. Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kushindana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu. Mungu anapofanya kazi katika mwili, kwa hakika Anakuwa Anapambana na Shetani katika mwili. Anapofanya kazi katika mwili, Anafanya kazi Yake katika ufalme wa kiroho, na Anafanya kazi Yake yote katika ufalme wa kiroho ili iwe halisi duniani. Yule anayeshindaliwa ni mwanadamu, ambaye si mtiifu Kwake, yule anayeshindwa ni mfano halisi wa Shetani (bila shaka, huyu pia ni mwanadamu), ambaye ana uadui Naye, na ambaye ataokolewa hatimaye ni mwanadamu. Kwa namna hii, ni muhimu zaidi Kwake kuwa mwanadamu ambaye ana ganda la nje la kiumbe, ili kwamba Awe na uwezo wa kupambana na Shetani katika uhalisia, kumshinda mwanadamu, ambaye si mtii Kwake na ambaye ana mwonekano wa nje ambao unafanana na Yeye, na kumwokoa mwanadamu, ambaye ana umbo la nje kama Lake na aliyeumizwa na Shetani. Adui Wake ni mwanadamu, mlengwa wa mateka ni mwanadamu, na mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, aliyeumbwa na Yeye. Hivyo ni lazima awe mwanadamu, na kwa njia hii, kazi Yake inakuwa rahisi zaidi. Ana uwezo wa kumshinda Shetani na kumshinda mwanadamu, aidha, anaweza kumwokoa mwanadamu. Ingawa mwili huu ni wa kawaida na halisi, Yeye si mwili wa kawaida. Yeye si mwili ambao ni mwanadamu tu, bali mwili ambao una uanadamu na uungu. Hii ndio tofauti Yake na mwanadamu, na ni alama ya utambulisho wa Mungu. Ni mwili tu kama huu ndio unaweza kufanya kazi Anayokusudia kufanya, na kutimiza huduma ya Mungu mwenye mwili, na kukamilisha kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Isingekuwa hivyo, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingekuwa tupu na yenye makosa. Ingawa Mungu anaweza kupambana na roho wa Shetani na kuibuka mshindi, silika ya zamani ya mwanadamu aliyepotoka haiwezi kuondolewa, na wale ambao sio watiifu Kwake na wanaompinga hawawezi kuwa wahusika katika utawala Wake, ni sawa na kusema, hawezi kamwe kumshinda mwanadamu, na hawezi kamwe kuwapata wanadamu wote. Kama kazi Yake duniani haiwezi kufanywa, basi usimamizi Wake hautafika mwisho, na wanadamu wote hawataweza kuingia katika pumziko. Ikiwa Mungu hawezi kuingia katika pumziko pamoja na viumbe Wake wote, basi hakutakuwa na matokeo ya usimamizi huo, na utukufu wa Mungu kwa sababu hiyo utatoweka. Ingawa mwili Wake hauna mamlaka, kazi Anayofanya itapokea matokeo yake. Huu ndio mwelekeo usioepukika wa kazi Yake. Haijalishi kama mwili Wake una mamlaka au la, maadamu Ana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, basi ni Mungu Mwenyewe. Haijalishi mwili wake ni wa kawaida kiasi gani, Anaweza kufanya kazi Anayopaswa kufanya, maana mwili huu ni Mungu na wala si mwanadamu tu. Sababu ambayo inafanya mwili huu unaweza kufanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya ni kwa sababu kiini Chake cha ndani si kama cha mwanadamu yeyote yule, na sababu ya kuweza kumwokoa mwanadamu ni kwa sababu utambulisho Wake ni tofauti na wa mwanadamu yeyote yule. Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyeharibika, ambaye anaishi pamoja Naye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. Na matokeo yake, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa mwanadamu kunamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani kujikabidhi kikamilifu katika utawala Wake. Ni kwa sababu Mungu amefanyika mwili ili kwamba Aweze kumshinda Shetani na aweze kumwokoa mwanadamu. Hamwangamizi Shetani moja kwa moja, bali Anakuwa mwili ili kuweza kufanya kazi ya kumshinda mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Kwa njia hii, Anakuwa na uwezo zaidi wa kutoa ushuhuda Wake Mwenyewe miongoni mwa viumbe, na Anakuwa na uwezo zaidi wa kumwokoa mwanadamu aliyepotea. Ushindi wa Mungu mwenye mwili dhidi ya Shetani unabeba ushuhuda mkubwa, na una ushawishi mkubwa, kuliko Roho wa Mungu kumwangamiza Shetani moja kwa moja. Mungu mwenye mwili Ana uwezo zaidi wa kumsaidia mwanadamu kumjua Muumba, na Ana uwezo zaidi wa kubeba ushuhuda Wake mwenyewe miongoni mwa viumbe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp