Wimbo wa Dini | Mungu Hutumaini Mtu Anaweza Kumjua na Kumwelewa

14/01/2020

I

Tangu uhusiano wa kwanza wa Mungu na mwanadamu,

Amekuwa akifichua kwao

Kiini Chake na vile Alivyo na Alicho nacho, bila kukoma, kila wakati.

Kama watu katika enzi wanaweza kuona au kuelewa,

Mungu huzungumza na kufanya kazi ili kuonyesha tabia Yake na kiini.

Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita,

Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake,

vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.

II

Mungu anatumaini mwanadamu aweza kumwelewa, ajue kiini Chake, na tabia,

ambavyo Hataki vichukuliwe kama siri za milele.

Wala Hataki mwanadamu amwone Yeye

kama kitendawili ambacho hakiwezi kutatuliwa.

Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita,

Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake,

vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.

III

Ni wakati tu binadamu amemjua Mungu

ndipo anaweza kujua njia ya kwendelea, kustahili kuongozwa na Mungu.

Ataishi chini ya mamlaka Yake na kuishi katika mwanga na baraka Zake.

Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita,

Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake.

Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita,

Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake,

vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp