Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili)

Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo sio kazi ya hukumu. Je, upotovu wa wanadamu wote si ni sawa? Je, kiini cha wanadamu wote hakifanani? Kinachohukumiwa ni dutu ya mwanadamu iliyopotoka, dutu ya mwanadamu iliyopotoshwa na Shetani, na dhambi zote za mwanadamu. Mungu hahukumu makosa madogo madogo ya mwanadamu na yasiyokuwa na umuhimu. Kazi ya hukumu ni ya uwakilishi, na haifanywi mahususi kwa ajili ya mtu fulani. Badala yake, ni kazi ambayo kwayo kundi la watu wanahukumiwa ili kuiwakilisha hukumu ya wanadamu wote. Kwa Yeye mwenyewe kufanya kazi Yake katika kundi la watu, Mungu mwenye mwili anatumia kazi Yake ili kuwakilisha kazi ya wanadamu wote, ambayo inaenea taratibu. Kazi ya hukumu pia ipo hivyo. Mungu hahukumu aina fulani ya mtu au kundi fulani la watu, bali anawahukumu wasio na haki wote miongoni mwa wanadamu—upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, kwa mfano, au mwanadamu kutomcha Yeye, au kusababisha usumbufu katika kazi ya Mungu, na kadhalika. Kile kinachohukumiwa ni hulka ya mwanadamu ya kumpinga Mungu, na kazi hii ni kazi ya mashindano ya siku za mwisho. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili lililoshuhudiwa na mwanadamu ni kazi ya hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi wakati wa siku za mwisho, ambacho kilibuniwa na mwanadamu katika kipindi cha siku za nyuma. Kazi ambayo sasa inafanywa na Mungu mwenye mwili ni hukumu yenyewe mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu mwenye mwili wa leo ni Yule Mungu anayewahukumu wanadamu wote wakati wa siku za mwisho. Mwili huu na kazi, neno, na tabia Yake yote, vyote ni ujumla Wake. Ingawa mawanda ya kazi Yake ni finyu, na hayahusishi moja kwa moja ulimwengu wote, kiini cha kazi ya hukumu ni hukumu ya moja kwa moja kwa wanadamu wote; si kazi inayofanywa kwa ajili ya Uchina tu, au kwa idadi ndogo ya watu. Wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, ingawa mawanda ya kazi hii hayahusishi ulimwengu mzima, inawakilisha kazi ya ulimwengu mzima na, baada ya kuhitimisha kazi ndani ya mawanda ya mwili Wake, ataipanua kazi hii mara moja katika ulimwengu mzima, kwa namna ile ile, injili ya Yesu ilienea ulimwengu mzima baada ya kufufuka Kwake na kupaa mbinguni. Bila kujali endapo ni kazi ya Roho au ni kazi ya mwili, ni kazi ambayo inafanywa ndani ya mawanda finyu, lakini ambayo inauwakilisha ulimwengu mzima. Wakati wa siku za mwisho, Mungu Anaonekana kufanya kazi Yake kwa kutumia utambulisho Wake wa Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili ni Mungu anayemhukumu mwanadamu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Bila kujali endapo ni Roho au mwili, Yule ambaye anafanya kazi ya hukumu ni Mungu anayemhukumu mwanadamu katika siku za mwisho. Hii inafasiliwa kwa kuangalia kazi Yake, na haifasiliwi kulingana na umbo lake la nje au sababu nyinginezo. Ingawa mwanadamu ana dhana za maneno haya, hakuna anayeweza kukana ukweli wa hukumu ya Mungu mwenye mwili na kuwashinda wanadamu wote. Bila kujali ni jinsi gani unatathminiwa, ukweli ni, baada ya yote, ukweli tu. Hukuna anayeweza kusema “Kazi imefanywa na Mungu lakini mwili si Mungu.” Huu ni upuuzi, maana kazi hii haiwezi kufanywa na mtu yeyote isipokuwa Mungu mwenye mwili. Kwa kuwa kazi hii imekwishakamilika, kufuatia kazi hii, kazi ya hukumu ya Mungu kwa mwanadamu haitatokea kwa mara ya pili; Mungu wa pili katika mwili amekwishaikamilisha kazi yote ya usimamizi, na hakutakuwa na hatua ya nne ya kazi ya Mungu. Kwa sababu yule anayehukumiwa ni mwanadamu, mwanadamu ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa, na sio roho ya Shetani ambayo inahukumiwa moja kwa moja, kazi ya hukumu haifanywi katika ulimwengu wa roho, bali miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayefaa zaidi na mwenye vigezo, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Aidha, kazi kama hiyo itakuwa vigumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, sembuse mwanadamu hataweza kuona kwa uwazi kabisa tabia ya Mungu isiyokosewa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye aliyehitimu, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Ikiwa kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi usingekuwa ushindi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa ameinuliwa sana kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na anaushinda mwili. Ikiwa Roho alifanya kazi hii moja kwa moja, asingeweza kuhukumu kutotii kote kwa mwanadamu, na asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kwa mitazamo ya mwanadamu juu ya Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala kuweza kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga Yeye, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, bali hatua kwa hatua tu atamwelewa taratibu kupitia neno la mdomo Wake, ametwaliwa Naye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho. Kazi iliyofanywa na Mungu mwenye mwili ni kazi kubwa sana, na ni kazi ya kina sana, na sehemu muhimu ya hatua tatu za kazi ya Mungu ni hatua mbili za kazi ya kufanyika mwili. Upotovu wa kina wa mwanadamu ni kikwazo kikubwa sana katika kazi ya Mungu mwenye mwili. Kwa umahususi, kazi inayofanywa kwa watu wa siku za mwisho ni ngumu sana, na mazingira ni ya uhasama, na tabia ya kila aina ya mwanadamu ni duni sana. Lakini mwishoni mwa kazi hii, bado itapokea matokeo mazuri, bila dosari yoyote; haya ni matokeo ya kazi ya mwili, na matokeo haya yanashawishi sana kuliko kazi ile ya Roho. Hatua tatu za kazi ya Mungu zitahitimishwa na Mungu mwenye mwili, na lazima ikamilishwe na Mungu mwenye mwili. Kazi muhimu sana imefanywa na Mungu mwenye mwili, na wokovu wa mwanadamu ni lazima ufanywe na Mungu mwenye mwili. Ingawa watu wote wanahisi kwamba Mungu mwenye mwili hahusiani na mwanadamu, kwa kweli ni kuwa mwili huu unahusiana na majaliwa na uwepo wa wanadamu wote.

Kila hatua ya kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote, na inawalenga wanadamu wote. Ingawa ni kazi Yake katika mwili, bado inaelekezwa kwa wanadamu wote; ni Mungu wa wanadamu wote, na ni Mungu wa viumbe vyote vilivyoumbwa na ambavyo havijaumbwa. Ingawa kazi Yake katika mwili ipo ndani ya mawanda yenye mipaka, na kusudi la kazi hii pia lina mipaka, kila wakati Anapokuwa mwili kufanya kazi Yake, Yeye huchagua chombo cha kazi Yake ambacho ni wakilishi na ambacho kina uakilishi mkubwa; Hachagui kikundi cha watu wa kawaida na wasiosifika kwa ajili ya kuwafanyiza kazi, lakini badala yake huwachagua kama wawakilishi wa kazi Yake kundi la watu wenye uwezo kuwa wahusika wa kazi Yake katika mwili. Kundi hili la watu linachaguliwa kwa sababu ya mawanda ya kazi Yake katika mwili ni finyu, na wamejiandaa mahususi kwa ajili ya Kufanyika Kwake kuwa mwili, na amechaguliwa mahususi kwa ajili ya kazi Yake katika mwili. Uchaguzi wa Mungu wa walengwa wa kazi Yake si ambao hauna msingi, bali kulingana na kanuni: Mlengwa wa kazi anapaswa kuwa na manufaa katika kazi ya Mungu mwenye mwili, na anapaswa kuwa na uwezo wa kuwawakilisha wanadamu wote. Kwa mfano, Wayahudi wangeweza kuwawakilisha wanadamu wote katika kupokea wokovu binafsi wa Yesu, na Wachina wanaweza kuwawakilisha wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu mwenye mwili. Kuna msingi kwa Wayahudi kuwa wawakilishi wa wanadamu wote, na kuna msingi kwa uwakilishi wa Wachina wa wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu. Hakuna kinachodhihirisha maana ya ukombozi kuliko kazi ya wokovu iliyofanywa kwa Wayahudi, na hakuna kinachodhihirisha uhakika na mafanikio ya kazi ya ushindi kuliko kazi ya ushindi iliyofanywa miongoni mwa Wachina. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili inaonekana kuelekezwa kwa kikundi kidogo tu cha watu, lakini kwa hakika, kazi Yake miongoni mwa kikundi hiki kidogo ni kazi ya ulimwengu wote, na neno lake limeelekezwa kwa wanadamu wote. Baada ya kazi Yake katika mwili kufikia kikomo, wale wanaomfuata wataanza kueneza kazi ambayo Amefanya mwiongoni mwao. Kitu kizuri kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ya kusihi, na mapenzi Yake kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwa na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambayo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya matendo zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisia na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili badala ya Roho wa Mungu. Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili wake, wale wanaofuata wanakuwa hawatafuti tena vitu hivyo visivyo yakini, na wanaacha kukisia mapenzi ya Munguasiye yakini. Mungu anapoeneza kazi Yake katika mwili, wale wanaomfuata wataieneza kazi ambayo Ameifanya katika mwili kwa dini na madhehebu yote, na watazungumza maneno Yake yote katika masikio ya wanadamu wote. Yote yale yanayosikizwa na wale wanaoipokea injili Yake yatakuwa ni ukweli wa kazi Yake, yatakuwa mambo ambayo mwanadamu ameyashuhudia na kuyaona, na utakuwa ukweli na sio uvumi. Ukweli huu ni ushahidi ambao anauenezea kazi na pia ni zana ambazo Anazitumia katika kueneza kazi. Bila uwepo wa ukweli, Injili yake isingeweza kuenea katika nchi zote na maeneo yote; bila ukweli bali kwa fikra tu za mwanadamu, Asingeweza kufanya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Mwanadamu hawezi kumgusa Roho, na wala hawezi kumwona, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Hata hivyo picha anazozijenga mwanadamu kumhusu Mungu, sio halisi na haziwezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; silika ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigizwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekana na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye Yeye binafsi anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwangalia Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili. Baada ya Mungu kufanya kazi yake hadi hatua hii, kazi yake tayari imeshafanikiwa kuwa na matokeo mazuri, na imekuwa ni mafanikio kamili. Kazi binafsi ya Mungu mwenye mwili tayari imekwishakamilisha asilimia tisini ya kazi yote ya usimamizi wa Mungu. Mwili umetoa mwanzo mzuri katika kazi Yake yote, na muhtasari kwa ajili ya kazi Yake yote, na ametangaza kazi Yake yote na Ameifanya ya mwisho kupitia ujazaji tena wa kazi hii yote. Kuanzia sasa, hakutakuwepo na Mungu mwingine katika mwili kwa ajili ya kufanya hatua ya nne ya kazi ya Mungu, na hakutakuwa na kazi ya miujiza zaidi ya Mungu mwenye mwili wa tatu.

Kila hatua ya kazi ya Mungu mwenye mwili inawakilisha kazi yake ya enzi yote, na haiwakilishi kipindi fulani kama kazi ya mwanadamu. Na hivyo mwisho wa kazi ya kufanyika Kwake mwili mara ya mwisho haimaanishi kwamba kazi Yake imefikia mwisho kabisa, kwa maana kazi Yake katika mwili inawakilisha enzi yote, na haiwakilishi kipindi tu ambacho Anafanya kazi Yake katika mwili tu. Ni kwamba tu Anakamilisha kazi Yake ya enzi yote wakati ambapo yupo katika mwili, ambayo baadaye inaenea sehemu zote. Baada ya Mungu mwenye mwili kutimiza huduma yake, atawakabidhi wale wote wanaoifuata kazi Yake ya baadaye. Kwa njia hii kazi Yake ya enzi yote itaendelezwa bila kusitishwa. Kazi ya enzi yote ya kufanyika kuwa mwili itachukuliwa tu kuwa imekamilika baada ya kuenea ulimwenguni kote. Kazi ya Mungu mwenye mwili huanzisha enzi mpya, na wale wanaoiendeleza kazi Yake ni watu wanaotumiwa Naye. Kazi inayofanywa na mwanadamu yote ipo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili, na haina uwezo wa kwenda zaidi ya mawanda haya. Ikiwa Mungu mwenye mwili haji kufanya kazi Yake, mwanadamu hana uwezo wa kuhitimisha enzi ya zamani, na hana uwezo wa kuikaribisha enzi mpya. Kazi inayofanywa na mwanadamu ipo tu ndani ya wajibu wake ambao unawezekana kibinadamu, na haiwakilishi kazi ya Mungu. Ni Mungu mwenye mwili pekee ndiye anayeweza kuja na kukamilisha kazi ambayo Anapaswa kuifanya, na mbali na Yeye, hakuna anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Bila shaka, kile Ninachozungumzia ni kuhusiana na kazi ya kufanyika mwili. Huyu Mungu mwenye mwili, kwanza anachukua hatua ya kazi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu, baada ya hapo Anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu. Lengo la kazi hii ni kumshinda mwanadamu. Kwa upande mmoja, Mungu mwenye mwili hapatani na mitazamo ya mwanadamu, aidha, anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu, na kwa hivyo mwanadamu anakuza mawazo zaidi ya kukosoa kuhusu Yeye. Anafanya kazi ya ushindi miongoni mwa wanadamu ambaye ana dhana nyingi sana kumhusu Yeye. Bila kujali jinsi wanavyomchukulia, Atakapokuwa Amekamilisha huduma Yake, wanadamu wote watakuwa ni wenyeji wa utawala wake. Ukweli wa kazi hii hauonekani tu miongoni mwa Wachina, bali wao wanawakilisha namna ambavyo wanadamu wote watakavyoshindwa. Matokeo yanayoonekana kwa watu hawa ni kitangulizi cha matokeo yatakayoonekana kwa wanadamu wote, na matokeo ya kazi Anayofanya wakati ujao yatazidi sana matokeo kwa watu hawa. Kazi ya Mungu mwenye mwili haihusishi mshindo mkubwa wa tarumbeta, wala haijakita katika mafumbo. Ni halisi na ya kweli, na ni kazi ambayo moja kujumlisha na moja ni sawa sawa na mbili. Hajafichwa kwa mtu yeyote, na wala haimdanganyi mtu yeyote. Kile ambacho watu wanaona ni vitu halisi, na kile ambacho mwanadamu anapata ni ukweli halisi na maarifa. Kazi itakapokamilika, mwanadamu atakuwa na maarifa mapya juu Yake, na wale ambao kweli wanamtafuta Mungu hawatakuwa na dhana yoyote juu Yake. Haya sio tu matokeo ya kazi Yake kwa Wachina, lakini pia inawakilisha matokeo ya kazi yake katika kuwashinda wanadamu wote, kwa maana hakuna kitu ambacho ni cha manufaa zaidi katika kazi ya kuwashinda watu kuliko mwili huu, na kazi ya mwili huu, na kila kitu cha mwili huu. Vina manufaa katika kazi Yake leo, na vina manufaa katika kazi Yake hapo baadaye. Mwili huu utawashinda wanadamu wote na utawapata wanadamu wote. Hakuna kazi bora zaidi ambayo kwayo wanadamu wote watamwona Mungu, na kumtii Mungu, na kumfahamu Mungu. Kazi inayofanywa na mwanadamu inawakilisha tu mawanda finyu, na Mungu anapofanya kazi Yake hazungumzi na watu fulani, bali Anazungumza na wanadamu wote, na wale wote wanaoikubali kazi Yake. Mwisho Anaoutangaza ni mwisho wa wanadamu wote, na sio mwisho wa mtu fulani tu. Hamtendei mtu yeyote kwa umahususi, wala hamkandamizi mtu yeyote, na Anafanya kazi kwa ajili ya, na Anazungumza na wanadamu wote. Na kwa hiyo Mungu huyu katika mwili amekwisha waainisha wanadamu wote kulingana na aina yao, tayari amekwisha wauhukumu wanadamu wote, na amwekwishapangilia hatima inayofaa kwa wanadamu wote. Ingawa Mungu anafanya kazi Yake China tu, kwa hakika ameshaamua kazi ya ulimwengu mzima. Hawezi kusubiri hadi kazi Yake itakapoenea miongoni mwa wanadamu wote kabla ya kutoa matamshi Yake na kuweka mipango hatua kwa hatua. Hivyo, sio kwamba utakuwa umechelewa sana? Sasa Anaweza kabisa kukamilisha kazi ya wakati ujao kabla ya wakati huo. Kwa sababu Yule anayefanya kazi ni Mungu mwenye mwili, Anafanya kazi isiyokuwa na mipaka ndani ya mawanda yenye mipaka, na baadaye Atamfanya mwanadamu atekeleze jukumu ambalo mwanadamu anapaswa kulitekeleza; hii ni kanuni ya kazi Yake. Anaweza kuishi tu na mwanadamu kwa muda, na hawezi kushirikiana na mwanadamu hadi kazi ya enzi zote itakapokamilika. Ni kwa sababu Yeye ni Mungu kwamba Yeye hutabiri kazi Yake ya Wakati ujao kabla ya wakati. Baada ya hapo, Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina kwa maneno Yake, na mwanadamu ataingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua kulingana na neno Lake. Hakuna atakayekwepa, na wote wanapaswa kutenda kulingana na hili. Hivyo, katika wakati ujao, enzi itaongozwa na maneno Yake, na sio kuongozwa na Roho.

Kazi ya Mungu mwenye mwili ni lazima ifanywe katika mwili. Ikiwa ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu isingeweza kutoa matokeo yoyote. Hata kama ingefanywa na Roho, kazi hii isingekuwa na maana kubwa, na hatimaye isingekuwa na ushawishi. Viumbe vyote vinatamani kujua iwapo kazi ya Muumbaji ina maana, na inawakilisha kitu gani, na ni kwa ajili ya nini, na iwapo kazi ya Mungu ina mamlaka kamili na hekima, na endapo ina thamani na maana ya kina. Kazi Anayofanya ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote, kwa ajili ya kumshinda Shetani, na kwa kuwa na ushuhuda wa Mungu miongoni mwa vitu vyote. Kwa namna hiyo, kazi Anayoifanya ni lazima iwe ya umuhimu mkubwa. Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana. Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu. Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kushindana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu. Mungu anapofanya kazi katika mwili, kwa hakika Anakuwa Anapambana na Shetani katika mwili. Anapofanya kazi katika mwili, Anafanya kazi Yake katika ufalme wa kiroho, na Anafanya kazi Yake yote katika ufalme wa kiroho ili iwe halisi duniani. Yule anayeshindaliwa ni mwanadamu, ambaye si mtiifu Kwake, yule anayeshindwa ni mfano halisi wa Shetani (bila shaka, huyu pia ni mwanadamu), ambaye ana uadui Naye, na ambaye ataokolewa hatimaye ni mwanadamu. Kwa namna hii, ni muhimu zaidi Kwake kuwa mwanadamu ambaye ana ganda la nje la kiumbe, ili kwamba Awe na uwezo wa kupambana na Shetani katika uhalisia, kumshinda mwanadamu, ambaye si mtii Kwake na ambaye ana mwonekano wa nje ambao unafanana na Yeye, na kumwokoa mwanadamu, ambaye ana umbo la nje kama Lake na aliyeumizwa na Shetani. Adui Wake ni mwanadamu, mlengwa wa mateka ni mwanadamu, na mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, aliyeumbwa na Yeye. Hivyo ni lazima awe mwanadamu, na kwa njia hii, kazi Yake inakuwa rahisi zaidi. Ana uwezo wa kumshinda Shetani na kumshinda mwanadamu, aidha, anaweza kumwokoa mwanadamu. Ingawa mwili huu ni wa kawaida na halisi, Yeye si mwili wa kawaida. Yeye si mwili ambao ni mwanadamu tu, bali mwili ambao una uanadamu na uungu. Hii ndio tofauti Yake na mwanadamu, na ni alama ya utambulisho wa Mungu. Ni mwili tu kama huu ndio unaweza kufanya kazi Anayokusudia kufanya, na kutimiza huduma ya Mungu mwenye mwili, na kukamilisha kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Isingekuwa hivyo, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingekuwa tupu na yenye makosa. Ingawa Mungu anaweza kupambana na roho wa Shetani na kuibuka mshindi, silika ya zamani ya mwanadamu aliyepotoka haiwezi kuondolewa, na wale ambao sio watiifu Kwake na wanaompinga hawawezi kuwa wahusika katika utawala Wake, ni sawa na kusema, hawezi kamwe kumshinda mwanadamu, na hawezi kamwe kuwapata wanadamu wote. Kama kazi Yake duniani haiwezi kufanywa, basi usimamizi Wake hautafika mwisho, na wanadamu wote hawataweza kuingia katika pumziko. Ikiwa Mungu hawezi kuingia katika pumziko pamoja na viumbe Wake wote, basi hakutakuwa na matokeo ya usimamizi huo, na utukufu wa Mungu kwa sababu hiyo utatoweka. Ingawa mwili Wake hauna mamlaka, kazi Anayofanya itapokea matokeo yake. Huu ndio mwelekeo usioepukika wa kazi Yake. Haijalishi kama mwili Wake una mamlaka au la, maadamu Ana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, basi ni Mungu Mwenyewe. Haijalishi mwili wake ni wa kawaida kiasi gani, Anaweza kufanya kazi Anayopaswa kufanya, maana mwili huu ni Mungu na wala si mwanadamu tu. Sababu ambayo inafanya mwili huu unaweza kufanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya ni kwa sababu kiini Chake cha ndani si kama cha mwanadamu yeyote yule, na sababu ya kuweza kumwokoa mwanadamu ni kwa sababu utambulisho Wake ni tofauti na wa mwanadamu yeyote yule. Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyeharibika, ambaye anaishi pamoja Naye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. Na matokeo yake, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa mwanadamu kunamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani kujikabidhi kikamilifu katika utawala Wake. Ni kwa sababu Mungu amefanyika mwili ili kwamba Aweze kumshinda Shetani na aweze kumwokoa mwanadamu. Hamwangamizi Shetani moja kwa moja, bali Anakuwa mwili ili kuweza kufanya kazi ya kumshinda mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Kwa njia hii, Anakuwa na uwezo zaidi wa kutoa ushuhuda Wake Mwenyewe miongoni mwa viumbe, na Anakuwa na uwezo zaidi wa kumwokoa mwanadamu aliyepotea. Ushindi wa Mungu mwenye mwili dhidi ya Shetani unabeba ushuhuda mkubwa, na una ushawishi mkubwa, kuliko Roho wa Mungu kumwangamiza Shetani moja kwa moja. Mungu mwenye mwili Ana uwezo zaidi wa kumsaidia mwanadamu kumjua Muumba, na Ana uwezo zaidi wa kubeba ushuhuda Wake mwenyewe miongoni mwa viumbe.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp