Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 111

25/10/2020

Mungu mwenye mwili Anajidhihirisha mwenyewe kwa watu kadhaa wanaomfuata Anapofanya kazi Yeye binafsi, na sio kwa viumbe wote. Alijifanya mwili ili Akamilishe hatua ya kazi Yake, na sio ili amwonyeshe mwanadamu mfano Wake. Hata hivyo, kazi Yake lazima ifanywe na Yeye binafsi, kwa hivyo inalazimu Afanye kazi hiyo katika mwili. Kazi hii inapokamilika, Ataondoka duniani; Hawezi kusalia duniani kwa muda mrefu kwa hofu ya kuzuia kazi inayokuja. Anachokionyesha kwa halaiki ni tabia Yake ya haki na matendo Yake yote, na sio umbo la wakati Amejifanya mwili mara mbili, kwa maana mfano wa Mungu unaweza tu kuonyeshwa kupitia kwa tabia Yake, na si kubadilishwa na mfano wa mwili Wake wa nyama. Mfano wa mwili Wake wa nyama huonyeshwa kwa watu wachache tu, kwa wale wanaomfuata Anapofanya kazi katika mwili. Hiyo ndio maana kazi inayofanywa wakati huu inafanywa kwa siri. Ni kama tu vile Yesu alivyojionyeshwa kwa Wayahudi pekee yao Alipofanya kazi Yake, na hakujionyesha hadharani kwa mataifa mengine. Hivyo, pindi Alipomaliza kazi Yake, Aliondoka miongoni mwa wanadamu na hakukawia; kwa wakati uliofuata Hakujionyesha kwa nafsi Yake kwa mwanadamu, bali kazi iliendeshwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu. Mara tu kazi ya Mungu katika mwili inapokamilika, Anaondoka katika dunia ya mwanadamu, na kamwe Hafanyi tena kazi sawa na ile Aliyofanya Akiwa katika mwili. Kazi inayofuata hufanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Wakati huu, mwanadamu hawezi kuona mfano Wa Mungu katika mwili; Yeye Hajionyeshi wazi kwa mwanadamu hata kidogo, na daima Anabaki mafichoni. Muda wa kazi ya Mungu mwenye mwili ni mchache, ambayo lazima ifanywe katika Enzi bayana, muda, taifa na kati ya watu bayana. Kazi kama hiyo inawakilisha tu kazi ya wakati wa Mungu katika mwili, na inalenga enzi fulani, ikiwakilisha kazi ya Roho wa Mungu katika enzi moja hasa, na sio ujumla wa kazi Yake. Kwa hivyo, umbo la Mungu mwenye mwili halitaonyeshwa kwa kila mwanadamu. Kinachoonyeshwa kwa halaiki ni haki ya Mungu na tabia Yake kwa ukamilifu, na wala sio mfano Wake Alipokuwa mwili mara mbili. Sio sura inayoonyeshwa kwa mwanadamu, wala mifano yote miwili ikijumlishwa. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba mwili wa Mungu uondoke duniani baada ya kukamilisha kazi Anayohitajika kufanya, kwa kuwa Anakuja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya, na sio kuwaonyesha wanadamu mfano wa umbo Lake. Ingawa umuhimu wa kuingia katika mwili umeshatimizwa na Mungu mara mbili Akijifanya mwili na nyama, bado hatajionyesha wazi kwa taifa ambalo halijawahi kumwona mbeleni. Yesu hatajionyesha Mwenyewe kamwe mara nyingine kwa Wayahudi kama Jua la haki, wala Hataupanda Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa watu wote: yote ambayo Wayahudi huona ni taswira Yake wakati wa kipindi Chake katika Uyahudi. Hili ni kwa sababu kazi ya Yesu aliyepata mwili iliisha kitambo sana miaka elfu mbili iliyopita; Hatarudi Uyahudi katika sura ya Myahudi, sembuse kujionyesha katika sura ya Myahudi kwa nchi yoyote ya Mataifa, kwani sura ya Yesu aliyepata mwili ni sura ya Myahudi tu, na siyo sura ya Mwana wa Adamu ambayo Yohana alikuwa ameiona. Ingawa Yesu aliwaahidi wafuasi Wake kwamba Angerudi tena, Hatajionyesha tu Mwenyewe katika sura ya Myahudi kwa wote walio katika nchi za Mataifa. Mnapaswa kujua kwamba kazi ya Mungu katika mwili inafaa kufungua enzi mpya. Kazi hii ni ya muda wa miaka michache tu, na Hawezi kukamilisha kazi yote ya Roho wa Mungu. Hii ni sawia na vile umbo la Yesu kama Myahudi linaweza tu kuwakilisha mfano wa Mungu alivyofanya kazi katika Yudea, na Angefanya tu kazi ya msalabani. Wakati ambao Yesu Alikuwa katika mwili, Hangefanya kazi ya kutamatisha enzi au kumwangamiza mwanadamu. Kwa hivyo, baada ya kusulubiwa na kukamilisha kazi Yake, Alipaa juu na daima Akajificha kutoka kwa mwanadamu. Kutoka wakati huo kuendelea, wale waumini wa mataifa waliweza tu kuiona picha Yake ambayo walibandika kwenye kuta zao, na sio udhihirisho wa Bwana Yesu. Picha hii imechorwa na mwanadamu tu, na si mfano ambao Mungu Mwenyewe Alimwonyesha mwanadamu. Mungu Hatajionyesha kwa halaiki wazi wazi katika mfano ambao Yeye Alikuwa nao mara mbili Akiwa katika mwili. Kazi Anayofanya miongoni mwa wanadamu ni kuwaruhusu kuelewa tabia Yake. Yote haya yanaonyeshwa kwa mwanadamu kwa njia ya kazi za enzi tofauti; yanakamilishwa kupitia tabia ambazo Ameziweka wazi na kazi ambayo Amefanya, na bali si kupitia kwa udhihirisho wa Yesu. Hiyo ni kusema, umbo la Mungu halionyeshwi kwa mwanadamu kupitia katika mfano wa Mungu mwenye mwili, lakini ni kwa kupitia katika kazi iliyotekelezwa na Mungu mwenye mwili wa sura na umbo; na kupitia kazi Yake, mfano Wake unaonekana na tabia Yake inajulikana. Huu ndio umuhimu wa kazi Angependa kufanya katika mwili.

Wakati kazi ya Alipokuwa mwili mara mbili inakamilika, Anaanza kuonyesha tabia Yake ya haki katika mataifa, Akiruhusu halaiki ione mfano wa umbo Lake. Anapenda kudhihirisha tabia Yake, na kupitia katika hili Aweke wazi tamati za aina tofauti ya wanadamu, hapo kuifikisha mwisho kabisa enzi nzee. Kazi Yake katika mwili haitendeki katika sehemu pana (kama vile Yesu Alivyofanya kazi katika sehemu ya Yuda peke Yake, na leo hii Ninafanya kazi miongoni mwenu pekee) kwa sababu kazi Yake katika mwili ina mipaka na kingo. Anafanya tu kazi ya muda mchache katika mfano wa kawaida na mwili wa kawaida, badala ya kufanya kazi ya milele kupitia kwa Mungu mwenye mwili, ama kufanya kazi ya kuwaonekania watu wote wa mataifa. Kazi hii katika mwili lazima izuiliwe katika mawanda (kama vile kufanya kazi katika Yuda ama kati Yenu), kisha kupanua kazi iliyofanyika katika mipaka hii. Bila shaka, kazi ya upanuzi huu huendeshwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja na haiwezi kuwa kazi ya mwili Wake wa nyama. Kwa maana kazi katika mwili iko na mipaka na haiwezi kuenea katika pembe zote za ulimwengu. Hauwezi kuyatekeleza haya. Kupitia kwa kazi katika mwili, Roho Wake hutekeleza kazi inayofuatia. Kwa hivyo, kazi inayofanywa katika mwili ni ya matayarisho inayotekelezwa ndani ya mipaka; Roho Wake kisha Anaendeleza kazi hii, na kuipanua.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp