Swahili Christian Testimony Video | Kuishi kwa Kudhihirisha Mfano Kidogo wa Mwanadamu Hakika Ni Vizuri

05/06/2020

Kuishi kwa Kudhihirisha Mfano mdogo wa Mwanadamu Hakika Ni Vizuri ni ushuhuda wa Mkristo anayepitia hukumu na kuadibiwa na maneno ya Mungu. Mhusika mkuu anachukua wajibu wa kuwa mwelekezi wa filamu katika kanisa lake na baada ya kuona kazi yake ikipata matokeo kiasi, anaanza kuhisi kuwa yeye ni mtu mwenye kipaji muhimu. Tabia yake inazidi kuwa ya kiburi: Kila wakati anataka kuwa na kauli ya mwisho katika wajibu wake na anakataa kuyasikiliza mapendekezo ya kina ndugu. Yeye pia anawazungumzia wengine kwa njia inayomwonyesha kuwa bora, anawazuia ndugu zake na kuvuruga kazi ya kanisa. Baada ya kuondolewa kutoka katika wajibu wake, kupitia kusoma maneno ya Mungu na kutafakari kujihusu, anapata ufahamu kiasi kuhusu asili yake ya kishetani ya kiburi na majivuno, na yeye si fidhuli tena kama alivyokuwa hapo awali. Anapokabili maswala, anatafuta ukweli kimakusudi na kusikiza maoni ya wengine, na mwishowe anaishi kwa kudhihirisha mfano kidogo wa binadamu. Yeye mwenyewe anapata uzoefu kwamba hukumu ya Mungu na kuadibu Kwake ni upendo wa kweli wa Mungu na wokovu Wake kwa wanadamu.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp