Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 470
Kwa kila hatua ya kazi ya Mungu, kunayo njia ambayo watu wanapaswa washirikiane. Mungu Anawasafisha watu ili wawe na imani katikati ya...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Wakati mtu hana maarifa yaliyo wazi na hajapitia ukuu wa Mungu na mipangilio Yake, maarifa ya mtu kuhusu hatima na yale ya kifo yatakuwa yale yasiyoeleweka. Watu hawawezi kuona waziwazi kwamba haya yote yamo kwenye kiganja cha mkono wa Mungu, hawatambui kwamba Mungu ameushika usukani na Anashikilia ukuu juu yao, hawatambui kwamba binadamu hawezi kutupa nje au kutoroka ukuu kama huo; na kwa hivyo wakati wanapokabiliwa na kifo hakuna mwisho wowote katika maneno yao ya mwisho, wasiwasi wao, na hata majuto. Wanalemewa sana na mambo mengi, wanajivuta ajabu, kunakuwa na mkanganyo mkubwa, na haya yote yanawafanya kuogopa kifo. Kwani mtu yeyote aliyezaliwa ulimwenguni humu, kuzaliwa kwake kunahitajika, na kuaga kwake hakuwezi kuepukika, na hakuna mtu anayeweza kuupiga chenga mkondo huu. Kama mtu atataka kuondoka ulimwenguni humu bila maumivu, kama mtu atataka kukabiliana na awamu ya mwisho ya maisha bila kusitasita au wasiwasi, njia pekee ni kutokuwa na majuto. Na njia pekee ya kuondoka bila majuto ni kujua ukuu wa Muumba, kujua mamlaka yake, na kunyenyekea mbele zake. Ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuwa mbali na mahangaiko ya binadamu, maovu, utumwa wa Shetani; ni kwa njia hii ndipo mtu anaweza kuishi maisha kama ya Ayubu, akiongozwa na akibarikiwa na Muumba, maisha yaliyo huru na yaliyokombolewa, maisha yenye thamani na maana, maisha yenye uaminifu na moyo wazi; ni kupitia kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kunyenyekea, kama Ayubu, kujaribiwa na kunyang’anywa na Muumba, kunyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Muumba; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kumwabudu Muumba maisha yake yote na kuweza kupata pongezi Lake, kama Ayubu alivyopata, na kusikia sauti Yake, kumwona akionekana; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi na kufa kwa furaha, kama Ayubu, bila ya maumivu, bila wasiwasi, bila majuto; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi kwa nuru, kama Ayubu, kupita kila mojawapo ya awamu ya maisha kwa nuru, na kukamilisha vizuri safari yake kwa nuru, kutimiza kwa ufanisi kazi yake maalum—kupitia, kujifunza, na kujua ukuu wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa—na kuiaga dunia kwa nuru, na milele hadi milele kusimama upande wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa, kilichopongezwa na Yeye.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Kwa kila hatua ya kazi ya Mungu, kunayo njia ambayo watu wanapaswa washirikiane. Mungu Anawasafisha watu ili wawe na imani katikati ya...
Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu Kabla ya kuwa na mitazamo au...
Kwa hakika, tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haijafichika, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi...
Katika mpango wa Mungu wa miaka elfu kadhaa, kazi inayofanywa ndani ya mwili ni katika sehemu mbili: Kwanza ni kazi ya kusulubiwa, ambayo...
Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 133