Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 191

Mungu amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, lakini hakuna mtu yeyote aliyejua kuhusu jambo hilo. Hata leo hii, hakuna mtu anayelitambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajitambulishi. Mtu anaweza kusema kwamba ni kana kwamba hatua hii ya kazi Yake inafanyika katika ulimwengu wa mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua. Mungu atakapomaliza hatua hii ya kazi Yake, kila mtu atazinduka kutoka katika ndoto yake ndefu na kugeuza mtazamo wake wa zamani. Nakumbuka Mungu akisema wakati mmoja, “Kuja katika mwili wakati huu ni sawa na kuanguka katika tundu la duma.” Hii ina maana kwamba kwa sababu awamu hii ya kazi ya Mungu imemfanya Mungu kuja katika mwili na kuzaliwa katika makazi ya joka kuu jekundu, kuja Kwake duniani wakati huu kumeambatana na hatari nyingi hata zaidi. Anachokabiliana nacho ni visu na bunduki na rungu; Anachokabiliana nacho ni vishawishi; Anaokutana nao ni umati wa watu wenye sura hatari zinazoonyesha kutaka kuua. Ana hatari ya kuuawa wakati wowote. Mungu alikuja na ghadhabu. Hata hivyo, Alikuja ili Aweze kufanya kazi ya kukamilisha, ikiwa na maana kwamba kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake inayoendelea baada ya kazi ya wokovu. Kwa ajili ya hatua hii ya kazi Yake, Mungu amejitolea mawazo na uangalizi wa hali ya juu kabisa na Anatumia njia yoyote inayoweza kufikiriwa ili kuepuka mashambulio ya majaribu, Akijificha kwa unyenyekevu Wake na kamwe haringii utambulisho Wake. Katika kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, Yesu alikuwa Anakamilisha tu kazi ya wokovu; Hakuwa anafanya kazi ya kukamilisha. Hivyo ni nusu tu ya kazi ya Mungu ndiyo ilikuwa inafanywa, na kukamilisha kazi ya ukombozi ilikuwa ni nusu tu ya mpango Wake mzima. Kwa kuwa enzi mpya ilikuwa inakaribia kuanza na ile ya zamani kukaribia kutoweka, Mungu Baba alianza kufikiria kwa makini kuhusu sehemu ya pili ya kazi Yake na Akaanza kujiandaa kwa ajili yake. Wakati uliopita, kupata mwili huku katika siku za mwisho huenda hakukutolewa unabii, na hivyo kuliweka msingi wa usiri mkubwa unaozunguka ujio wa Mungu katika mwili katika kipindi hiki. Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari amewasili duniani. Mungu alifanya kazi hivi ili Aifanye kazi Yake kwa urahisi na kupata matokeo bora zaidi, na pia ilikuwa ni kwa sababu ya kuepuka majaribu zaidi. Mwanadamu anapoamka kutoka usingizini, kazi ya Mungu itakuwa imekwisha kamilika zamani sana na Ataondoka, na kukamilisha maisha Yake ya kutembeatembea na kusafiri duniani. Kwa kuwa kazi ya Mungu inamtaka Mungu kutenda na kuzungumza Yeye binafsi, na kwa kuwa hakuna namna ambayo mwanadamu anaweza kusaidia, Mungu amevumilia maumivu makali ili kuja duniani kufanya kazi Yeye mwenyewe. Mwanadamu hawezi kushikilia nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hiyo Mungu alijihatarisha mara elfu kadhaa kuliko ilivyokuwa katika wakati wa Enzi ya Neema ili kuja chini mahali ambapo joka kuu jekundu linaishi ili kufanya kazi Yake, kuweka mawazo Yake yote na uangalizi katika kuokoa kundi hili la watu maskini, kulikomboa kundi hili la watu lililochafuliwa katika rundo la samadi. Ingawa hakuna anayejua uwepo wa Mungu, Mungu hahangaiki kwa sababu ni faida kubwa sana kwa kazi ya Mungu. Kila mtu ni mwovu sana, sasa inawezekanaje mtu yeyote avumilie uwepo wa Mungu? Ndiyo maana duniani Mungu yuko kimya siku zote. Haijalishi mwanadamu ni katili kiasi gani, Mungu haathiriwi nayo, bali Anaendelea tu kufanya kazi Anayotaka kuifanya ili kutimiza agizo kuu ambalo Baba wa mbinguni Alimpatia. Ni nani miongoni mwenu ametambua uzuri wa Mungu? Ni nani anayejali sana mzigo Alio nao Mungu Baba kuliko Mwana Wake Anavyofanya? Ni nani awezaye kuelewa mapenzi ya Mungu Baba? Roho wa Mungu Baba aliye mbinguni Anasumbuka kila mara, na Mwana Wake duniani Anaomba mara kwa mara juu ya mapenzi ya Mungu Baba, Akihofu sana. Kuna mtu yeyote anayejua kuhusu upendo wa Mungu Baba kwa Mwana Wake? Kuna mtu yeyote anayejua jinsi ambavyo Mwana mpendwa Anavyomkumbuka Mungu Baba? Wakipata shida ya kuchagua kati ya mbingu na nchi, wote wawili wanatazamana kutoka mbali, sambamba katika Roho. Ee wanadamu! Ni lini mtaufikiria moyo wa Mungu? Ni lini mtaielewa nia ya Mungu? Baba na Mwana siku zote Wamekuwa Wakitegemeana. Kwa nini basi Watenganishwe, mmoja juu mbinguni na mmoja chini duniani? Baba anampenda Mwana Wake kama vile Mwana anavyompenda Baba Yake. Kwa nini basi Anapaswa kusubiri kwa shauku hivyo na kwa muda mrefu huku Akiwa na hamu hivyo? Ingawa kwa muda mrefu, je, mtu yeyote anajua kwamba Baba tayari Amekuwa Akitaka sana kwa shauku kwa siku nyingi na Amekuwa Akitarajia kwa muda mrefu kurudi haraka kwa Mwana Wake mpendwa? Anatazama, Anakaa kwa utulivu, Anasubiri. Haya yote ni kwa ajili ya kutaka Mwana Wake mpendwa Arudi haraka. Ni lini Atakuwa tena na Mwana ambaye Anazungukazunguka duniani? Ingawa watakapokuwa pamoja tena, Watakuwa pamoja milele, Anawezaje kustahimili maelfu ya siku za utengano, mmoja juu mbinguni na mwingine chini duniani. Makumi ya miaka duniani ni kama maelfu ya miaka mbinguni. Mungu Baba anawezaje kutokuwa na wasiwasi? Mungu anapokuja duniani, Anapitia mabadiliko mengi ya ulimwengu wa kibinadamu jinsi mwanadamu anavyopitia. Mungu Mwenyewe hana hatia, hivyo kwa nini kumruhusu Mungu ateseke maumivu kama mwanadamu? Si ajabuMungu Baba Anatamani sana Mwana Wake Arudi haraka; nani awezaye kuuelewa moyo wa Mungu? Mungu humpa mwanadamu vitu vingi sana; mwanadamu anawezaje kuulipa moyo wa Mungu kikamilifu? Lakini mwanadamu anampatia Mungu kidogo sana; kwa hivyo Mungu angewezaje kutokuwa na wasiwasi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (4)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp