Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 143

Kumbuka maisha yenu hadi sasa kwa yote ambayo Mungu amekufanyia katika miaka yote ya imani yako. Iwapo unaihisi kwa kina au la, haikuwa ya umuhimu sana? Haikuwa kile ulichohitaji zaidi kupata? (Ndiyo.) Huu si ukweli? Huu si uhai? (Ndiyo.) Kwa hivyo Mungu amewahi kukupa nuru kurudisha chochote ama kulipia kitu baada ya Yeye kukupa vitu hivi? (La.) Kwa hivyo madhumuni ya Mungu ni yapi? Mbona Mungu anafanya hivi? Mungu pia ana lengo la kukumiliki? (La.) Je, Mungu anataka kuwa mfalme katika moyo wa mwanadamu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini tofauti kati ya Mungu kuwa mfalme na umiliki wa nguvu wa Shetani? Mungu anataka kupata moyo wa wanadamu, Anataka kumiliki moyo wa mwanadamu—hii inamaanisha nini? Je, inamaanisha kwamba Mungu anataka mwanadamu kuwa vikaragosi Vyake? Mashine Yake? (La.) Kwa hivyo madhumuni ya Mungu ni nini? Kuna tofauti kati ya Mungu kutaka kumiliki moyo wa mwanadamu na umiliki wa nguvu wa Shetani na utawala wa mwanadamu? (Ndiyo.) Tofauti ni nini? Unaweza kuniambia wazi? (Shetani anaifanya kupitia kwa nguvu ilhali Mungu anaacha mwanadamu ajitolee.) Shetani anaifanya kupitia kwa nguvu ilhali Mungu anaacha mwanadamu ajitolee. Hii ndiyo tofauti? Mungu anataka moyo wako kufanyia nini? Na zaidi ya hayo, kwa nini Mungu anataka kukumiliki? Mnaelewa vipi ndani ya mioyo yenu “Mungu anamiliki moyo wa mwanadamu”? Ni lazima tuwe na haki kwa Mungu hapa, vinginevyo watu daima hawataelewa, na kufikiri: “Mungu daima anataka kunimiliki. Anataka kunimiliki kwa nini? Sitaki kumilikiwa, nataka tu kuwa mimi mwenyewe. Mnasema Shetani anawamiliki watu, lakini Mungu pia anawamiliki watu: Haya si sawa? Sitaki kumwacha yeyote kunimiliki. Mimi ni mimi mwenyewe!” Tofauti hapa ni nini? Chukua dakika kuifikiria. Nawauliza, je “Mungu hummiliki mwanadamu” ni kirai tupu? Umiliki wa Mungu wa mwanadamu unamaanisha kwamba Anaishi katika moyo wako na anatawala kila neno na kusonga kwako? Akikwambia uketi, huthubutu kusimama? Akikwambia uende Mashariki, huthubutu kwenda Magharibi? Je, ni umiliki unaomaanisha kitu kama hiki? (La.) Kwa hivyo ni nini? (Inaamisha kwa mwanadamu kuishi kwa kudhihirisha kile Mungu anacho na alicho.) Kwa miaka hii yote Mungu amemsimamia mwanadamu, kwa kazi Yake kwa mwanadamu hadi sasa kwa hatua hii ya mwisho, ni athari ipi imekusudiwa kwa mwanadamu kuhusu maneno yote ambayo Amesema? Je, ni kwamba mwanadamu anaishi kulingana na kile anacho Mungu na alicho? Kwa kuangalia maana halisi ya “Mungu humiliki moyo wa mwanadamu,” inaonekana kama Mungu anachukua moyo wa mwanadamu na kuumiliki, Anaishi ndani yake na Hatoki nje tena; Anaishi ndani yake na kuwa bwana wa moyo wa mwanadamu, kutawala na kupanga moyo wa mwanadamu atakavyo, ili mwanadamu lazima aende asemapo Mungu aende. Katika kiwango hiki cha maana, inaonekana ni kama kila mtu alikuwa amekuwa Mungu, amemiliki kiini cha Mungu, amemiliki tabia ya Mungu. Kwa hivyo hapa, mwanadamu pia angeweza kufanya vitendo na matendo ya Mungu? Je, “umiliki” unaweza kuelezewa kwa njia hii? (La.) Kwa hivyo ni nini? Nawauliza hii: Je, maneno na ukweli wote Mungu anampa mwanadamu ni ufunuo wa kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho? (Ndiyo.) Hii ni ya uhakika. Lakini je, maneno yote Mungu anampa mwanadamu ni ya Mungu Mwenyewe kuweka katika vitendo, ya Mungu Mwenyewe kumiliki? Chukua dakika moja kuifikiria? Wakati Mungu anamhukumu mwanadamu, Anafanya hivi kwa sababu ya nini? Maneno haya yalitoka wapi? Ni nini yaliyomo katika maneno haya ambayo Mungu anazungumza Anapomhukumu mwanadamu? Ni nini msingi wake? Msingi wake ni tabia potovu ya mwanadamu? (Ndiyo.) Kwa hivyo athari iliyofikiwa na hukumu ya Mungu ya mwanadamu imetokana na kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo umiliki wa Mungu wa mwanadamu ni kirai tupu? Kwa hakika sicho. Kwa hivyo mbona Mungu anasema maneno haya? Ni nini madhumuni Yake ya kusema maneno haya? Anataka kutumia maneno haya kwa maisha ya mwanadamu? (Ndiyo.) Mungu anataka kutumia ukweli huu wote ambao amezungumza kwa maisha ya mwanadamu. Wakati mwanadamu anachukua ukweli huu wote na neno la Mungu na kuyabadilisha katika maisha yake, mwanadamu basi anaweza kumtii Mungu? Mwanadamu basi anaweza kumcha Mungu? Mwanadamu basi anaweza kuepuka maovu? Wakati mwanadamu amefika hapa, anaweza basi kutii ukuu na mipango ya Mungu? Mwanadamu sasa yuko katika nafasi ya kutii mamlaka ya Mungu? Wakati watu kama Ayubu, ama kama Petro wanafika mwisho wa barabara yao, wakati maisha yao yanaweza kufikiriwa kuwa yamekomaa, wakati wako na uelewa halisi wa Mungu—Shetani bado anaweza kuwapoteza? Shetani bado anaweza kuwamiliki? Shetani bado anaweza kuwatawala kwa nguvu? (La.) Kwa hivyo huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni mtu ambaye amepatwa kabisa na Mungu? (Ndiyo.) Katika kiwango hiki cha maana, unamwonaje mtu huyu ambaye amepatwa kabisa na Mungu? Kwa Mungu, katika hali hii tayari Amemiliki moyo wa mtu huyu. Lakini mtu huyu anahisi nini? Je, ni kwamba neno la Mungu, mamlaka ya Mungu, na njia ya Mungu yamekuwa uhai ndani ya mwanadamu, basi uhai huu unamiliki utu wote wa mwanadamu, na unafanya yote anayozidi pamoja na kiini chake kutosha kumridhisha Mungu? Kwa Mungu, moyo wa binadamu wakati huu umemilikiwa na Yeye? (Ndiyo.) Mnaelewaje kiwango hiki cha maana sasa? Je, ni Roho wa Mungu anayekumiliki? (La.) Kwa hivyo ni nini hasa kinachokumiliki? (Neno la Mungu.) Ni njia ya Mungu na neno la Mungu. Ni ukweli ambao umekuwa maisha yako, na ni neno la Mungu ambayo yamekuwa maisha yako. Wakati huu, mwanadamu basi ana maisha yanayotoka kwa Mungu, lakini hatuwezi kusema kwamba haya maisha ni maisha ya Mungu. Kwa maneno mengine, hatuwezi kusema kwamba maisha ambayo mwanadamu anapaswa kupata kutoka kwa neno la Mungu ni maisha ya Mungu. Hivyo, licha ya muda ambao mwanadamu anamfuata Mungu, licha ya idadi ya maneno ambayo mwanadamu anapata kutoka kwa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa Mungu. Hii ni sahihi? (Ndiyo.) Hata kama siku moja Mungu aseme, “Nimemiliki moyo wako, sasa unamiliki maisha Yangu,” utahisi basi kwamba wewe ni Mungu? (La.) Utakuwa nini basi? Hutakuwa na utii kabisa wa Mungu? Mwili na moyo wako hautajawa na maisha Mungu amekupa? Huu ni udhihirisho wa kawaida wakati Mungu anamiliki moyo wa mwanadamu. Huu ni ukweli. Kwa hivyo kuuangalia kutoka kipengele hiki, mwanadamu anaweza kuwa Mungu? (La.) Wakati mwanadamu amepata maneno yote ya Mungu, wakati mwanadamu anaweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, mwanadamu basi anaweza kumiliki utambulisho wa Mungu? (La.) Mwanadamu anaweza basi kumiliki kiini cha Mungu? (La.) Licha ya kile kitakachofanyika, mwanadamu bado ni mwanadamu wakati yote yamesemwa na kufanywa. Wewe ni kiumbe; wakati umepokea neno la Mungu kutoka kwa Mungu na kupokea njia ya Mungu, unamiliki tu maisha ambayo yanatoka kwa neno la Mungu, na kamwe huwezi kuwa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp