Ushuhuda wa Kweli | Kuishi Mbele za Mungu

22/07/2020

Watu wengi hulenga tu maombi, kuhudhuria mikutano, na kusoma maneno ya Mungu katika imani yao. Wanakosa kuhusisha maneno ya Mungu na maisha halisi, na hivyo kupoteza fursa nyingi za kupata ukweli. Mhusika mkuu katika video hii analenga kuishi mbele za Mungu. Anachunguza mawazo na matendo yake mwenyewe kutoka ndani ya maneno ya Mungu, na anapofichua upotovu, anatafuta ukweli ili kuutatua upotovu huo. Anapotenda kwa njia hii, ingawa anaweza kukabiliwa tu na mambo kadhaa madogo maishani yasiyo ya ajabu, bado anapata ufahamu fulani na kuvuna matunda. Kwa hivyo ni vipi hasa anavyoshirikisha maneno ya Mungu katika maisha ya kila siku?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp