Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 173

Kazi ya Roho Mtakatifu inakamilishwa na kukamilika kupitia watu wa aina nyingi na hali nyingi tofauti tofauti. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inaweza kuwakilisha kazi ya enzi zote, na inaweza kuwakilisha uingiaji wa watu katika enzi nzima, kazi kwa watu wengi bado inahitajika kufanywa na watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu na sio Mungu mwenye mwili. Kwa hivyo, kazi ya Mungu, au huduma ya Mungu mwenyewe, ni kazi ya Mungu mwenye mwili na haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya Roho Mtakatifu imekamilishwa kupitia watu wa aina mbalimbali na haiwezi kukamilishwa na mtu mahususi mmoja tu, au kufafanuliwa kikamilifu kupitia mtu mmoja mahususi. Wale ambao wanaongoza kanisa pia hawawezi kuiwakilisha kazi ya Roho Mtakatifu kikamilifu; wanaweza kufanya tu kazi fulani ya kuongoza. Kwa njia hii, kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kugawanywa katika sehemu tatu: Kazi ya Mungu mwenyewe, kazi ya wanadamu wanaotumiwa, na kazi kwa wale wote walioko katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Miongoni mwa hizo tatu, kazi ya Mungu ni kuongoza enzi nzima; kazi ya wanadamu wanatumiwa ni kuwaongoza wafuasi wote wa Mungu kwa kutumwa au kupokea maagizo kwa ajili ya kazi ya Mungu mwenyewe; na wanadamu hawa ndio wanaoshirikiana na kazi ya Mungu; kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa wale waliopo katika mkondo wake ni kudumisha kazi Yake yote, yaani, kudumisha usimamizi wote na kudumisha ushuhuda Wake, na wakati uo huo kuwakamilisha wale wanaoweza kukamilishwa. Sehemu tatu hizi ni kazi kamili ya Roho Mtakatifu, lakini bila kazi ya Mungu Mwenyewe, kazi yote ya usimamizi inaweza kutuama. Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo unaofanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi. Kwa sababu ya utambulisho na uwakilishaji tofauti wa kazi hii, licha ya ukweli kwamba zote ni kazi za Roho Mtakatifu, kuna tofauti za wazi na bainifu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Aidha, kiwango cha kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa watu wenye tambulisho tofauti inatofautiana. Hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp