Wimbo wa Kikristo | Eh Mungu! Sistahili Upendo Wako Kweli

11/02/2020

Nimefanya mambo mengi ambayo siwezi kustahimili kukumbuka.

Nilizembea na kupoteza muda mwingi sana.

Majuto mengi sana na hisia za deni ndani zinajaa moyoni mwangu.

Siku zote nilidai thawabu nilipostahimili kujituma kwa ajili ya Mungu.

Hamu yangu ya kupokea baraka ilipozuiwa, nilifikiria kumwacha Mungu,

lakini upendo Wake ulikuwa bado wazi katika akili yangu na ulikuwa mwingi kusahau.

Maneno ya Mungu yaliugonga moyo wangu,

yakiniondoa katika kurudi nyuma na uhasi hatua baada ya nyingine.

Shida zilipotishia, niliogopa, mwepesi kutishiwa na kutishwa.

Nilikuwa dhaifu na hasi na tena nilifikiria kumwacha Mungu.

Maneno Yake yaliupasua moyo wangu kama upanga mkali wenye makali kuwili,

yakiniacha bila mahali pa kuficha aibu yangu.

Zamani nilikimbia huku na kule nikitafuta umaarufu, utajiri na hadhi,

nikishindwa kupinga majaribu ya Shetani.

Mara kadhaa nilikuwa na wasiwasi,

nikasita na kupoteza mwelekeo maishani.

Nilijitahidi kwa uchungu dhambini, bila kujua jinsi ya kurudi nyuma.

Eh Mungu! Huyu ndiye niliye! Huyu ndiye niliye!

Mpotovu sana, sistahili wokovu Wako.

Eh Mungu! Ni neno Lako liniongozalo na kunielekeza,

la sivyo ningeanguka katika majaribu na nipambane kuchukua hatua ndogo zaidi.

Eh Mungu! Sitawahi tena kuwa hasi au kurudi nyuma.

Usiniache, siwezi kuishi bila Wewe.

Eh Mungu! Naomba Unipe kuadibu, hukumu na usafishaji Wako,

ili upotovu Wangu uweze kutakaswa, na niweze kuishi kama binadamu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp