Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 113

Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa. Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. Nani anayejua iwapo Mungu atabadili na kughairi, na kuiacha ghadhabu yake iliyo kali, ili tusiangamie? Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo alikuwa amesema angeliwafanyia; na hakulifanya.

Mungu Aona Kutubu kwa Dhati katika Vina vya Mioyo ya Waninawi

Baada ya kusikiliza tangazo la Mungu, mfalme wa Ninawi na raia Wake walitekeleza misururu ya vitendo. Je, ni nini asili ya tabia na matendo yao? Kwa maneno mengine, ni nini kiini cha uzima wa mwenendo wao? Kwa nini walifanya kile walichofanya? Katika macho ya Mungu walikuwa wametubu kwa dhati, si tu kwa sababu walikuwa wamemsihi Mungu kwa dhati na kuungama dhambi zao mbele Yake, lakini pia kwa sababu walikuwa wameacha mwenendo wao wenye maovu. Walichukua hatua namna hii kwa sababu baada ya kusikia matamshi ya Mungu, walitishika pakubwa na kusadiki kwamba angefanya vile ambavyo alikuwa amesema. Kwa kufunga, kuvalia nguo ya gunia na kukalia jivu, walipenda kuonyesha namna walivyokuwa radhi kubadilisha njia zao na kujizuia na maovu, kumwomba Yehova Mungu kuzuia hasira Yake, kusihi Yehova Mungu kutupilia mbali uamuzi Wake, pamoja na msiba mkuu ambao ulikuwa karibu kuwasibu. Kupitia uchunguzi wa tabia yao yote, tunaona ya kwamba tayari walielewa kwamba vitendo vyao vya awali vilimchukiza Yehova Mungu na kwamba walielewa sababu iliyomfanya kutaka kuwaangamiza hivi karibuni. Kwa sababu hizi, wote walipenda kutubu kabisa, kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, pindi tu walipotambua tangazo la Yehova Mungu, kila mmoja wao alihisi woga katika mioyo yao; hawakuendelea tena na mwenendo wao wa maovu wala kuendelea kutenda vitendo ambavyo Yehova Mungu alichukia. Vilevile, walimsihi Yehova Mungu kusamehe dhambi zao za kale na kutowatendea kulingana na vitendo vyao vya kale. Walikuwa radhi kutowahi kujihusisha tena katika maovu na kutenda kulingana na maagizo ya Yehova Mungu, kama tu wasingewahi kumkasirisha Yehova Mungu. Toba yao ilikuwa ya dhati na ya kweli. Ilitoka kwenye kina cha mioyo yao na haikuwa ya kujidanganya, wala haikuwa ya muda.

Baada ya watu wa Ninawi, kutoka kwa mfalme mwenye mamlaka hadi kwa raia wake, kujua kwamba Yehova Mungu alikuwa amewakasirikia, kila mojawapo ya vitendo vyao, tabia yao nzima, pamoja na kila mojawapo ya uamuzi na machaguo yao vilikuwa wazi na dhahiri mbele ya Mungu. Moyo wa Mungu ulibadilika kulingana na tabia yao. Akili Zake Mungu zilikuwa zinafikiria nini wakati huo? Biblia inaweza kukujibia swali hili. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo alikuwa amesema angeliwafanyia; na hakulifanya” (Yona 3:10). Ingawaje Mungu alibadilisha fikira Yake, hakukuwa na chochote kigumu kuhusu mtazamo wa fikira Yake. Aliweza kubadilika kutoka katika kuonyesha hasira Yake hadi kutuliza hasira Yake, na kisha kuamua kutouleta msiba mkuu katika mji wa Ninawi. Sababu ya uamuzi wa Mungu wa—kuwaokoa Waninawi dhidi ya msiba wao mkuu—ilikuwa ya haraka mno, ni kwa sababu Mungu aliangalia moyo wa kila mmoja wa wale Waninawi. Aliona kwamba katika kina cha mioyo yao waliweza: kuungama na kutubu kwa dhati dhambi zao, imani yao ya dhati kwake Yeye, mtazamo wao wa kina kuhusu vile vitendo vyao vya maovu vilikuwa vimeipa tabia Yake hasira kali, na woga uliotokana na adhabu ya Yehova Mungu iliyokuwa inakaribia. Wakati uo huo, Yehova Mungu aliweza kusikia maombi kutoka kwenye kina cha mioyo yao wakimsihi kusitisha hasira Yake dhidi yao ili waweze kuepuka msiba huu mkuu. Wakati Mungu alipoangalia hoja hizi zote, kwa utaratibu hasira yake ilitoweka. Licha ya vile hasira yake ilivyokuwa kuu hapo awali, alipoona kutubu kwao kwa dhati ndani ya kina cha mioyo ya watu hawa, moyo Wake uliguswa na hili, na kwa hivyo Hakuweza kuvumilia kuwaletea msiba mkuu, na Alisitisha hasira yake kwao. Badala yake Aliendelea kuwaonyesha huruma Yake na uvumilivu kwao na akaendelea kuwaongoza na kuwakimu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp