Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Swahili Gospel Song | "Njia Yote Pamoja na Wewe" Mungu ni Upendo

Mfululizo wa Video za Muziki   2336  

Utambulisho

Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini.

Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza.

Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako,

nina amani kabisa.

Unanibariki, Unatoa maneno Yako ya hukumu.

Bado sijui jinsi ninavyokosa kuithamini neema Yako.

Kila mara nikiasi, kwa namna fulani nikiuumiza moyo Wako.

Na bado Hunitendei kulingana na dhambi

zangu lakini Unafanya kazi kwa ajili ya wokovu wangu.

Ninapokuwa mbali, Unaniita nirudi kutoka hatarini.

Ninapoasi, Unauficha uso Wako, giza likinifunika.

Ninaporudi Kwako,

Unaonyesha neema, Unatabasamu ili kukumbatia.

Shetani anaponipiga,

Unatibu vidonda vyangu, Unaupa joto moyo wangu.

Shetani anaponiumiza,

Uko nami kuanzia mwanzo hadi mwisho wa majaribu.

Alfajiri itafika karibuni,

na anga itang’aa samawati kama awali,

wakati Uko nami.

Alfajiri itafika karibuni,

anga itang’aa samawati kama awali,

wakati Uko nami.


Wewe ni uhai wangu, Wewe ni Bwana wangu.

Mwenzi wa kila siku, kivuli cha karibu kando yangu.

Ukinifunza jinsi ya kuwa binadamu

na kunipa ukweli na uhai.

Pamoja na Wewe maisha yangu yanasonga mbele kwa utukufu .

Bila chaguo langu, natii amri Yako.

Kuwa kiumbe wa kweli, narudi upande Wako.

Kuishi katika uwepo Wako,

nazungumza na Wewe na kusikia sauti Yako.

Hutangoja tena katika umbali mpweke.

Pamoja na Wewe, hakuna kuogopa dhoruba.

Usiku unaponifunika, siko pekee yangu tena.

Pamoja na Wewe kando yangu,

hatari au matatizo, naweza kuvikabili.

Pamoja na Wewe, safari hazitakuwa ngumu sana.

Njia zenye mabonde zinapita katika matatizo,

zinafungua njia kwenda kwa chemichemi ya kupendeza.

Alfajiri itafika karibuni,

anga itang’aa samawati kama awali,

wakati Uko nami.

Pamoja na Wewe, hakuna kuogopa dhoruba tena.

Usiku unaponifunika, siko pekee yangu tena.

Pamoja na Wewe kando yangu,

hatari na matatizo, naweza kuvikumba.

Pamoja na Wewe, safari haziwezi kuwa ngumu sana.

Njia zenye mabonde zinapita katika matatizo,

zinafungua njia kwenda kwa chemichemi ya kupendeza.

Alfajiri itafika karibuni,

anga itang’aa samawati kama awali.

Niko pamoja na Wewe.


kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Uimbe Nyimbo Mpya

Pakua Programu Bila Malipo

Video za Ajabu Zakuongoza Kuielewa Kazi ya Mungu

Pakua Programu Bila Malipo

Video za Ajabu Zakuongoza Kuielewa Kazi ya Mungu