Christian Praise Choral Work | “Mungu Atarudisha Hali ya Kitambo ya Uumbaji”
02/07/2017
Wanadamu Ameupata tena Utakatifu Wao Waliokuwa Nao Awali
1 Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, mwanadamu amepata tena utakatifu aliokuwa nao wakati mmoja. Eh, dunia potovu ya zamani! Mwishowe, imeanguka na kutumbukia ndani ya maji machafu na, imezama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu? Wanawezaje, katika mwanga, kukosa kuendeleza kazi zao? Dunia si kimya cha mauti na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena.
2 Mbingu na nchi, bila kutenganishwa na utupu tena, zimeungana kama kitu kimoja, kamwe kutotenganishwa tena. Katika wakati huu wa shangwe, wakati huu wa nderemo, haki Yangu na utakatifu Wangu umeenea katika kila pembe ya ulimwengu, na binadamu wote wanavisifu bila kikomo. Miji yote ya mbingu inacheka kwa furaha, na falme zote za nchi zinacheza kwa shangwe. Ni nani wakati huu ambaye haonyeshi furaha? Na ni nani wakati huu ambaye halii? Nchi katika hali yake ya asili ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wa mwanadamu, kwa ajili ya kufanywa upya kwa mwanadamu, mbingu haijafichwa tena kutoka kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu. Nyuso za binadamu zimezingirwa na tabasamu za shukurani, na nyoyo zao zinadondokwa na utamu usiokuwa na kifani. Mwanadamu hagombani na mwanadamu, wala binadamu kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kunao wale ambao, katika mwanga Wangu, hawaishi kwa furaha na wenzao? Kunao wale ambao, katika siku Yangu, hulifedhehesha jina Langu?
3 Watu wote huelekeza macho yao ya heshima Kwangu, na wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao. Nimechunguza kila kitendo cha binadamu: Miongoni mwa wanadamu waliotakaswa, hakuna yeyote aliye mkaidi Kwangu, hakuna anayenielekezea hukumu. Binadamu wote umejawa na tabia Yangu. Kila mtu anakuja kunijua, ananijongelea, na ananiabudu. Msimamo wangu ni mmoja katika roho ya mwanadamu, Nimetukuzwa kwa kiwango cha juu zaidi kwa macho ya mwanadamu, na hububujika katika damu ya mishipa yake. Nderemo za furaha katika nyoyo za wanadamu huenea kila sehemu ya uso wa nchi, hewa ni ya kuchangamsha na bichi, ukungu mzito hauitandai ardhi tena, na mwangaza wa jua huvutia.
Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 18” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video