Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hukumu Katika Siku za Mwisho | Dondoo 90

10/09/2020

Mungu alipata mwili katika mahali palipokuwa nyuma kimaendeleo na pachafu zaidi, na ni kwa njia hii tu ndiyo Mungu anaweza kuonyesha wazi tabia Yake yote iliyo takatifu na yenye haki. Na tabia Yake yenye haki inaonyeshwa kupitia nini? Inaonyeshwa Anapozihukumu dhambi za mwanadamu, Anapomhukumu Shetani, Anapochukia dhambi sana, na Anapowadharau maadui wanaompinga na kuasi dhidi Yake. Maneno Ninayonena leo ni kwa ajili ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, kuhukumu udhalimu wa mwanadamu, kulaani uasi wa mwanadamu. Upotovu na udanganyifu wa mwanadamu, maneno na vitendo vya mwanadamu—yote ambayo hayapatani na mapenzi ya Mungu lazima yatapitia hukumu, na uasi wa mwanadamu kushutumiwa kama dhambi. Maneno Yake yanahusu kanuni za hukumu; Yeye hutumia hukumu ya udhalimu wa mwanadamu, laana ya uasi wa mwanadamu, na mfichuo wa asili mbaya za mwanadamu ili kudhihirisha tabia Yake mwenyewe yenye haki. Utakatifu ni kielelezo cha tabia Yake yenye haki, na kwa kweli utakatifu wa Mungu ni tabia Yake yenye haki. Tabia zenu potovu ni muktadha wa maneno ya leo—Ninazitumia kunena na kuhukumu, na kutekeleza kazi ya ushindi. Hii pekee ndiyo kazi halisi, na hii pekee inadhihirisha kabisa utakatifu wa Mungu. Ikiwa hakuna dalili ya tabia potovu ndani yako, basi Mungu hatakuhukumu, wala hatakuonyesha tabia Yake yenye haki. Kwa kuwa unayo tabia potovu, Mungu hatakusamehe, na ni kwa njia hii ndiyo utakatifu Wake unaonyeshwa. Mungu angaliona kuwa uchafu na uasi wa mwanadamu vilikuwa vikubwa sana lakini Asinene au kukuhukumu, wala kukuadibu kwa ajili ya udhalimu wako, basi hii ingethibitisha kwamba Yeye si Mungu, kwa maana Asingeichukia dhambi; Angelikuwa mchafu sawasawa na mwanadamu. Leo, ni kwa sababu ya uchafu wako ndiyo Ninakuhukumu, na ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako ndiyo Ninakuadibu. Mimi sijivunii nguvu Zangu kwenu au kuwadhulumu kwa makusudi; Ninafanya mambo haya kwa sababu ninyi, ambao mmezaliwa katika nchi hii ya uchafu, mmenajisiwa vikali kwa uchafu. Mmepoteza uadilifu na ubinadamu wenu kabisa na mmekuwa kama nguruwe waliozaliwa katika pembe chafu zaidi za ulimwengu, na kwa hiyo ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mnahukumiwa na ndiyo Ninawaachia huru hasira Yangu. Ni kwa sababu hasa ya hukumu hii ndiyo mmeweza kuona kuwa Mungu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba Mungu ndiye Mungu mtakatifu; ni kwa sababu hasa ya utakatifu Wake na haki Yake ndiyo Anawahukumu na kuachia huru hasira Yake juu yenu. Kwa sababu Anaweza kufichua tabia Yake yenye haki Aonapo uasi wa mwanadamu, na kwa sababu Anaweza kufichua utakatifu Wake anapoona uchafu wa mwanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na wa asili, na bado Anaishi katika nchi ya uchafu. Mungu angelikuwa mtu na kufuata mfano wa mwanadamu na kugaagaa na wanadamu katika matope machafu, basi kusingelikuwa na chochote kitakatifu kumhusu, na Asingelikuwa na tabia yenye haki, na kwa hiyo Asingelikuwa na haki ya kuhukumu uovu wa mwanadamu, wala Asingelikuwa na haki ya kutekeleza hukumu ya mwanadamu. Mtu angelimhukumu mtu mwingine, haingekuwa kana kwamba anajipiga kofi usoni? Watu ambao wote ni wachafu kwa kiwango sawa wanastahili vipi kuwahukumu wale ambao ni sawa na wao? Ni Mungu mtakatifu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu. Mwanadamu angewezaje kuhukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na mwanadamu angewezaje kuwa na sifa za kulaani dhambi hizi? Mungu Asingelikuwa na sifa ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki Mwenyewe? Tabia potovu za watu zinapofichuliwa, Mungu hunena ili Awahukumu watu, na ni hapo tu ndipo watu wanapoona kuwa Yeye ni mtakatifu. Anapomhukumu na kumwadibu mwanadamu kwa ajili ya dhambi zake, wakati huo wote Akizifichua dhambi za mwanadamu, hakuna mtu au kitu kinachoweza kuepuka hukumu hii; mambo yote ambayo ni machafu yanahukumiwa na Yeye, na ni kwa sababu hiyo tu ndiyo tabia Yake inaweza kusemwa kuwa yenye haki. Kama ingekuwa vinginevyo, ingewezaje kusemwa kwamba ninyi ni foili kwa jina na kwa kweli?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp