Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 143

Wakati wa siku za mwisho Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu. Mara tu taswira ya Mungu ndani ya mwanadamu inapozeeka, basi inakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hii ya kazi, Hakuwakilisha Mungu kikamilifu. Alifanya baadhi ya ishara na maajabu, Alizungumza maneno kadhaa, na hatimaye Akasulubishwa, na Aliwakilisha upande mmoja wa Mungu. Hakuweza kuwakilisha yale yote ambayo ni ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya upande mmoja wa kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu, na ni wa ajabu sana, na Haeleweki, na kwa sababu Mungu Anafanya upande mmoja tu wa kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Akazungumza maneno fulani kwa Wanaisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu yaliwekwa wazi, lakini kwa sababu ubora wa tabia ya mwanadamu ulikuwa finyu na hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kukamilika, Mungu Aliendelea kuzungumza na kufanya kazi. Wakati wa Enzi ya Neema, mwanadamu aliweza kuona tena sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu Aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kutoa mapepo, na kusulubishwa, siku tatu baadaye. Akafufuka na Akawatokea watu Akiwa katika mwili. Kumhusu Mungu, mwanadamu hakujua chochote zaidi ya hiki. Mwanadamu anajua tu kile ambacho Mungu Amemwonyesha, na kama Mungu Asingeonyesha chochote zaidi kwa mwanadamu, basi hicho kingekuwa kiwango cha mwanadamu kumwekea mipaka Mungu. Hivyo, Mungu Anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu juu Yake yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili taratibu aweze kuijua hulka ya Mungu. Mungu anatumia maneno yake kumkamilisha mwanadamu. Tabia yako iliyoharibika imewekwa wazi kwa maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinaondolewa na uhalisia wa Mungu. Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kutimiza maneno haya kwamba “Neno Lafanyika kuwa mwili, Neno Lakuwa mwili, na Neno Laonekana katika mwili,” na kama huna maarifa ya kina kuhusu hili, basi hutaweza kusimama imara; wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa Mungu wa usimamizi. Hivyo, maarifa yako yanapaswa kuwa wazi; bila kujali namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, Mungu Hamruhusu mwanadamu kumwekea mipaka. Ikiwa Mungu Asingefanya kazi hii wakati wa siku za mwisho, basi maarifa ya mwanadamu juu Yake yasingeweza kwenda popote. Ungeweza kujua tu kwamba Mungu Anaweza kusulubiwa na Anaweza kuiangamiza Sodoma, na kwamba Yesu Anaweza kufufuliwa kutoka katika wafu na kumtokea Petro…. Lakini usingeweza kusema kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutimiza yote, na yanaweza kumshinda mwanadamu. Ni kwa njia tu ya kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu ndipo unaweza kuzungumza juu ya maarifa hayo, na kadri unapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu zaidi, ndivyo maarifa yako yanavyokuwa ya kina zaidi kumhusu Yeye. Ni baada ya hapo tu ndipo utaacha kumwekea Mungu mipaka ndani ya dhana zako binafsi. Mwanadamu anakuja kumjua Mungu kwa kupitia kazi Yake, na hakuna njia nyingine sahihi ya kumjua Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp