Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 151

14/07/2020

Mungu hutumia usimamizi Wake wa watu kumshinda Shetani. Kwa kuwapotosha watu, Shetani huleta hutamatisha hatima ya watu na kuinyanyasa kazi ya Mungu. Kwa upande mwingine, kazi ya Mungu ndiyo wokovu wa binadamu. Ni hatua gani ya kazi yenyewe ya Mungu ambayo hainuii kuwaokoa binadamu? Ni hatua gani hainuii kutakasa watu, ili kuwafanya kuwa wenye haki na kuwafanya kuishi kwa njia ambayo huunda taswira inayoweza kupendwa? Shetani, hata hivyo, hafanyi hivi. Yeye huwapotosha binadamu; siku zote anatekeleza kazi zake za kuwapotosha binadamu kote ulimwenguni. Bila shaka, Mungu pia hufanya kazi Yake. Hamtilii maanani Shetani. Haijalishi ni mamlaka kiasi kipi Shetani anayo, mamlaka yake bado yalitoka kwa Mungu; Mungu kwa hakika hakumpa mamlaka Yake yote tu, na hivyo basi haijalishi ni nini afanyacho Shetani, hawezi kuzidi Mungu na siku zote huwa kwenye udhibiti wa Mungu. Mungu hakufichua vitendo Vyake vyovyote akiwa mbinguni. Alimpa Shetani kiwango kidogo tu cha mamlaka ili kumruhusu kutekeleza udhibiti wake dhidi ya malaika. Hivyo basi, haijalishi ni nini hufanya, hawezi kuzidi mamlaka ya Mungu kwa sababu mamlaka ambayo Mungu alimpa awali ni finyu. Huku Mungu akifanya kazi, Shetani hunyanyasa. Katika siku za mwisho, atamaliza unyanyasaji wake; vilevile, kazi ya Mungu itakamilika, na aina ya mtu ambaye Mungu angependa kumkamilisha atakuwa amekamilika. Mungu huwaelekeza watu kwa njia nzuri; maisha Yake ni maji yenye uzima, yasiyopimika na yasiyo na mipaka. Shetani amepotosha binadamu hadi kiwango fulani; hatimaye, yale maji hai ya uzima yatamkamilisha binadamu, na haitawezekana kwa Shetani kuingilia kati na kutekeleza kazi yake. Hivyo basi, Mungu ataweza kuwapata kabisa watu wake. Shetani angali anakataa kukubali haya sasa; siku zote hupambana na Mungu, lakini Mungu hamtilii maanani. Amesema, Nitakuwa mshindi dhidi ya nguvu zote za giza za Shetani na dhidi ya ushawishi wote wa giza. Hii ndiyo kazi ambayo lazima ifanywe kwa mwili, na ndiyo pia maana ya kupata mwili kwa Yesu Kristo. Ni kukamilisha awamu ya kazi ya kumshinda Shetani katika siku za mwisho, kuondoa vitu vyote vinavyomilikiwa na Shetani. Ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani ni mtindo usioepukika! Shetani kwa hakika alishindwa kitambo sana. Wakati injili ilipoanza kuenezwa kote nchini mwa joka kubwa jekundu, yaani, wakati Mungu mwenye mwili alipoanza kufanya kazi na kazi hii ikafanywa kuendelea, Shetani aliweza kushindwa kabisa, kwani kupata mwili wa Kristo kulimaanisha kumshinda Shetani. Shetani aliona kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na alikuwa ameanza kutekeleza kazi Yake, na akaona kwamba hakuna nguvu ambazo zingeweza kukomesha kazi hii. Hivyo basi, alipigwa na bumbuazi alipoona kazi hii na hakuthubutu kufanya kazi yoyote nyingine zaidi. Kwanza Shetani alifikiria kwamba pia alimiliki hekima nyingi, na akaingilia kati na kunyanyasa kazi ya Mungu; hata hivyo, hakutarajia kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili, na kwamba katika kazi Yake, Mungu alikuwa ametumia uasi Wake kuhudumu kama ufunuo na hukumu kwa binadamu; na hivyo basi kushinda binadamu na kumshinda Shetani. Mungu ni mwerevu kumshinda, na kazi Yake inamzidi Shetani. Hivyo basi, Niliwahi kutaja awali kwamba: Kazi Ninayoifanya inatekelezwa kutokana na ujanja wa Shetani. Mwishowe Nitafichua uweza Wangu na hali ya kutoweza kwa Shetani. Wakati Mungu anapofanya kazi Yake, Shetani anamfuata unyo kwa unyo kutoka nyuma mpaka mwishowe anaangamizwa—hatajua hata kilichomgonga! Ataweza kutambua tu ukweli baada ya kuvunjwa na kupondwapondwa; na wakati huo atakuwa tayari amechomwa kwenye ziwa la moto. Hatakuwa ameshawishika kabisa wakati huo? Kwani hatakuwa na njama zozote zingine za kutumia!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp