Wimbo wa Kikristo | Hakuna Mwanadamu Awezaye Kufanya Kazi ya Mungu Badala Yake

06/07/2020

Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe,

inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe.

Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu— ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe,

na kama haikuwa hivyo,

basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu;

awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote,

na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe,

awamu ya tatu inaenda bila kusemwa:

Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe.

Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu

wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe.

Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu,

na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani,

Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu;

kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote,

ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii.

Yehova mwenyewe alimuumba mwanadamu na kumwainisha kila mmoja kulingana na aina

na siku ya mwisho itakapowadia bado Atafanya kazi Yake Mwenyewe,

kuanisha kila kitu kulingana na aina—hili haliwezi kufanywa na mwingine isipokuwa Mungu.

Ukweli wa hatua tatu za kazi

ni ukweli wa uongozi wa Mungu kwa wanadamu wote,

ukweli ambao hakuna anayeweza kuupinga.

Mwishoni mwa hatua tatu za kazi,

vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina

na kurejea chini ya utawala wa Mungu.

Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe,

na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake,

ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo.

Ingawa hatua tatu za kazi ya Mungu

zimefanywa katika enzi tofauti na maeneo tofauti,

na ingawa kazi ya kila moja ni tofauti,

yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja.

Kati ya maono yote,

hili ndilo kuu zaidi ambalo mwanadamu anapaswa kulijua.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp