Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 144

Majaribu ya Shetani

Mat 4:1-4 Baada ya hapo Yesu akaongozwa mwituni na Roho Mtakatifu kwa minajili ya kujaribiwa na ibilisi. Na baada ya kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, alihisi njaa. Na aliyemjaribu alipokuja kwake, alimwambia, Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike mikate. Lakini akamjibu na kusema, imeandikwa, Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.

Haya ndiyo maneno ambayo ibilisi kwanza alijaribu kumjaribu Bwana Yesu. Ni nini maudhui ya aliyoyasema ibilisi? (“Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike mikate.”) Ibilisi alisema maneno haya, ambayo yalikuwa rahisi kiasi, lakini kuna shida na maudhui muhimu ya maneno haya? (Ndiyo.) Shida ni nini? Alisema, “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu,” lakini katika moyo wake, alijua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mwana wa Mungu? Alijua kwamba Alikuwa Kristo? (Ndiyo.) Basi kwa nini alisema “Iwapo wewe ni”? (Alikuwa akijaribu kumjaribu Mungu.) Hakika, alikuwa akijaribu kumjaribu Mungu, lakini ni nini madhumuni ya kufanya hivyo? Alisema, “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu.” Katika moyo wake alijua kwamba Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, haya yalikuwa wazi katika moyo wake, lakini licha ya haya, alinyenyekea Kwake au kumwabudu Yeye? (La.) Alitaka kufanya nini? Alitaka kufanya hivi na kusema maneno haya kumfanya Bwana Yesu kukasirika na kisha kumshawishi kuchukua chambo, na kumdanganya Bwana Yesu kufanya mambo kulingana na njia yake ya kufikiri na kuinuka kwa chango chake. Si alimaanisha hivi? Katika moyo wa Shetani alijua wazi kwamba huyu alikuwa Bwana Yesu Kristo, lakini alisema hivi hata hivyo. Hii si asili ya Shetani? Asili ya Shetani ni nini? (Kuwa mjanja, mwovu na kutokuwa na Heshima kwa Mungu.) Hamheshimu Mungu. Ni kitu kipi hasi alichokuwa akifanya hapa? Hakutaka kumshambulia Mungu? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, alisema: “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike mikate”; si hii ni nia ovu ya Shetani? (Ndiyo.) Alikuwa anajaribu kufanya nini kweli? Lengo lake ni wazi sana: Alikuwa anajaribu kutumia mbinu hii kukanusha nafasi na utambulisho wa Bwana Yesu Kristo. Alisema, “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Usipo, basi wewe siwe Mwana wa Mungu na Hufanyi kazi hii.” Ni haya yaliyomaanishwa hapa? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, alitaka kuvunja na kuharibu kazi ya Mungu; huu ndio uovu wa Shetani. Uovu wake ni maonyesho ya kiasili ya asili yake. Ingawaje alijua Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, kupata mwili kwenyewe kwa Mungu Mwenyewe, hangeweza kuwacha kufanya kitu kama hiki, kumfuata Mungu nyuma na kuendelea kumshambulia na kujaribu sana kuvuruga na kuharibu kazi ya Mungu.

Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichotumia Shetani: “yaamrishe mawe haya yabadilike mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Iwapo kuna chakula, mbona usile? Mbona ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? (La.) Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? Je, Alikuwa na chakula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upuuzi wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Shetani anafanya idadi fulani ya mambo; unaona asili yake ovu na yenye kudhuru na unaona akiharibu kazi ya Mungu, na wa kuchukiza na kuudhi sana. Lakini kwa upande mwingine, unapata asili ya kitoto na ujinga nyuma ya maneno na vitendo vyake? (Ndiyo.) Huu ni ufunuo kuhusu asili ya Shetani; ana asili ya aina hii na atafanya kitu kama hiki. Kwa wanadamu, kirai hiki ni cha upuuzi na cha kuchekesha. Lakini maneno kama hayo kwa hakika yanaweza kutamkwa na Shetani. Tunaweza kusema kwamba ni asiyejua? Mjinga? Uovu wa Shetani uko kila mahali na daima unafichuliwa. Na Bwana Yesu anamjibu aje? (“Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.”) Maneno haya yana nguvu yoyote? (Yanayo.) Mbona tunasema kwamba yana nguvu? (Ni ya ukweli.) Sahihi. Maneno haya ni ukweli. Sasa, mtu anaishi kwa mkate tu? Bwana Yesu alifunga kwa siku na usiku 40. Alikufa kwa njaa? (La.) Hakufa kwa njaa, kwa hivyo Shetani alimkaribia, akimwambia abadili mawe yawe chakula kwa kusema kitu kama hiki: “Ukiyabadili mawe yawe chakula, Hutakuwa basi na vitu vya kula? Si basi Hutalazimika kufunga, Hutalazimika kuwa na njaa?” Lakini Bwana Yesu alisema, “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee,” inayomaanisha kwamba, ingawa mwanadamu anaishi katika mwili, kile kinachompa uhai, kile kinachouruhusu mwili wake kuishi na kupumua, si chakula, ila maneno yote yaliyotamkwa na kinywa cha Mungu. Katika upande mmoja, mwanadamu anachukulia maneno haya kuwa ukweli. Maneno haya yanampa imani, yanamfanya ahisi kwamba anaweza kumtegemea Mungu, kwamba Mungu ni ukweli. Kwa upande mwingine, kuna kipengele cha vitendo katika maneno haya? (Kunacho.) Mbona? Kwa sababu Bwana Yesu amefunga kwa siku na usiku 40 na bado Anasimama hapo, bado yuko hai. Huu ni mfano? Hajakula chochote, chakula chochote kwa siku na usiku 40. Bado yuko hai. Huu ni ushahidi wa nguvu nyuma ya kirai Chake. Kirai hiki ni rahisi, lakini, kuhusiana na Bwana Yesu, kirai hiki kutoka kwa roho Yake Alifunzwa na mtu mwingine, ama Alikifikiria tu kwa sababu ya kile Shetani alimwambia? Fikiria jambo hili. Kuliweka kwa njia nyingine, Mungu ni ukweli, Mungu ni uhai, lakini je, ukweli na uhai wa Mungu uliongezwa kwa kuchelewa? Ulitokana na uzoefu? (La.) La, ni ya asili ndani ya Mungu, kumaanisha kwamba ukweli na uhai vipo ndani ya kiini cha Mungu. Licha ya kile kinachomfanyikia, Anachofichua ni ukweli. Ukweli huu, kirai hiki—iwapo maudhui yake ni mapama ama finyu—kinaweza kumwacha mwanadamu aishi, kimpe uhai; kinaweza kumwezesha mwanadamu kupata, ndani yake, ukweli, uwazi kuhusu njia ya maisha ya binadamu, na kumwezesha kuwa na imani kwa Mungu. Kwa maneno mengine, ndicho chanzo cha matumizi ya Mungu ya kirai hiki ni chema. Hivyo tunaweza kusema kitu hiki chema ni takatifu? (Ndiyo.) Kirai cha Shetani kinatoka kwa asili ya Shetani. Shetani anafichua asili yake ovu, asili yake yenye kijicho, kila mahali, daima. Sasa, ufunuo huu, Shetani anaufanya kiasili? (Ndiyo.) Kuna yeyote anayemchochea? Kuna yeyote anayemsaidia? Kuna yeyote anayemshurutisha? (La.) Anautoa kwa hiari yake mwenyewe. Hii ni asili ovu ya Shetani. Licha ya kile Mungu anafanya na jinsi Anavyokifanya, Shetani yuko nyuma Yake. Kiini na sura ya ukweli ya vitu hivi ambavyo Shetani anasema na kufanya ni kiini cha Shetani—kiini ovu, kiini cha kuonea kijicho.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp