Christian Testimony Video | Maneno ya Mungu Yalinifanya Nijijue (Swahili Subtitles)

17/07/2020

Kabla ya mhusika mkuu kuwa muumini, alikuwa akiamini kila wakati kwamba alikuwa mtu mwenye ubinadamu mzuri, mvumilivu na mstahimilivu kwa wengine, mtu ambaye angefanya chochote alichoweza ili kusaidia kila alipomwona mtu akipitia wakati mgumu; alijiona kuwa mtu mzuri. Baada ya kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, kwa kufunuliwa na ukweli na kupitia ufunuo na hukumu ya maneno ya Mungu, anaona kwamba ingawa anaonekana kuwa mwenye tabia nzuri kwa nje na anaepuka kutenda dhambi za wazi, ndani mwake kuna tabia za kishetani za kiburi, udanganyifu, na uovu. Punde maneno au matendo ya mtu yanapoathiri masilahi yake mwenyewe, yeye humchukia na kumhukumu, akimdhoofisha pasi na yeye kujua, na yeye husababisha usumbufu katika kazi ya kanisa. Mara anapopata ufahamu juu ya tabia yake potovu na asili yake ya kishetani ya kumpinga Mungu, anaanza kutubu kwa Mungu…

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp