Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 302

Chanzo cha ufunuo wa upotovu wa tabia ya mwanadamu ni dhamiri yake iliyofifia, asili yake mbovu na akili yake isiyo timamu; kama dhamiri ya mwanadamu na hisia vinaweza kurudi kawaida, basi atafaa kwa matumizi mbele ya Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa dhamiri ya mwanadamu daima imekuwa isiyosikia, akili ya mwanadamu haijawahi kuwa timamu, na inazidi kuwa hafifu ndio mwanadamu amezidisha uasi wake kwa Mungu, hata akampiga Yesu misumari juu ya msalaba na kumkataa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kuingia katika nyumba yake, na analaani mwili wa Mungu, na anaona mwili wa Mungu kuwa ya kuchukiza na wa hali ya chini. Kama mwanadamu angekuwa na ubinadamu kidogo, hangekuwa mkatili kiasi hicho katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na akili hata kidogo tu, hangekuwa hivyo katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na dhamiri hata kidogo, hangekuwa mwenye “shukrani” kwa Mungu mwenye mwili kwa njia hii. Mwanadamu anaishi katika enzi ya Mungu kuwa katika mwili, lakini yeye hawezi kumshukuru Mungu kwa kumpatia nafasi nzuri kiasi hicho, na badala yake analaani kuja kwa Mungu, au kupuuza kabisa ukweli wa Mungu aliyepata mwili, na inaonekana anapinga hali hii na anachoshwa nayo. Haijalishi jinsi mwanadamu anachukua kuja kwa Mungu, Mungu, kwa ufupi, daima ameendeleza kazi yake bila kujali—hata kama mwanadamu hajawahi kumkaribisha, na bila kujua yeye hufanya maombi kwa Mungu. Tabia ya mwanadamu imekuwa mbaya zaidi, akili yake imekuwa hafifu zaidi, na dhamiri yake imekanyagwa kabisa na yule muovu na kwa muda mrefu imekoma kuwa dhamiri ya awali ya mwanadamu. Mwanadamu hajakosa tu shukrani kwa Mungu mwenye mwili kwa kukabidhi maisha na neema nyingi juu ya wanadamu, bali pia anachukia Mungu kwa kumpatia ukweli; ni kwa sababu mwanadamu hana haja ya kujua ukweli hata kidogo ndio maana anamchukia Mungu. Haitoshi kwamba mwanadamu hawezi kuutoa uhai wake kwa ajili ya Mungu mwenye mwili tu, lakini pia anajaribu kutoa neema kutoka kwa Mungu, na anafanya madai kwa Mungu yaliyo mara kadhaa kubwa kuliko kile mwanadamu ametoa kwa Mungu. Watu wa dhamiri na hisia kama hizo huchukua yote haya kama haki yao, na bado wanaamini kuwa wao wamefanya mengi sana kwa ajili ya Mungu, na kwamba Mungu amewapa kidogo sana. Kuna watu ambao wamenipa bakuli la maji na kisha kunyosha mikono yao na kudai sawia na bakuli mbili za maziwa, au kunipa chumba kwa usiku mmoja lakini walijaribu kunilipisha mara nyingi zaidi katika ada ya makazi. Ukiwa na ubinadamu kama huo, na dhamiri ya aina hii, ni jinsi gani bado mnatarajia kupata uzima? Nyinyi ni fukara wa kudharauliwa mlioje! Ni kwa sababu ya ubinadamu huu na dhamiri ya mwanadamu ndio maana Mungu mwenye mwili anatembea katika ardhi yote, asipate mahali pa makazi. Wale ambao kwa kweli wanayo dhamiri na ubinadamu wanapaswa kumuabudu na kwa moyo wote kumhudumia Mungu mwenye mwili si kwa sababu ya kiasi cha kazi aliyofanya, lakini hata kama Yeye hangefanya kazi yoyote kamwe. Hili ndilo linafaa kufanywa na wale walio na akili timamu, na ndio wajibu wa mwanadamu. Watu wengi hata huzungumza juu ya masharti katika huduma yao kwa Mungu: Hawajali kama yeye ni Mungu au mwanadamu, na wao huzungumza juu ya masharti yao tu, na kufuata mafanikio ya tamaa zao wenyewe. Wakati mnanipikia, mnadai malipo ya mpishi, wakati mnakimbia kwa ajili Yangu, mnadai pesa za mkimbiaji, mkinifanyia kazi mnadai ada ya kazi, mkifua nguo Zangu, mnadai ada ya kufua, wakati mnatoa kwa ajili ya kanisa mnadai malipo ya kurudisha nguvu, mkizungumza, mnadai malipo ya msemaji, mkipeana vitabu mnadai ada ya usambazaji, na wakati mnaandika mnadai malipo ya kuandika. Wale Nimehusiana nao hata hudai malipo kutoka Kwangu, na wale waliotumwa nyumbani hudai fidia kwa uharibifu wa majina yao; wale ambao hawajaoa au kuolewa hudai mahari, au fidia kwa ujana wao waliopoteza, wale wanaochinja kuku wanadai ada ya uchinjaji, wale wanaokaanga chakula wanadai ada ya kukaanga, na wale ambao hupika supu wanadai malipo pia…. Huu ndio ubinadamu wenu mkuu na wenye majivuno, na haya ndiyo matendo yanayoamrishwa na dhamiri yenu yenye joto. Hisia zenu ziko wapi? Ubinadamu wenu uko wapi? Wacha Niwaambie! Mkiendelea hivi Nitakoma kufanya kazi miongoni mwenu. Sitafanya kazi miongoni mwa wanyama waliovalia mavazi ya binadamu, Sitateseka hivyo kwa ajili ya kundi la watu ambao nyuso zao nzuri zimeficha nyoyo za uhasama, Sitavumilia kwa ajili ya kundi la wanyama ambao hawana uwezekano hata kidogo wa kuokolewa. Siku Nitakayowapa mgongo ndiyo siku mtakayokufa, ndiyo siku ambayo giza litakuja juu yenu, na ni siku mtakayoachwa na mwanga! Hebu Niwaambie! Sitakuwa mwema kamwe kwa kundi kama lenu, kundi ambalo liko chini ya hata wanyama! Kuna mipaka katika maneno na matendo Yangu, na vile ubinadamu wenu na dhamiri zilivyo, Sitafanya kazi zaidi, kwani mmekosa dhamiri, umenisababishia maumivu mengi sana, na tabia yenu ya kudharauliwa inanichukiza Mimi sana! Watu wanaokosa utu na dhamira kamwe hawatakuwa na nafasi ya wokovu; Mimi kamwe Sitawaokoa watu kama hao wasio na utu wala shukurani. Siku Yangu itakapofika, Nitanyesha mvua ya moto Wangu mkali milele juu ya wana waasi walioiamsha hasira na ghadhabu yangu kali hapo awali, Nitalazimisha adhabu yangu milele juu ya wanyama wale ambao wakati mmoja waliupa lugha chafu Kwangu na wakaniacha, Nitawachoma wakati wote kwa moto wa hasira Yangu wana wa uasi waliokula na kuishi pamoja Nami lakini hawakuniamini, na wakanitukana na kunisaliti. Nitawatia wote walionikasirisha kwa adhabu Yangu, Nitanyesha ghadhabu Yangu kwa ukamilifu juu ya wanyama hao waliotamani wakati mmoja kusimama bega-kwa-bega na Mimi ilhali hawakuniabudu wala kunitii, fimbo Ninayotumia kumgonga mwanadamu itaanguka juu ya wanyama hao waliofurahia utunzaji Wangu na siri Nilizonena, na waliojaribu kuchukua starehe ya mali ya dunia kutoka Kwangu. Sitamsamehe mtu yeyote anayejaribu kuchukua nafasi Yangu; Sitamsamehe yeyote anayejaribu kupokonya chakula na nguo kutoka Kwangu. Kwa sasa, mnabaki huru kutokana na madhara na kuendelea kujiharibia kwa kuzidi katika mahitaji mnayotaka kutoka Kwangu. Siku ya ghadhabu inapofika hamtafanya madai yoyote zaidi Kwangu; wakati huo, Nitawaruhusu “kujifurahia” hadi mtakaporidhika, Nitalazimisha nyuso zenu kuingia mchangani, na kamwe hamtaweza kuinuka tena! Wakati mmoja au mwingine, Ninaenda “kulipiza” madeni hayo kwenu na Natumaini mnasubiri kwa uvumilivu kuwasili kwa siku hii.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp