Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kazi na Kuingia (10) | Dondoo 197

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kazi na Kuingia (10) | Dondoo 197

209 |14/08/2020

Mungu kupata mwili imesababisha mawimbi mazito katika vikundi na madhehebu yote, “imeparaganya” mpangilio wao wa awali, na imetikisa mioyo ya wale wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu. Ni nani asiyeabudu? Nani hatamani kumwona Mungu? Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi, lakini mwanadamu kamwe hajawahi kutambua. Leo, Mungu mwenyewe Amejitokeza, na Ameonyesha kwa watu—inawezekanaje hii isiufurahishe moyo wa mwanadamu? Mungu aliwahi kushiriki furaha na huzuni pamoja na mwanadamu, na leo Ameunganika tena na mwanadamu, na Anashiriki visa vya muda uliopita Akiwa pamoja naye. Baada ya kutoka Uyahudi, watu hawakuweza Kumwona tena. Wanatamani kukutana na Mungu tena, bila kujua kwamba leo wamekutana naye tena, na kuungana naye tena. Inawezekanaje hii isiamshe mawazo ya jana? Siku kama ya leo miaka elfu mbili iliyopita, Simoni wa Yona, uzao wa Wayahudi, alimtazama Yesu Mwokozi, alikula meza moja naye, na baada ya kumfuata kwa miaka mingi alihisi kumpenda sana: Alimpenda sana kutoka moyoni mwake, alimpenda sana Bwana Yesu. Wayahudi hawakujua jinsi mtoto huyu mwenye nywele za dhahabu, Aliyezaliwa katika hori la ng’ombe lililo baridi, Alikuwa sura ya kwanza ya Mungu kupata mwili. Wote walidhani kwamba Alikuwa mmoja wao, hakuna aliyemfikiria kuwa tofauti—watu wangewezaje kumtambua Yesu huyu wa kawaida? Wayahudi walidhani kwamba alikuwa ni mtoto wa Kiyahudi wa wakati huo. Hakuna aliyemtazama kama Mungu mwenye upendo, na watu walitoa masharti Kwake tu bila kufikiri, wakiomba Awape neema nyingi, na amani, na furaha. Walijua tu kwamba, kama milionea, Alikuwa na kila kitu ambacho mtu angetamani kuwa nacho. Lakini watu hawakumchukulia kama mtu ambaye Alikuwa mpendwa; watu wa wakati huo hawakumpenda, na walimpinga tu, na walitoa masharti yasiyokuwa na mantiki kutoka Kwake, na Hakuwahi kupinga, Aliendelea kutoa neema kwa mwanadamu, hata ingawa mwanadamu hakumjua. Hakufanya chochote isipokuwa kwa kimya kumpatia mwanadamu wema, upendo, na huruma, na hata zaidi, Alimpatia mwanadamu njia mpya ya kutenda, Akimwondoa mwanadamu kutoka katika vifungo vya sheria. Mwanadamu hakumpenda, alimhusudu tu na kutambua talanta Zake za kipekee. Wanadamu vipofu wangejuaje jinsi ambavyo Yesu Mwokozi Alipitia mateso makubwa Alipokuja miongoni mwa wanadamu? Hakuna aliyejali dhiki Zake, hakuna mtu aliyejua upendo Wake kwa Mungu Baba, na hakuna ambaye angeweza kujua kuhusu upweke Wake; hata ingawa Maria alikuwa mama Yake wa kumzaa, angewezaje kujua mawazo yaliyokuwa moyoni mwa Bwana Yesu mwenye huruma? Nani alijua mateso yasiyoelezeka Aliyoyapitia Mwana wa Adamu? Baada ya kutoa masharti Kwake, watu wa kipindi hicho walimsahau bila huruma, na kumtupa nje. Basi Alizungukazunguka mitaani, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, Akienda bila mwelekeo kwa miaka mingi hadi Alipofikisha miaka thelathini na mitatu, miaka ambayo ilikuwa mirefu na mifupi. Watu walipomhitaji, walimwalika nyumbani mwao wakiwa na nyuso za tabasamu, wakijaribu kutoa masharti Kwake—na baada Yake kuwasaidia, walimsukuma nje ya mlango mara moja. Watu walikula Alichokitoa mdomoni Mwake, walikunywa damu Yake, walifurahia neema Alizowapatia, lakini bado walimpinga, maana hawakuwahi kujua nani aliyewapa uhai wao. Hatimaye, walimsulubisha msalabani, lakini bado Hakutoa sauti. Hata leo, bado Anabakia kimya. Watu wanakula mwili Wake, wanakula chakula Anachowatengenezea, wanapita njia ambayo Ameifungua kwa ajili yao, na wanakunywa damu Yake, lakini bado wanakusudia kumkataa, kimsingi wanamchukulia Mungu ambaye Amewapa maisha yao kama adui, na badala yake wanawachukulia wale ambao ni watumwa kama wao jinsi walivyo kama Baba wa mbinguni. Katika hili, je, hawampingi kwa makusudi? Yesu aliwezaje kufa msalabani? Je, mnajua? Je, Hakusalitiwa na Yuda, ambaye alikuwa karibu kabisa naye, na alikuwa amemla, akamnywa, na akamfurahia? Je, sababu ya usaliti wa Yuda haikuwa kwa sababu Yesu alikuwa tu mwalimu mdogo wa kawaida? Ikiwa watu walikuwa wameona kweli kwamba Yesu hakuwa wa kawaida, na Ambaye Alitoka mbinguni, wangewezaje kumsulubisha msalabani Akiwa hai kwa masaa ishirini na manne, hadi Alipoishiwa na pumzi katika mwili wake? Nani awezaye kumjua Mungu? Watu wanamfurahia Mungu tu kwa tamaa isiyotosheka, lakini hawajawahi kumjua. Walipewa inchi na wamechukua maili, na wanamfanya Yesu kutii kabisa amri zao, maelekezo yao. Nani ambaye amewahi kuonyesha huruma kwa Mwana wa Adamu huyu, Ambaye hana mahali pa kuweka kichwa Chake? Nani ambaye amewahi kufikiria kuungana naye ili kukamilisha agizo la Mungu Baba? Ni nani ambaye amewahi kumuwaza? Ni nani mbaye amewahi kuyajali matatizo Yake? Bila upendo hata kidogo, mwanadamu anamvuta nyuma na mbele; mwanadamu hajui nuru na uhai wake vinatoka wapi, na anapanga kwa siri tu jinsi ya kumsulubisha tena Yesu wa miaka elfu mbili iliyopita, ambaye amepitia uzoefu wa maumivu miongoni mwa wanadamu. Je, Yesu anawatia anachochea chuki ya namna hiyo? Je, yote Aliyoyafanya yamesahaulika kitambo? Chuki ambayo ilichanganyika kwa maelfu ya miaka itaibuka tena. Nyinyi tabaka la Wayahudi! Yesu amewahi kuwa adui kwenu lini, hadi mmchukie kiasi hicho? Amefanya mengi sana, na kuzungumza mengi sana—je, hakuna chochote chenye manufaa kwenu? Ameyatoa maisha Yake kwenu bila kutazamia kulipwa chochote, Amejitoa mzima kwenu—kweli bado mnataka kumla Akiwa mzima? Amejitoa kwenu kikamilifu bila kuacha kitu chochote, bila kufurahia utukufu wa kidunia, wema miongoni mwa wanadamu, na upendo miongoni mwa wanadamu, au baraka zote miongoni mwa wanadamu. Watu ni wachoyo sana Kwake, Hajawahi kufurahia utajiri wote duniani, Anautoa moyo Wake wote, wa upendo na dhati, kwa mwanadamu, Amejitoa Yeye mzima kwa mwanadamu—na nani ambaye amemfanyia wema? Ni nani aliyewahi kumpatia faraja? Mwanadamu amemjazia mashinikizo yote, balaa yote amempatia Yeye, Amejitwika shida zote mbaya kati ya wanadamu, anamtupia lawama kwa uonevu wote, na Ameikubali kimyakimya. Je, Amewahi kumpinga mtu yeyote? Je, Amewahi kuomba fidia hata ndogo kutoka kwa mtu yeyote yule? Nani amewahi kuonyesha huruma yoyote Kwake? Kama watu wa kawaida, ni nani miongoni mwenu ambaye hakuwa na kipindi cha utotoni chenye mapenzi ya dhati? Ni nani ambaye hakuwa na ujana wa kupendeza? Ni nani ambaye hana joto la wapendwa? Ni nani ambaye hana upendo wa jamaa na marafiki? Ni nani ambaye haheshimiwi na wengine? Ni nani ambaye hana familia yenye upendo? Ni nani ambaye hana faraja ya wandani wake? Je, Amewahi kufurahia yote kati ya haya? Ni nani ambaye amewahi kumtendea wema hata kidogo? Ni nani ambaye amewahi kumpa faraja hata kidogo? Ni nani ambaye amewahi kumwonyesha angalau maadili kidogo ya kibinadamu? Ni nani ambaye amewahi kuwa mvumilivu Kwake? Ni nani ambaye amewahi kuwa pamoja naye katika nyakati za shida? Ni nani ambaye amewahi kupitia maisha ya shida pamoja naye? Mwanadamu hajawahi kulegeza matakwa yake Kwake; anatoa masharti Kwake tu bila hata haya, kana kwamba kwa kuwa Amekuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Anapaswa kuwa ng’ombe au farasi wake, mtumwa wake, na Anapaswa kumpa mwanadamu kila kitu Chake; Asipofanya hivyo, mwanadamu hatawahi kumsamehe, hatawahi kumtendea vyema, hatawahi kumwita Mungu, na hatawahi kumheshimu. Mwanadamu ni katili sana katika mtazamo wake kwa Mungu, kana kwamba ana nia ya kumtesa Mungu hadi kifo, ni baada ya hapo tu ndipo atapunguza masharti yake kwa Mungu; kama sivyo, mwanadamu hatapunguza kiwango cha matakwa yake kwa Mungu. Inawezekanaje mwanadamu kama huyu asidharauliwe na Mungu? Je, hili si janga la siku hizi? Dhamiri ya mwanadamu haionekani. Anasema tu ataulipiza upendo wa Mungu, lakini anamchanachana Mungu na kumtesa hadi kifo. Je, hii sio “mbinu ya siri” kwa imani yake kwa Mungu, iliyorithishwa kutoka kwa mababu zake? Hakuna mahali popote ambapo “Wayahudi” hawapatikani, na leo bado wanafanya kazi ile ile, bado wanafanya kazi ile ile ya kumpinga Mungu, na bado wanaamini kwamba wanamheshimu Mungu. Inawezekanaje macho ya mwanadamu yamjue Mungu? Inawezekanaje mwanadamu, anayeishi katika mwili, kumchukulia Mungu kama Mungu mwenye mwili ambaye Amekuja kutokana na Roho? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kumjua? Ukweli uko wapi miongoni mwa wanadamu? Haki ya kweli iko wapi? Ni nani anayeweza kuijua tabia ya Mungu? Ni nani anayeweza kushindana na Mungu mbinguni? Haishangazi kwamba, Alipokuja miongoni mwa wanadamu, hakuna aliyemjua Mungu, na amekataliwa. Mwanadamu anawezaje kuvumilia kuwepo kwa Mungu? Anawezaje kuruhusu mwanga kuliondosha giza la ulimwengu? Je, hii yote si kujitoa kwa heshima kwa mwanadamu? Je, huku sio kuingia adilifu kwa mwanadamu? Na kazi ya Mungu haijajikita katika kuingia kwa mwanadamu? Ningependa muunganishe kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu, na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya mwanadamu na Mungu, na kutekeleza jukumu ambalo linapaswa kutekelezwa na mwanadamu kadri ya uwezo wake. Kwa njia hii, kazi ya Mungu hatimaye itafikia mwisho, ikimalizika na utukufu Wake!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi