Swahili Christian Testimony Video | Siku za Kutafuta Umaarufu na Faida

21/06/2020

Siku za Kutafuta Umaarufu na Faida ni ushuhuda wa Mkristo anayepitia hukumu na kuadibiwa na Mungu. Kwa sababu ya hamu ya mhusika mkuu kutaka kutafuta umaarufu na hadhi huku akitimiza wajibu wake, anapoona kwamba Ndugu Li amechaguliwa kuwa kiongozi wa timu badala yake, anahisi kutoridhika, na anaanza kupingana naye kwa siri. Hata anapanga njama ya kutomhusisha ili apate nafasi yake mwenyewe ya kujionyesha, na anawakaripia ndugu zake wengine kwa kiburi. Hili linawafanya wahisi kuzuiliwa, na linawadhuru; kwa sababu hiyo, kazi ya kanisa inakatizwa, na yeye mwenyewe anaumia. Ni baada tu ya yeye kupitia hukumu na kuadibiwa na maneno ya Mungu ndipo hatimaye anapata ufahamu kiasi wa tabia yake potovu. Anatambua kiini na matokeo ya kutafuta hadhi na fahari kuu, na ni hapo tu ndipo mwishowe anaanza kugutuka na kuhisi majuto. Hatamani tena kufuatilia vitu hivi, na badala yake anaanza kulenga kutenda ukweli na kumridhisha Mungu. Mwishowe, anafanikiwa kufikia hali ya amani na uthabiti ambavyo hajawahi kuhisi hapo awali.

Baadhi ya taarifa katika video hii zinatoka kwa: 【ESO】

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp