Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 142

Ni sifa ya uwakilishi gani inaonyeshwa na kazi ya Shetani kwa mwanadamu? Mnapaswa kujua kuhusu hii kutokana na uzoefu wenu wenyewe—sifa ya uwakilishi zaidi ya Shetani, kitu ambacho anafanya zaidi, kitu ambacho anajaribu kufanya na kila mtu. Ana sifa ambayo pengine hamwezi kuona, ili msiweze kufikiria jinsi Shetani anatisha na wa kuchukia. Kuna mtu anayejua sifa hii ni nini? Niambieni. (Kila kitu anachofanya kinafanywa kumdhuru mwanadamu.) Anafanya vitu kumdhuru mwanadamu. Anamdhuru mwanadamu vipi? Mnaweza kunionyesha hasa zaidi na kwa kina? (Anamshawishi, anamlaghai na kumjaribu mwanadamu.) Hii ni sahihi, hii inaonyesha vipengele vingi. Kuna vingine? (Anamdanganya mwanadamu.) Anadanganya, anashambulia na anatuhumu. Ndiyo, haya yote. Kuna mengine zaidi? (Anasema uwongo.) Udanganyifu na uongo hujitokeza kiasili kabisa kwa Shetani, Anafanya hivi mara nyingi hadi uongo unabubujika kutoka kwa mdomo wake bila yeye hata kuhitaji kufikiria. Mengine zaidi? (Anapanda mfarakano.) Hii si muhimu sana. Nitawaelezea kitu ambacho kitawatisha, lakini Sifanyi hivyo ili kuwaogopesha. Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu na mwanadamu anathaminiwa katika mtazamo na moyo wa Mungu. Kinyume na hayo, Shetani anamthamini mwanadamu? Hamthamini mwanadamu. Anataka nini na mwanadamu? Anataka kumdhuru mwanadamu, anachofikiria tu ni kumdhuru mwanadamu. Hii si sahihi? Wakati anafikiria kumdhuru mwanadamu, anafanya hivyo katika hali ya dharura ya akili? (Ndiyo.) Kwa hivyo inapokuja kwa kazi ya Shetani kwa mwanadamu, hapa Nina maneno mawili yanayoweza kuelezea vizuri asili yenye nia mbaya na ovu ya Shetani, yanayoweza kuwaruhusu kujua chuki ya Shetani: Katika mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu, daima anataka kumiliki na kumtawala kwa nguvu, kila mmoja wao, ili aweze kufika mahali ambapo anaweza kumdhibiti mwanadamu kabisa, kumdhuru mwanadamu, ili aweze kutimiza lengo hili na tamaa isiyowezekana. “Umiliki wa nguvu” unamaanisha nini? Unafanyika na kibali chako, ama bila kibali chako? Unafanyika na kujua kwako, ama bila kujua kwako? Ni bila kujua kwako kabisa! Katika hali ambazo huna ufahamu, pengine wakati hajasema chochote ama pengine wakati hajafanya chochote, wakati hakuna kauli kigezo, hakuna muktadha, yuko hapo karibu nawe, akikuzunguka. Anatafuta fursa ya kukunyonya, kisha anakumiliki kwa nguvu, anakutawala, kutimiza lengo lake la kukudhibiti kikamilifu na kukudhuru. Hii ni nia na tabia ya kawaida zaidi katika mapambano ya Shetani dhidi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mnahisi vipi mnaposikia haya? (Tuna hofu na woga katika mioyo yetu.) Mnahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Mnapohisi kuchukizwa, mnafikiria Shetani hana haya? (Ndiyo.) Mnapofikiria Shetani hana haya, mnahisi kuchukizwa na wale watu walio karibu nanyi ambao daima wanataka kuwatawala, wale walio na matarajio yasiyowezekana ya hadhi na maslahi yao? (Ndiyo.) Hivyo ni mbinu gani anazotumia Shetani kumtawala kwa nguvu na kummiliki mwanadamu? Mnaelewa hii vizuri? Mnaposikia virai hivi viwili vya “umiliki wa nguvu” na “utawala,” mnapata hisia isiyo ya kawaida na mnahisi maudhi, sivyo? Je, mnapata kionjo cha ladha yao mbovu? Bila kibali ama maarifa yako anakutawala, anakumiliki na kukupotosha. Unaweza kuonja nini kwa moyo wako? Chuki? (Ndiyo.) Maudhi? (Ndiyo.) Wakati unahisi hii chuki na maudhi kwa njia hii ya Shetani, una hisia gani kwa Mungu? (Kushukuru.) Kushukuru Mungu kwa kukuokoa. Kwa hivyo sasa, wakati huu, unayo hamu ama matakwa ya kumwacha Mungu kuongoza yako yote na kutawala yako yote? (Ndiyo.) Kwa muktadha upi? Unasema ndiyo kwa sababu unaogopa kumilikiwa kwa nguvu na kutawaliwa na Shetani? (Ndiyo.) Huwezi kuwa na mawazo kama haya, siyo sahihi. Usiwe na hofu, Mungu yuko hapa. Hakuna chochote cha kuhofia, siyo? Ukishaelewa asili mbovu ya Shetani, unapaswa kuwa na uelewa sahihi zaidi ama upendo wa kina wa mapenzi ya Mungu, nia nzuri za Mungu, huruma ya Mungu na stahamala kwa mwanadamu na tabia Yake ya haki. Shetani ni wa kuchukia sana, lakini ikiwa hii bado haitii moyo upendo wako kwa Mungu na utegemezi na uaminifu wako kwa Mungu, basi wewe ni mtu wa aina gani? Uko tayari kumwacha Shetani akudhuru hivyo? Baada ya kuona uovu na ubaya wa Shetani, tunamgeuza na kisha kumwangalia Mungu. Maarifa yako ya Mungu sasa yamepitia mabadiliko yoyote? (Ndiyo.) Mabadiliko ya aina gani? Tunaweza kusema Mungu ni mtakatifu? Tunaweza kusema Mungu hana dosari? “Mungu ni utakatifu wa kipekee”—Mungu anaweza kuvumilia jina hili? (Ndiyo.) Hivyo kwa dunia na miongoni mwa mambo yote, ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kuvumilia huu uelewa wa mwanadamu? Kuna wengine? (La.) Hivyo, ni nini hasa Mungu anampatia mwanadamu? Je, Anakupa tu utunzaji, wasiwasi na kukutia maanani kidogo wakati huko makini? Mungu amempa nini mwanadamu? Mungu amempa mwanadamu uhai, Amempa mwanadamu kila kitu, na amempa mwanadamu bila masharti bila kudai chochote, bila nia zozote za siri. Anatumia ukweli, Anatumia maneno Yake, Anatumia uhai Wake kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu, kumtoa mwanadamu mbali na madhara ya Shetani, mbali na majaribio ya Shetani, mbali na ushawishi wa Shetani na kumruhusu mwanadamu kuona wazi asili mbovu ya Shetani na uso wake unaotisha. Je, upendo na wasiwasi wa Mungu kwa binadamu ni wa kweli? Ni kitu ambacho kila mmoja wenu anaweza kupitia? (Ndiyo.)

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp