Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 468

02/11/2020

Watu wanafaa kushirikiana na Mungu vipi katika hatua hii ya kazi Yake? Mungu Anawajaribu watu kwa wakati huu. Haneni neno lolote; Anajificha na Hawasiliani na watu moja kwa moja. Kutoka nje, inaonekana kama Hafanyi kazi, lakini ukweli ni kwamba bado Anafanya kazi ndani ya mwanadamu. Yeyote anayefuatilia kuingia katika maisha ana maono kwa kufuata kwake maisha, na hana mashaka, hata kama haelewi kazi ya Mungu kikamilifu. Katikati ya majaribu, hata kama hajui ni nini Mungu Anataka kufanya na kazi gani Anataka kukamilisha, unafaa kujua kuwa nia za Mungu kwa wanadamu ni nzuri kila wakati. Ukimfuata na moyo wa kweli, Hatawahi kukuacha, na mwishowe kwa kweli Atakukamilisha, na kuwaleta watu katika mwisho unaofaa. Haijalishi ni vipi Mungu Anawajaribu watu kwa sasa, kuna siku moja ambayo Atawatolea watu matokeo yanayofaa na kuwapa adhabu inayofaa kulingana na kile ambacho wamefanya. Mungu Hatawaongoza watu hadi kituo fulani halafu Awatupe tu kando na kuwapuuza. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu mwaminifu. Katika hatua hii, Roho Mtakatifu anafanya kazi ya usafishaji. Anamsafisha kila mmoja. Katika hatua za kazi zilizoundwa na majaribu ya kifo na majaribu ya kuadibu, usafishaji katika wakati huo ulikuwa usafishaji kupitia maneno. Ili watu wapate uzoefu wa kazi ya Mungu, lazima kwanza waelewe kazi Yake ya sasa na kuelewa jinsi wanadamu wanafaa kushirikiana. Hili ni jambo ambalo kila mtu anafaa kuelewa. Haijalishi ni nini Mungu Anafanya, kama ni usafishaji ama kama Haneni, kila hatua ya kazi ya Mungu hailingani na dhana za wanadamu. Yote yanaenda mbali na kupenya katika dhana za watu. Hii ni kazi Yake. Lakini lazima uamini kwamba, kwa kuwa kazi ya Mungu imefika hatua fulani, Hatakubali wanadamu wote waangamie hata iweje. Anawapa ahadi na baraka kwa wanadamu, na wale wote wanaomfuata wataweza kupata baraka Yake, na wale wasiomfuata watatupwa nje na Mungu. Hii inategemea kufuata kwako. Haijalishi chochote, lazima uamini kuwa wakati kazi ya Mungu itakapomalizika, kila mtu atakuwa na mwisho unaofaa. Mungu Amewapa wanadamu matamanio mazuri, lakini wasipofuatilia, hawawezi kuyapata. Unafaa kuweza kuona hii sasa—Mungu kusafisha na kuwaadibu watu ni kazi Yake, lakini kwa watu, lazima wafuate badiliko katika tabia kila wakati. Katika mazoea yako ya kivitendo, lazima kwanza ujue jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu; lazima upate kile unachofaa kuingia ndani na mapungufu yako ndani ya maneno Yake, utafute kuingia katika mazoea yako ya kivitendo, na uchukue sehemu ya kazi ya Mungu inayofaa kuwekwa katika matendo na ujaribu kuifanya. Kula na kunywa maneno ya Mungu ni kipengele kimoja, maisha ya kanisa lazima pia yadumishwe, lazima uwe na maisha ya kiroho ya kawaida, na uweze kumkabidhi Mungu hali zako zote za sasa. Haijalishi ni vipi kazi Yake inabadilika, maisha yako ya kiroho yanapaswa kubaki kawaida. Maisha ya kiroho yanaweza kudumisha kuingia ndani kwako kwa kawaida. Haijalishi kile ambacho Mungu Anafanya, unapaswa kuendeleza maisha yako ya kiroho bila kukatizwa na kutimiza wajibu wako. Hiki ndicho watu wanapaswa kufanya. Yote ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini huku kwa wale walio na hali ya kawaida huku ni kukamilishwa, kwa wale wasio na hali ya kawaida ni majaribu. Katika hatua ya sasa ya kazi ya Roho Mtakatifu ya kusafisha, watu wengine wanasema kuwa kazi ya Mungu ni kubwa sana na kwamba watu wanahitaji sana usafishaji, vinginevyo kimo chao kitakuwa ndogo sana na hawatakuwa na njia ya kufikia mapenzi ya Mungu. Hata hivyo, kwa wale walio na hali isiyo nzuri, inakuwa sababu ya kutomfuata Mungu, na sababu ya kutohudhuria mikusanyiko ama kula na kunywa neno la Mungu. Katika kazi ya Mungu, haijalishi ni nini Anafanya ama nini kinabadilika, kwa uchache sana watu lazima watu wadumishe hali ya chini zaidi ya maisha ya kawaida ya kiroho. Pengine umekuwa mwangalifu katika hatua hii ya sasa ya maisha yako ya kiroho, lakini bado hujapata mengi; hujavuna pakubwa. Katika hali za aina hizi lazima bado ufuate sheria; lazima ufuate sheria hizi ili usipate hasara katika maisha yako na ili uyakidhi mapenzi ya Mungu. Kama maisha yako ya kiroho si ya kawaida, huwezi kuelewa kazi ya sasa ya Mungu, badala yake kila wakati utahisi kwamba hayalingani kabisa na dhana zako mwenyewe, nawe una hiari ya kumfuata, lakini unakosa bidii ya ndani. Kwa hivyo haijalishi ni nini Mungu Anafanya sasa, lazima watu washirikiane. Watu wasiposhirikiana Roho Mtakatifu Hawezi kufanya kazi Yake, na kama watu hawana moyo wa kushirikiana, basi si rahisi wao kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Kama unataka kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani mwako, na kutaka kupata kibali cha Mungu, lazima udumishe moyo wako wa ibada asili mbele ya Mungu. Sasa, si lazima kwako kuwa na maelewano zaidi ya ndani, nadharia ya juu, ama vitu vingi—yote yanayohitajika ni kwamba ushikilie neno la Mungu juu ya msingi asili. Watu wasiposhirikiana na Mungu na wasipofuata kuingia zaidi, Mungu Atachukua kile walichokuwa nacho wakati mmoja. Ndani, watu wana tamaa kila wakati ya kilicho rahisi na afadhali wajifurahishe na kile ambacho kinapatikana. Wanataka kupata ahadi za Mungu bila kulipa gharama yoyote. Haya ni mawazo badhirifu ndani ya wanadamu. Kupata maisha yenyewe bila kulipa gharama—nini kimewahi kuwa rahisi? Mtu anapoamini katika Mungu na kutafuta kuingia katika maisha na kutafuta badiliko katika tabia yake, ni lazima alipe gharama na kufikia kiwango ambapo atamfuata Mungu daima bila kujali Anachofanya. Hiki ni kitu ambacho watu lazima wafanye. Hata kama unafuata haya yote kama sharti, ni lazima uyazingatie, na haijalishi majaribu yako ni makubwa kiasi gani, huwezi kuachilia uhusiano wako wa kufaa na Mungu. Unapaswa kuweza kuomba, udumishe maisha yako ya kanisa, na uishi na ndugu na dada. Mungu anapokujaribu, bado unapaswa kutafuta ukweli. Hiki ndicho kiwango cha chini cha maisha ya kiroho. Daima kuwa na moyo wa kutafuta na kujitahidi kushirikiana, kutumia nguvu zako zote—Je, hili linaweza kufanywa? Kwa msingi huu, utambuzi na kuingia katika uhalisi kitakuwa kitu ambacho unaweza kufanikisha. Ni rahisi kulikubali neno la Mungu wakati hali yako mwenyewe iko kawaida, na huhisi ugumu katika kuuweka ukweli katika matendo, na unahisi kuwa kazi ya Mungu ni kuu. Lakini kama hali yako ni duni, haijalishi kazi ya Mungu ni kuu vipi na haijalishi mtu anazungumza vizuri kivipi, hutasikiza chochote. Wakati hali ya mtu si ya kawaida, Mungu hawezi kufanya kazi ndani yao, na hawawezi kufanikisha mabadiliko katika tabia zao.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp