Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Siri Kuhusu Biblia | Dondoo 278

24/06/2020

Wayahudi wa wakati huo wote walisoma kutoka Agano la Kale na walijua unabii wa Isaya kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini. Mbona basi, na maarifa haya, bado walimtesa Yesu? Hii siyo kwa sababu ya asili yao ya kuasi na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu? Wakati huo, Mafarisayo waliamini kwamba kazi ya Yesu ilikuwa tofauti na ile waliyoijua ya mtoto mchanga wa kiume aliyetabiriwa; mwanadamu wa leo anamkataa Mungu kwa sababu kazi ya Mungu mwenye mwili haikubaliani na Biblia. Si kiini cha uasi wao dhidi ya Mungu ni moja na sawa? Unaweza kuwa yule ambaye anakubali tu bila swali kazi yote ya Roho Mtakatifu? Kama ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi ni “mkondo” sawa. Unapaswa kuikubali bila wasiwasi hata kidogo, badala ya kuokota na kuchagua nini cha kukubali. Ukipata maarifa kiasi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari dhidi Yake, hili silo tendo lisilohitajika? Unachopaswa kufanya ni kukubali, bila haja ya kuthibitisha zaidi kutoka kwa Biblia, kazi yoyote iwapo tu ni ya Roho Mtakatifu, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu. Hata kama umegundua ushuhuda usiopingika ndani ya Biblia, haiwezi kukuleta kikamilifu mbele Yangu. Wewe ndiye mmoja anayeishi ndani ya mipaka ya Biblia, na sio mbele Yangu; Biblia haiwezi kukusaidia kunijua, wala haiwezi kuimarisha upendo wako Kwangu. Ingawa Biblia ilitabiri kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa, hakuna yeyote angeweza kuelewa kupitia nani unabii ungetimia, kwani mwanadamu hakujua kazi ya Mungu, na hii ndiyo ilisababisha Mafarisayo kusimama dhidi ya Yesu. Wengine wanajua kwamba kazi Yangu iko katika maslahi ya mwanadamu, lakini bado wanaendelea kuamini kwamba Yesu na Mimi ni viumbe tofauti kabisa visivyopatana. Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri kwa Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu nini mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu. Hasa, haingekuwa tendo la imani ya uwongo kutafuta ndani ya Biblia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Nini unaweza kupambanua tu kwa kushika Biblia kwa mikono yako? Uwe mkalimani wa Biblia ama mhubiri, nani anaweza kujua mbeleni kazi ya leo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp