Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 324

08/07/2020

Mnafaa nyote kufahamu sasa maana kamili ya kumwamini Mungu. Maana ya imani katika Mungu Niliyozungumzia awali inahusiana na kuingia kwenu kwa hali dhahiri. Lakini leo hii si juu ya hayo. Leo hii Ningependa kuchambua umuhimu wa imani yako katika Mungu. Bila shaka, lengo la jambo hili ni kuwaelekeza kutoka kwenye mabaya; Nisipofanya hivyo, basi hamtawahi kuifahamu sura yako kamili na utakuwa ukijisifu kila mara kuhusu kujitolea kwako na uaminifu wako. Kwa maneno mengine, Nisipoangazia uovu uliomo ndani ya mioyo yenu, basi kila mmoja wenu atajitwika taji kichwani na kujipa utukufu wote. Asili zenu za majivuno na viburi huwaelekeza kusaliti dhamiri zenu wenyewe, kuasi na kumpinga Kristo, na kufichua uovu wenu, hivyo basi kuleta kwenye mwangaza fikra zenu, mawazo, tamaa nyingi na macho yaliyojaa ulafi. Ilhali mnaendelea kukiri kwamba mtajitolea maisha yenu kwa ajili ya kazi ya Kristo, na mnakariri tena na tena mambo ya kweli yaliyosemwa na Kristo zamani zile. Hii ndiyo “imani” yenu. Hii ndiyo “imani yenu isiyokuwa na doa”. Kwa muda huu wote, Nimemweka mwanadamu katika nidhamu ya hali ya juu. Iwapo uaminifu wako unakuja na nia na masharti, basi ni heri Nisijihusishe na huo mnaoita uaminifu wenu hata kidogo, kwa maana Ninachukia wale hunidanganya kupitia kwa nia zao na kunanihadaa na masharti. Mapenzi Yangu ni mwanadamu aniamini Mimi peke Yangu, na afanye mambo yote kwa ajili ya, na kudhibitisha neno hilo moja: imani. Ninachukizwa na matumizi yenu ya maneno matamu ili Unifurahishe Mimi. Kwa maana daima Mimi napenda mtende pia kwa ukweli mtupu na uwazi na hivyo Ningependa pia mfanye matendo yenu Kwangu kwa imani ya kweli. Inapofika katika swala la imani, watu wengi hufikiri kwamba wanamfuata Mungu kwa sababu wako na imani, la sivyo hawangevumilia mateso hayo. Basi Nakuuliza hivi: Ni kwa nini humheshimu Mungu ilhali unaamini kuwepo Kwake? Ni kwa nini, basi, haumchi Mungu moyoni mwako iwapo unaamini kuwa Mungu Yupo? Unakubali kuwa Kristo ni kupata mwili kwa Mungu, basi ni kwa nini uwe na dharau na matendo yasiyo na heshima Kwake? Ni kwa nini unamhukumu wazi wazi? Ni kwa nini unatazama mienendo Yake kila wakati? Mbona usijisalimishe katika mipango Yake? Ni kwa nini hutendi kulingana na neno Lake? Ni kwa nini unamhadaa na kumpokonya matoleo Yake? Ni kwa nini unazungumza katika nafasi ya Kristo? Ni kwa nini unatoa hukumu ya kubaini iwapo kazi Yake na neno Lake ni ya kweli? Mbona unadhubutu kumkufuru Yeye kisiri? Ni mambo haya na mengine ndiyo yanayounda imani yenu?

Kila sehemu ya usemi na tabia zenu hufichua dalili za kutoamini katika Kristo ulizobeba ndani yako. Nia na malengo yenu kwa yale mnayoyafanya yamejaa kutoamini; hata hiyo hisi itokayo kwa macho yenu imetiwa doa na dalili hizi. Kwa maneno mengine, kila mmoja wenu, katika kila dakika ya kila siku, amebeba vipengele vyenu vya kutoamini. Hii ina maana kuwa kila wakati mko katika hatari ya kumsaliti Kristo, kwa maana damu iliyo ndani ya mishipa yenu imechanganyika na kutomwamini Mungu Aliyepata mwili. Kwa hivyo, Ninasema kwamba nyayo mnazoziwacha katika njia ya imani katika Mungu si nyingi. Safari yenu katika njia ya kumwamini Mungu haina msingi mzuri, na badala yake mnafanya kazi bila ya kujali matokeo yake. Nyinyi huwa na shaka na neno la Kristo na huwezi kulitia katika matendo mara moja. Hii ndio sababu ya nyinyi kutokuwa na imani katika Kristo, na daima kuwa na fikira kumhusu Kristo ndio sababu nyingine ya nyinyi kutoamini Kristo. Kuwa na shaka kila mara kuhusu kazi ya Kristo, kuacha neno Lake kuangukia sikio lisilosikia, kuwa na maoni kwa kila kazi inayofanywa na Kristo na kutoifahamu vizuri kazi hiyo, kuwa na ugumu wa kutupilia mbali fikira zako hata baada ya nyinyi kupewa sababu za kufanya vile, na kadhalika; hizi zote ni dalili za kutoamini zilizochanganyika ndani ya mioyo yenu. Ingawa mnafuata kazi ya Kristo na kamwe hubaki nyuma, kuna uasi mwingi uliochanganyika ndani ya mioyo yenu. Uasi huu ni doa la uchafu katika imani yenu kwa Mungu. Pengine hamkubaliani na haya, lakini iwapo huwezi kutambua nia yako kutoka kwayo, basi wewe ndiwe utakayeangamia. Kwa maana Mungu hustawisha wale wanaomwamini kwa kweli pekee, wala sio wale walio na shaka na hasa wale wanaomfuata na hawajawahi kuamini kuwa Yeye ni Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp